Kama Spika Makinda hatamruhusu Zitto kusoma ushahidi wake leo kwenye Bunge la Dodoma, basi Zitto asome ushahidi huo kwenye bunge la juu yaani huku mtaani kwa wananchi. Wananchi ndio wenye mamlaka na kama Makinda ameshindwa kazi aliyotumwa Zitto anatakiwa atutaarifu sisi wananchi maana ndio tuna mamlaka ya mwisho na sio Makinda. Hivyo Zitto tunategemea kutupa ushahidi kupitia njia mbalimbali, radio, tv, magezeti, JF, etc. Ni haki yetu sisi wananchi kujua nyinyi wawakilishi mnatuwakilishaje hivyo leta taarifa hapa.