Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo; Spika Makinda akiri, amtaka Mkulo arekebishe

Nilikuwa najaribu kufahamu kitu gani unachokipinga katika hiyo barua nikaconclude nia yako ni kujaribu kubadilisha mjadala. Hoja iko pale pale kuwa hii bajeti ya chama chenu ni mbovu (niliwahi kuyasema hayo alipokuwa akiisoma siku ile alipokuwa anaisoma). Kimsingi budget hii haina nia ya kumsaidia mlalahoi kwani inaua sekta ya binafsi, haionyeshi kwa kiwango gani mapato ya nchi yataongezeka zaidi ya kudai wanapandisha vitu vyengine kodi (cha kusikitisha hakuna vyanzo vipya vya kodi). Mwisho kabisa hili la posho kwani watakachobadilisha ni kupunguza malimbikizo ya mishahara na kujiongezea marupurupu yasioyokatwa kodi.

Worse enough wasivyo na huruma wala haya wanachokua kodi kwa mlalahoi yule yule wanayemkandamiza. Pole pole tutafika nchi ya ahadi tu!!!

Tazama post #49 na 148
 
Tatizo nilionalo ni kushindwa kwetu kama taifa kuwa makini katika utoaji wa taarifa zetu. Mimi ni mtu wa mahesabu kwa hiyo niliona immediately kuwa taarifa ya Zitto ilikuwa na makosa katika takwimu alizotoa ambapo hii inaonyesha kurudia makosa wafanyayo kina Mkullo. Ni vema. Tukawa makini zaidi tutoapo public statements ili zisiweze kuonekana fake simply because you didn't take enough time to do do some simple additions. Na hili liko kila mahali katika kukosa umakini. Nani asiyekumbuka barua aliyosain Tido Mhando ambayo ilikuwa na makosa chungu nzima kwenye uandishi na grammar and he just went ahead and signed it! One would have expected kwa mtu kama yeye angeaiangalia mara mbili mbili kabla ya kuisign kwani kakaa kwa wenzetu makini lakini wapi! Ndicho kilichomkuta Zitto. Now Zomba ia picking holes in the statement na kuifanya ya uongo kumbe kina Zitto wangeondoa ubishi wote huu kwa kuwa makini kidogo tu. Jana daily news wametoa takwimu za ajabu kabisa kwenye front page eti infrastructure imechukua 85 percent ya bajet na hapao hapo energy ikachuka 65 percent na wakachora na graph zao! Nikawapigia simu kwamba how can you be so ridiculous? Wakaomba msamaha but hii ndio trnd ya nchi yetu na viongozi wetu

At least daily news wamekuomba msamaha na sasa waliombe msamaha Taifa. Hapo juu utaona post ya Zitto imerekebishwa lakini sijui kama hii taarifa iligaiwa hard copies, kama ni hivyo, nawapa pole sana.

Na ingekuwa vyema kui edit post #1 wangetuomba msamaha , kwani hapo tunaongelea mawaziri vivuli, wanawakilisha Taifa hawa, watuombe msamaha kwa makosa yao ya kijinga, wamepotosha umma.
 
2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

"... Children Edition"! (Observe the font colors) KOBELLO; Please make sure you come again with another version kwa ajili ya wenye uelewa (wakubwa)!
 
Cha kushangaza! wengi wa changiaji humu, wanasifia na kuponda bila mantiki. Ni matatizo tuliyonayo Tanzania. Upinzani haumaanishi hata mema tuyapinge.Taarifa ya Zitto inaonesha kabisa kuwa ni upinzani usio na mantiki, mpaka kiasi inanishangaza, najiuliza kwa hayo aliyoyaandika, alikuwa labda ametingwa na kazi nyingi sana mpaka akakubali kuandika mambo yanayoitia aibu kambi ya upinzani?Kutumia nembo za bunge na kuishusha hii taarifa kwenye tovuti ambayo wengi, wa ndani na wa nje, wataiona na kuona makosa ya kipuuzi kabisa kutoka kwa Waziri kivuli wa fedha? Hata namba zinampiga chenga! ni kujivunjia hadhi kwa Zitto. Hivi Zitto na umakini wake wote anaweza kufanya makosa ya kijinga kama niliyoyaainisha katika post yangu hapo juu? Au Regia? Halafu kwa nembo ya Bunge?Inasikitisha sana, hata kukiwa na kosa moja tu la spelling kwa taarifa muhimu kama hiyo lazima ikemewe sana seuse hiyo yenye makosa mpaka ya sentensi nzima. Ni aibu kwa upinzani na inaonesha jinsi upinzani unavyokurupuka kutafuta makosa mpaka kiasi wao wanajiingiza kwenye makosa makubwa.Au ndio yule Zitto anaesemwa kuwa yuko pale si kwa ajili ya upinzani na ana agenda zake? Nashindwa kuelewa.Naomba Zitto au Regia aliyobandika hiyo taarifa, wawaombe radhi wa Tanzania kwa kuwawekea taarifa yenye nia ya kuupotosha umma ya ama kwa makusudi kabisa au kwa uzembe wa kukurupuka.Na hata baada ya makosa yote hayo, wanazi wa cdm bado wanashangilia tu, inanikumbusha ile habari ya "kufungwa twafungwa lakini chenga twawala". Nawaonea huruma kwa kutoyaona makosa ya viongozi wao.
we kweli zomba! Umeongea upuuzi mwiiiingi lakini hujatueleza makosa yaliyopo kwenye taarifa yenyewe. Kifupi, ulichokifanya ni ujinga tu!
 
Zitto,

Nakuheshimu sana mdogo wangu.

Nasikitika sana ninapoona, kwa umakini wako wote ulionao, unaaandika kwa kubabaisha na kupotosha. Mimi sijaipitia bajeti yote, lakini hayo ulyoainisha hapo ya ama umefanya makusudi kupotosha katika maandishi yako ya ama hujui namna ya kuandika, hususan ikija kwenye namba.

1. Mstari wa kwanza umeandika "shilingi 537 Bilioni", mstari wa tatu na wa nne ukaandika "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" na "shilingi 325,448,137,000." halafu mstari wa nne ukarudia tena "Shilingi Bilioni 325".

Swali: Kwanini
"shilingi 537 Bilioni" ziwe ni billioni? na kwanini "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" ziwe millioni? na kwa nini "shilingi 325,448,137,000." ziwe si millioni wala billioni? na halafu "Shilingi Bilioni 325" ziwe tena billioni?

2) Unaeleza kuwa:
kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa.

Halafu unasema:
Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011

Swali : Mbona hizo "
shilingi trilioni 11.624" "za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 huoneshi ngapi kati ya hizo zililipa madeni?

3) Swali: Jee, bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 zilikuwa ngapi? mbona huoneshi?

4) Kauli ilikuwa baadhi ya posho zitafutwa na baadhi ya posho zitapunguzwa.

Jee, ni nini kilichozugwa hapo?
.
Na kauli uliyowekea "bold" haihusiani na kufutwa au kupunguzwa kwa posho, kauli hiyo inaongelea "kusamehe" kodi, sasa mdogo wangu Zitto huelewi maana ya kusamehe kodi? Kama huelewi, hiyo kauli inamaanisha zile posho ambazo hazijafutwa na ambazo zimepunguzwa na ambazo hazijapunguzwa, zitasamehewa kodi. Sasa nini unachoona hakiko sawa hapo?

5) Labda ili ueleweke vizuri, ungeweka hizo faini ambazo zitafikia 50,000/= na ambazo zitazidi zaidi ya 50,000 na kufikia 300,000/= Usitupotoshe na usiupoteshe umma kwa kuwaambia kuwa huku hivi huku hivi.

Kwa kukukumbusha tuu, ingawa faini za barabarani tunazijuwa kikawaida ni 20,000/= tuliona hata Chenge alichapwa faini ya 700,000/= kwa makosa hayo hayo ya barabarani. Nimekutajia ya Chenge kwa kuwa ndio kesi maarufu na ni wengi wanayoifahamu. Kwa mantiki hiyo, inabidi ufafanue kwa kina hiyo faini ya 300,000 na ya 50,000. Tafadhali usipotoshe watu.

Hapo hapo, sentensi yako hii haieleweki "kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho". sijui inamaanisha nini?

6) Jee, ulitaka serikali isilipe madeni? na Jee, ulitaka serikali isilipe posho?, kama hutaki serikali ilipe posho, kwanza onyesha mfano kwa kuzikataa posho zako kama mbunge, kwani mojawapo ya wenye posho kubwa katika watumishi wa serikali ni wabunge. Halafu onesha na takwimu za bajeti iliyopita, asilimia ngapi ililipa madeni na asilimia ngapi ililipa posho. Usiandikie mate na wino upo.

7) Tunaisubiri kwa hamu na kama ni nzuri tutaiomba serikali iifate, kwani upinzani ndio kazi yake kuu, kukosoa ili serikali ijirekebishe.

Kwa kusherehesha tu, ningeomba ajibu Zitto mwenyewe kama anavyonukuliwa kuwa ndio muandishi wa taarifa hii, nikimuomba mleta mada Regia Mtema ajibu ntakuwa sikutenda haki kwani yeye inaonesha kuwa ni kipaza sauti tu cha Zitto.

Nadhani hii taarifa ndio ina kusudio la kupotosha wananchi kwa kuandikwa ndivyo sivyo.

Zomba shida ni figures sio ila mantiki ya barua unakubali kwamba kuna ufisadi unaendelea? Tuende kwenye figures kuna hizi unazozingumzia unasema hivi nanukuu:
"Swali: Kwanini "shilingi 537 Bilioni" ziwe ni billioni? na kwanini "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" ziwe millioni? na kwa nini "shilingi 325,448,137,000." ziwe si millioni wala billioni? na halafu "Shilingi Bilioni 325" ziwe tena billioni?"

Jibu: Shida yako ni maandishi ya billioni na millioni? Hujamuelewa Zitto alikuwa anahoji kitu gani au unajitia ujuha? Nikuulize swali Bilioni 537 ukitoa Bilioni 325 unabakiwa na Bilioni 212 je hizi pesa zitatoka wapi? Au unategemea Tanesco ikope??? Tanesco hiyo hiyo inaelemewa na mzigo wa madeni jibu nikwamba deni la taifa litaongezeka (Hii ndio pointi anayoisisitiza Zitto)

Nakunukuu tena unauliza hivi:

"
Swali : Mbona hizo "shilingi trilioni 11.624" "za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 huoneshi ngapi kati ya hizo zililipa madeni?

3) Swali: Jee, bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 zilikuwa ngapi? mbona huoneshi?"

Jibu: Nilivyomwelewa mimi Zitto alikuwa anazungumzia hivyo figures in relative terms. Je nikuulize Billioni 11.6 za mwaka 2010/2011 zilikuwa sawa na USD ($) kiasi gani mwaka huo. Na je Billioni 13.5 ni sawa na USD ($) kiasi gani mwaka huu. Ndio utagundua hakuna kilichoongezeka zaidi ya ukapa kuzipi.

Nanukuu tena swali jengine:
"
Jee, ni nini kilichozugwa hapo?"

Jibu lako ni kwamba unapokuwa na Tshs 987 Billion on allowances ni sawa na 8% of the annual budget ya mwaka huu. Hiyo inamaana karibu Bilioni 197.4 of tax zinapotea on allowances hela ambazo zingelisaidia hospitali, barabara, mipango miji, na kadhalika.

Mkulo hawezi kufukuzwa na JK maana ndiye mmoja wapo wa wapiganaji waliomsaidia kuwepo madarakani 2005 maana jamaa huyu mapaka alikamatwa lakini kwa kuwa hela alipewa kijana kuitoa Dar kwenda dodoma ilipita bila kujua Morogoro. unajua kwa nini Mzee wetu alitolewa ukuu wa mkoa pale Mor baada ya uchaguzi? jibu ndio hilo maana waliweka ulinzi mkali wa kupekua kila gari iliyokuwa inaelekea Dodoma ili kuhakisha hela haifika Dom kwenye kampeni hilo ndilo lilimponza mzee wetu.
 
Asante kwa taharifa imenitoa matongotongo kwani wengine haya mambo ya uchumi ni "mashokoro mageni" yaani ni mbumbumbu kwani naona yanaongelewa katika high profile level. Mimi kama mwananchi wa kawaida inakuwa kigunguzungu..... ni jana tu nilimsikia Mh. Zitto Zuberi Kabwe akisifia bajeti hii na kushadadia kwamba serikari ni sikivu na imesikia mapendekezo ya wapinzani (source redio Mawingu Kipindi Jahazi saa 10- 1 jioni). Sasa hii tena mbona inanichanganya i dont real now my fate!!!!! Jamani suluhisho ni nini HALI NI MBAYA SANA..... je hiyo bajeti yenu mbadala itatusaidia vipi? Je kutatokea mabadiliko.... Mh. Mkulo anaweza fikisha mahakamani kwa kuwadanganya wadanganyika? Au sie wadanganyika TULIANZISHE??
Majibu tafadhali...
 
Zomba shida ni figures sio ila mantiki ya barua unakubali kwamba kuna ufisadi unaendelea? Tuende kwenye figures kuna hizi unazozingumzia unasema hivi nanukuu:
"Swali: Kwanini "shilingi 537 Bilioni" ziwe ni billioni? na kwanini "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" ziwe millioni? na kwa nini "shilingi 325,448,137,000." ziwe si millioni wala billioni? na halafu "Shilingi Bilioni 325" ziwe tena billioni?"

Jibu: Shida yako ni maandishi ya billioni na millioni? Hujamuelewa Zitto alikuwa anahoji kitu gani au unajitia ujuha? Nikuulize swali Bilioni 537 ukitoa Bilioni 325 unabakiwa na Bilioni 212 je hizi pesa zitatoka wapi? Au unategemea Tanesco ikope??? Tanesco hiyo hiyo inaelemewa na mzigo wa madeni jibu nikwamba deni la taifa litaongezeka (Hii ndio pointi anayoisisitiza Zitto)

Nakunukuu tena unauliza hivi:

"
Swali : Mbona hizo "shilingi trilioni 11.624" "za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 huoneshi ngapi kati ya hizo zililipa madeni?

3) Swali: Jee, bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 zilikuwa ngapi? mbona huoneshi?"

Jibu: Nilivyomwelewa mimi Zitto alikuwa anazungumzia hivyo figures in relative terms. Je nikuulize Billioni 11.6 za mwaka 2010/2011 zilikuwa sawa na USD ($) kiasi gani mwaka huo. Na je Billioni 13.5 ni sawa na USD ($) kiasi gani mwaka huu. Ndio utagundua hakuna kilichoongezeka zaidi ya ukapa kuzipi.

Nanukuu tena swali jengine:
"
Jee, ni nini kilichozugwa hapo?"

Jibu lako ni kwamba unapokuwa na Tshs 987 Billion on allowances ni sawa na 8% of the annual budget ya mwaka huu. Hiyo inamaana karibu Bilioni 197.4 of tax zinapotea on allowances hela ambazo zingelisaidia hospitali, barabara, mipango miji, na kadhalika.

1) Hivi inakuingia akilini kutumia nembo za bunge na kufanya madudu kama hayo? toka kwa waziri kivuli? ikiwa hajui kuiandika millioni na billioni vipi kuwe na credibility ya kuchambuwa zaidi?

2) Hujajibu kwa hiyo umekubaliana na mimi.

3) Hakuna dollar inayongelewa hapo, usichakachuwe.

4) 5) 6) 7) Hujajibu kwa hiyo umekubaliana na mimi.

Mwisho, huoni kuwa swali lako halina mantiki? allowance lazima zitakuwepo, ikibidi isibidi, isipokuwa zipo zitakazofutwa na zipo zitakazo rekebishwa.
 
yaani waziri hajua hata kujumlisha ..pumbavu kabisa ..mi nilisema huyu alichaguliwa wa ajili ya kuwa na liupara otherwise hajui kitu..bora arusi tu morogoro akasimamie ila drycleaner yake kule njia ya kwenda SUA
 
1. Nadhani Zitto anajua kuwa nishati hapa Tanzania hujengwa kutokana na misaada na mikopo kutoka nje.Hata TANESCO hutafuta funds na mikopo kutoka nje ya serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali,mfano ule wa kusambaza umeme kilomita 667 toka Iringa mpaka shinyanga ambao umekuwa funded na European Investment Bank,shs bilioni 150...je ulikuwa kwenye bajeti yoyote?

2.Kulipa deni la taifa ni moja kati ya matumizi ya maendeleo,ina facilitate uwezo wa kupata mikopo.

3. Kuhusu posho, ni wajibu wetu watanzania, hasa wafanyakazi wa serikali kuamua au kujitolea kutokuzipokea au kuomba kupunguziwa kwa asilimia hamsini..... hapatakalika!

4. Jumatano nakuchallenge Zitto, usome bajeti itakayoonyesha vyanzo mbadala vya kodi na makato ya matumizi, ili elimu iwe bure!...cos you promised this in your campaigns na ilani ya CDM, kama haita-include free education huo utakuwa ni uhuni tu! Ninayo video ya Mnyika akielezea what you will do in your first year kwenye utawala kama mngepata ridhaa.

Wee Nape sikutegemea jibu la kipumbavu zaidi
 
we kweli zomba! Umeongea upuuzi mwiiiingi lakini hujatueleza makosa yaliyopo kwenye taarifa yenyewe. Kifupi, ulichokifanya ni ujinga tu!

Faiza Foxy huwa anawaambia msidandie kwa mbele! soma post Tazama post #49 na 148.
 
1) Hivi inakuingia akilini kutumia nembo za bunge na kufanya madudu kama hayo? toka kwa waziri kivuli? ikiwa hajui kuiandika millioni na billioni vipi kuwe na credibility ya kuchambuwa zaidi?

2) Hujajibu kwa hiyo umekubaliana na mimi.

3) Hakuna dollar inayongelewa hapo, usichakachuwe.

4) 5) 6) 7) Hujajibu kwa hiyo umekubaliana na mimi.

Mwisho, huoni kuwa swali lako halina mantiki? allowance lazima zitakuwepo, ikibidi isibidi, isipokuwa zipo zitakazofutwa na zipo zitakazo rekebishwa.

Kwani Zitto ni kwanza kufanya madudu mbona mkuu wako wa nchi anafanya madudu hayo hayo tena anatumia nembo ya Ikulu? Wewe unataka kudivert mjadala na sikuachi jibu kwanza maswali ya Zitto ndio mie nitakujibu hoja zako. Dollar nimezungumzia kama alivyozungumzia zitto akilinganisha bajeti ya mwaka jana na mwaka huu. Budget ya mwaka jana $ ilikuwa between 1300-1400 wakati wa budget leo tunaelekea 1500-1600 (according to the BOT data please refer for a proof).

Allowance zinaweza kuwapo ila ziwe ni zile zenye faida unapomlipa mbunge milioni 3 kwa mwezi kwa kazi ya miezi michache bungeni ikisha unamlipa allowance kwa kufanya kazi hiyo hiyo ya bungeni ni ufisadi na ndio kitu Zitto anachokipinga hasa wakati huu wa ukapa.

Zomba hizi ni zama za wasomi jibu hoja za zitto kwanza!!!!
 
yaani waziri hajua hata kujumlisha ..pumbavu kabisa ..mi nilisema huyu alichaguliwa wa ajili ya kuwa na liupara otherwise hajui kitu..bora arusi tu morogoro akasimamie ila drycleaner yake kule njia ya kwenda SUA

Hawezi kumfukuza kwani Kikwete naye ametoa ilani isiyotekelezeka.
 
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, anadaiwa kulipotosha taifa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwa lengo la kuwajengea wananchi matumaini hewa yenye kuonyesha serikali inawajali na kusikiliza matatizo yao.
Matumaini hayo aliyaonyesha kupitia hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2011/2012 juzi ambayo ilionyesha kuwa kutakuwa na nafuu ya maisha wakati hali halisi haipo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi wa kambi ya upinzani, Zitto Kabwe, na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika.
Katika taarifa yao iliyotolewa kwa niaba ya kambi ya upinzani, wabunge hao walisema wameshtushwa na upotoshaji huo ambao walisema una lengo la kuwapa wananchi matumaini hewa.
“Hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa, tuna uhakika ulifanywa kwa makusudi ili kuonyesha serikali inajali matatizo ya wananchi.”
Akiainisha maeneo aliyodai yamepotoshwa, Zitto alisema wakati waziri akitaja kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo kuwa ni kumaliza tatizo la umeme na serikali imetenga sh trilioni 537, upembuzi uliofanywa na kambi ya upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa sh 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58.
Alisema fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi kawaida sh 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa sh 325,448,137,000.
Alisema sh bilioni 325 zilizotengwa katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa megawati 160 zikiwamo megawati 100 za Dar es Salaam) na 60 za Mwanza.
“Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme,” ilisema taarifa hiyo.
Eneo lingine la upotoshaji ni hili: wakati waziri na serikali anataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa ya mwaka 2010/2011, kambi ya upinzani inasema kuwa hakuna ongezeko lililofanyika.
“Bajeti iliyopita ilikuwa sh trilioni 11.6 wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya sh trilioni 13.525…Kati ya fedha hizo za mwaka huu kiasi cha sh trilioni 1.901 ambazo ni sawa na asilimia 14.06 ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la taifa.
“Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha sh trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka wa fedha uliomalizika (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011).”
Kutokana na hali hiyo, kambi ya upinzani imesema hii si bajeti ya maendeleo bali ni ya madeni.
Katika eneo la tatu la upotoshaji, kambi ya upinzani ilisema wakati waziri akisema bajeti ya mwaka huu itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, ukweli ni kuwa bajeti hiyo imetenga sh trilioni 2.987, sawa na asilimia 13 ya bajeti yote kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama “Personnel allowances (non discretionary na In-kind”).
“Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bajeti ya mwaka huu imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji.
“Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vipaumbele vyake rasmi vya
bajeti ni kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
Lakini Waziri Mkulo katika hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha,” alisema.
Taarifa hiyo ilisema kambi ya upinzani imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (Asilimia 27 - 14 kulipa madeni na 13 kulipa posho mbalimbali).
Kambi ya upinzani inajipanga kuwasilisha bungeni bajeti mbadala Juni 15, ambayo Zitto alitamba kwamba, itakuwa inajali maslahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza uchumi wa vijijini na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta posho mbalimbali.
Juzi wakati Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, akisoma mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, aliliambia Bunge kwamba anapendekeza nyongeza ya kiwango cha faini kwa makosa ya usalama barabarani kutoka sh 20,000 za sasa hadi sh 50,000.
Lakini katika hotuba yake iliyochapishwa kwenye vitabu maalum na kusambazwa kwa wabunge, wanahabari na makundi mengine, ilisomeka kuwa amependekeza kiwango cha sh 300,000 badala ya sh 20,000.
“Mheshimiwa Spika napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama
Barabarani 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi sh 300,000,” ilisomeka sehemu ya hotuba ya Waziri Mkulo.
Akizungumzia utata huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alikiri kuwapo kwa mkanganyiko na kuahidi kuwa Waziri Mkulo atapeleka marekebisho ya usahihi wa faini hiyo.
“Kuna makosa, nadhani waziri ataleta marekebisho ya usahihi wa faini ya makosa ya barabarani,” alisema Spika Makinda.
Wakati Makinda akitoa kauli hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai, alisema kwa sasa Bunge linatambua kile kilichoingia kwenye Hansard za Bunge kwamba ndio sahihi.
“Waziri Mkulo alitamka kwamba faini ni sh 50,000. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hiki kitaingia kwenye kumbukumbu zetu. Kile kiasi cha sh 300,000, hatutakitambua hata kama kimo kwenye vitabu rasmi vya serikali.”
Chanzo: Tanzania daima.
 
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, anadaiwa kulipotosha taifa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwa lengo la kuwajengea wananchi matumaini hewa yenye kuonyesha serikali inawajali na kusikiliza matatizo yao.
Matumaini hayo aliyaonyesha kupitia hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2011/2012 juzi ambayo ilionyesha kuwa kutakuwa na nafuu ya maisha wakati hali halisi haipo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi wa kambi ya upinzani, Zitto Kabwe, na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika.
Katika taarifa yao iliyotolewa kwa niaba ya kambi ya upinzani, wabunge hao walisema wameshtushwa na upotoshaji huo ambao walisema una lengo la kuwapa wananchi matumaini hewa.
"Hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa, tuna uhakika ulifanywa kwa makusudi ili kuonyesha serikali inajali matatizo ya wananchi."
Akiainisha maeneo aliyodai yamepotoshwa, Zitto alisema wakati waziri akitaja kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo kuwa ni kumaliza tatizo la umeme na serikali imetenga sh trilioni 537, upembuzi uliofanywa na kambi ya upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa sh 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58.
Alisema fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi kawaida sh 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa sh 325,448,137,000.
Alisema sh bilioni 325 zilizotengwa katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa megawati 160 zikiwamo megawati 100 za Dar es Salaam) na 60 za Mwanza.
"Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme," ilisema taarifa hiyo.
Eneo lingine la upotoshaji ni hili: wakati waziri na serikali anataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa ya mwaka 2010/2011, kambi ya upinzani inasema kuwa hakuna ongezeko lililofanyika.
"Bajeti iliyopita ilikuwa sh trilioni 11.6 wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya sh trilioni 13.525…Kati ya fedha hizo za mwaka huu kiasi cha sh trilioni 1.901 ambazo ni sawa na asilimia 14.06 ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la taifa.
"Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha sh trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka wa fedha uliomalizika (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011)."
Kutokana na hali hiyo, kambi ya upinzani imesema hii si bajeti ya maendeleo bali ni ya madeni.
Katika eneo la tatu la upotoshaji, kambi ya upinzani ilisema wakati waziri akisema bajeti ya mwaka huu itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, ukweli ni kuwa bajeti hiyo imetenga sh trilioni 2.987, sawa na asilimia 13 ya bajeti yote kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama "Personnel allowances (non discretionary na In-kind").
"Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa," ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bajeti ya mwaka huu imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji.
"Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vipaumbele vyake rasmi vya
bajeti ni kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
Lakini Waziri Mkulo katika hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha," alisema.
Taarifa hiyo ilisema kambi ya upinzani imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (Asilimia 27 - 14 kulipa madeni na 13 kulipa posho mbalimbali).
Kambi ya upinzani inajipanga kuwasilisha bungeni bajeti mbadala Juni 15, ambayo Zitto alitamba kwamba, itakuwa inajali maslahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza uchumi wa vijijini na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta posho mbalimbali.
Juzi wakati Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, akisoma mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, aliliambia Bunge kwamba anapendekeza nyongeza ya kiwango cha faini kwa makosa ya usalama barabarani kutoka sh 20,000 za sasa hadi sh 50,000.
Lakini katika hotuba yake iliyochapishwa kwenye vitabu maalum na kusambazwa kwa wabunge, wanahabari na makundi mengine, ilisomeka kuwa amependekeza kiwango cha sh 300,000 badala ya sh 20,000.
"Mheshimiwa Spika napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama
Barabarani 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi sh 300,000," ilisomeka sehemu ya hotuba ya Waziri Mkulo.
Akizungumzia utata huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alikiri kuwapo kwa mkanganyiko na kuahidi kuwa Waziri Mkulo atapeleka marekebisho ya usahihi wa faini hiyo.
"Kuna makosa, nadhani waziri ataleta marekebisho ya usahihi wa faini ya makosa ya barabarani," alisema Spika Makinda.
Wakati Makinda akitoa kauli hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai, alisema kwa sasa Bunge linatambua kile kilichoingia kwenye Hansard za Bunge kwamba ndio sahihi.
"Waziri Mkulo alitamka kwamba faini ni sh 50,000. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hiki kitaingia kwenye kumbukumbu zetu. Kile kiasi cha sh 300,000, hatutakitambua hata kama kimo kwenye vitabu rasmi vya serikali."
Chanzo: Tanzania daima.

makinda amekiri wapi?
 
Back
Top Bottom