Zitto na ushahidi wake Bungeni (Mawaziri kushawishiwa kutoa maamuzi)

"Kama watanzania msipokuwa makini litakuja genge la wahuni litamobilize watu, likatwaa uongozi wa nchi, likatawala kihuni" JKN
ccm magamba mlioko humu JF tena kama mchwa semeni. Nawaombeni mlete hotuba za mwenyekiti wenu wa kwanza JKNyerere tuzijadili kama kweli mnatetea maslahi ya nchi, kama alivyokuwa yeye. Tuanze kujadili nukuu hiyo hapo juu. wahunina uhuni mtupu ccm.
 
HATMA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliyelituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa kubadili msimamo wa kubariki azimio la kuongeza muda wa uhai kwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa miaka mitatu kinyume cha mapendekezo ya Bunge itajulikana leo.


Hatua hiyo inatokana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumwagiza Zitto kuwasilisha utetezi wake hadi kufikia leo baada ya agizo lake la mara ya kwanza alilolitoa Juni 23 kumtaka mbunge huyo kuwasilisha utetezi huo hadi kufikia Juni 29 kugonga mwamba.


Hata hivyo, ulishindwa kutolewa uamuzi siku hiyo (Juni 29) baada ya siku ya kwanza ambayo Zitto alitakiwa kuthibitisha kauli yake kuwasilisha barua kwa Spika akiomba amsaidie kupata nyaraka kutoka Baraza la Mawaziri na Wizara ya Fedha zinazohusu mjadala wa CHC ambazo zitamsaidia katika utetezi wake, jambo ambalo Spika alisema alishindwa kumsaidia kwa kile alichoeleza kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri.
Baada ya tamko hilo la Spika bungeni kumtaka Zitto kuwasilisha utetezi wake, mbunge huyo alimzunguka na kuamua kuwasilisha utetezi wake na vielelezo Alasiri ya siku hiyo (Juni 29).
JE ATANUSURIKA NA HUO USHAHIDI WAKE LEO BUNGENI ATAKAPOKUWA ANAUSOMA MBELE YA BUNGE?
Akishindwa watamvictimise kama kawaida ya bunge la magamba. Nasi tuwe tayari kudai kwa nguvu zote uthibitisho wa waziri mkuu kulidanganya bunge kuhusu mauaji ya Arusha wa Lema. Bi Kiroboto upo kwenye kona BE CAREFUL afadhali uiweke kabatini kama ya Lema LA SIVYO!!!!
 
Vipi bado hajasoma ushahidi wake tu jamani??? mwenye kusikiliza huko naomba atujuze
 
Inasemekana kuna ka sheria kanakokataza kuwa na 'siri' za serikali. Vpi kama kweli kapo kakitumiwa kumnanihii Zitto?! iwapo tu ni kweli kaanika nini Baraza la Mawaziri liliazimia!
Hakuna siri ya kufanya kitu haramu.
 
spika mwenyewe "AHSA NGEDERE" HUYU SIJUI ITAKUWAJE VILE ....NGIJA TUSUBURI
 
Kikao cha bunge jioni hiii kinaendelea lakini ille issue ya muheshimiwa Zito Kabwe kuwasilisha ule ushahidi wake leo Tarehe 4/07/2011 Spika Anne Makinda ameutupa kapuni! Kweli tunaye spika komandoo mwanamke.
 
Hivi wananchi wanawezaje kumuondoa Spika kama wanaona hafai? Wanasheria mnaweza kusaidi hili.

Nasema haya kwa sababu ili wananchi wawe na imani na bunge ni lazima wawe na imani kuwa wawakilishi wao wanapata nafasi ya kuwawakilisha kama sheria inavyosema. Spika Makinda badala ya kuongoza vikao vya wawakilishi wa wananchi kwenye chombo cha kutunga sheria na kuhoji serikali yeye amegeuka kuwa msemaji wa serikali, muamuzi wa nini na kwa style gani majibu yatolewe! Pamoja na kelele za muda juu ya utendaji wake mbovu Spiake Makinda ama kwa kutojua kazi na mipaka ya bunge kama mhimili wa doa au kwa makusudi ameamua kuligeuza bunge kuwa taasisi ya serikali. Imani juu ya bunge kama sehemu ya kutafuta majibu ya matatizo ya wananchi imepotea. Sasa kuna umuhimu gani kuendelea kutumia kodi zetu kumlipa huyu mama?. Wanasheria saidieni - Makinda hafai, miezi sita tu tayari amechafua kwa kiasi cha ajabu, je hadi 2015 nchi hii itakuwaje kama bunge litaendeshwa hivi? Serikali itawajibika kwa wananchi kweli?
 
Siamini km atakuw na mud mrefu kwani anaidharirisha hata serikali anayoitete hata km yeye anafikiri anaisaidia.........anaiabisha kwa kuwa inaonehsa ccm wanaweza kuchagua mtu shalow kwa maslahi yao ya kijinga (ufisadi)
 
mbwembwe zote za kuomba ushahidi zimeishia mdomoni mwake. Nadhani kama Zito angekosa ushahidi leo ndiyo ingekuwa sesion ya kwanza hata kabla ya maswali na majibu. sasa wananchi tunaona , tunasikia , tunaweza kupembua zipi pumba na upi ni mchele. Subiri waendelee kudanganya watafikia mwisho.
 
Back
Top Bottom