Zitto Kabwe, ndani ya Addis na JK

WAKUU!

Namshangaa huyu Mh. Zitto Z. Kabwe. Wakati wa mkutano wa M4C Morogoro tuliambiwa angehudhuria. Baadae mawasiliano kati yake na Makamanda waliokuwa kwenye harakati za ukombozi yakapotea. Leo hii katia timu Addis na Mkulu.

Makamanda, hii ime kaa je? wakati Makamanda wengine wakiendeleza harakati za kuwakomboa waTanzania huyu Mh. mbona yupo beneti na Magogoni sana?

Ni kuuliza tu Makamanda.



Zitto Kabwe MWAKA 1975, mwanafunzi wa
mwaka wa kwanza wa Chuo
Kikuu cha Haile Selasie (sasa
Chuo Kikuu cha Addis Ababa),
Legese Zenawi, akiwa na umri
wa miaka 19 tu, aliacha masomo yake na kujiunga na
kikundi cha ukombozi cha
watu wa Tigray (Tigray
Peoples Liberation Front). Legese alikuwa anasomea
shahada ya kwanza ya
udaktari. Hakurudi tena chuoni
kusomea udaktari na hakuishi
tena maisha ya ujana ambayo
sisi wengine wote tumeishi na kuyafurahia. Mwaka 2012, Legese akiwa na
umri wa miaka 57 alifariki
dunia. Lakini aliaga dunia
akiwa Meles Zenawi na sio
Legese Zenawi, jina alilopewa
na wazazi wake huko Adwa kaskazini mwa Ethiopia. Legese alibadili jina lake kwa
hiari yake kufuatia kuuawa
kwa rafiki yake na mpiganaji
mwenzake, Meles mwaka
1975. Aliamua kumuishi
mpiganaji mwenzake kwa kuchukua jina lake na kuacha
jina alilopewa na wazazi
wake. Meles alifanikiwa kupigana
dhidi ya utawala wa kiimla
wa Mengistu Haile Mariam na
kumtoa madarakani, na
kuingiza uongozi wa
kimaendeleo chini ya chama cha kitaifa cha Ethiopian
People’s Revolutionary
Democratic Front (EPRDF). Meles Zenawi aliahidi
kumpigania rafiki yake Meles
kwa faida ya wananchi
wanyonge wa Ethiopia na
akatimiza ahadi hiyo kwa
mafanikio makubwa sana. Mwanzoni Meles alipigana
kwa lengo la kutaka uhuru wa
eneo la Tigray kutoka utawala
wa Mengistu na kundi la
wanajeshi chini ya Derg. Meles
na wenzake waliamini kabisa kwamba utawala nchini
mwao chini ya Mfalme Haile
Selasie na hata chini ya
utawala wa Derg uligubikwa
na ukabila na ueneo kwa faida
ya kabila kubwa nchini humo, Amhara. Aliamini kwamba makabila
madogo kama kabila lake la
Tigray kutoka kaskazini mwa
Ethiopia na hata makabila
mengine kama Wasomali
walikuwa wanakandamizwa na kunyonywa ndani ya nchi
yao. Aliamini kwamba utajiri
wa nchi ulikuwa unatumika
kwa faida ya kundi moja
lililohodhi madaraka ya nchi
na kabila lao. Akiwa na umri wa miaka 19
tu na mwanafunzi wa mwaka
wa kwanza wa chuo kikuu,
aliamua kushika silaha na
kupambana na ugandamizaji
huu. Hata hivyo, Meles alibadili
kabisa mtazamo wake
alipogundua kuwa sio watu
wa Tigray tu waliokuwa
wakinyonywa na
kugandamizwa na utawala wa Mengistu, bali ilikuwa ni
Waethiopia wote bila kujali
makabila yao. Mwaka 1985 alichaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa chama
cha TPLF akiwa na umri wa
miaka 29 tu. Alihakikisha
anaikomboa Tigray kama
mkakati wa kuikomboa Ethiopia yote. Alishirikiana na
wakombozi wa Jimbo jirani la
Eritrea ili kutetea uhuru wao
na kuwapa uhuru wa kuamua
kama wanataka kubakia
sehemu ya Ethiopia au kuwa taifa huru ambapo waliamua
kuwa taifa huru. Akiwa kijana wa chini ya umri
wa miaka 30, aliunganisha
makundi mbalimbali
yaliyokuwa na lengo la kuleta
ukombozi na kujenga Ethiopia
mpya chini ya mwavuli wa chama cha EPRDF. Chama
kilikuwa ni umoja wa
makabila yote nchini Ethiopia
na walimchagua Meles
kuongoza mapamabano ya
ukombozi. Mwaka 1991, Meles Zenawi
aliongoza EPRDF kuingia Addis
Ababa na kushika dola huku
Mengistu akikimbilia nchini
Zimbabwe. Meles akiwa na umri wa
miaka 36 tu alichaguliwa
kuwa Rais wa muda wa
Ethiopia na mkutano mkuu wa
kitaifa ambao kwa mara ya
kwanza ulikutanisha makabila yote nchini Ethiopia. Miaka
mitatu baadaye kufuatia kura
ya maoni, Jimbo la Eritrea
likajitenga kutoka Ethiopia na
kuunda taifa huru. Meles
alitimiza ahadi yake ya kuruhusu watu wa Eritrea
kuamua kama wanataka
kuwa taifa linalojitegemea au
kuwa sehemu ya Shirikisho la
Ethiopia. Hata mahusiano kati
ya Ethiopia na Eritrea yalipokuwa mabaya sana kiasi
cha kupigana vita kugombea
Kijiji cha Badme, Meles
hakuchukua fursa hiyo
kuirudisha Eritrea kuwa mkoa
ndani ya Ethiopia au hata kupata njia ya kwenda
baharini, bali aliheshimu
matakwa ya Waeritrea ya
kujitawala. Ukweli ni kwamba vita kati ya
Eritrea na Ethiopia ilikuwa ni
vita isiyo na maana yeyote ile
na itabakia kuwa doa katika
historia ya uongozi wa Meles.
Kitendo cha Meles kutoheshimu maamuzi ya
Umoja wa Mataifa kwamba
Badme ni sehemu ya Eritrea
pia ni doa ambalo wafuasi wa
Meles wataendelea kuwa nalo
daima dumu na wakosoaji wa Meles wataendelea kujengea
hoja kuonesha kuwa kiongozi
huyu hakuwa anaheshimu
maamuzi ya taasisi za
kimataifa. Hata hivyo doa hili
haliwezi kufuta mafanikio makubwa ambayo Kamaradi
Meles ameyapata katika
Ethiopia iliyokombolewa. Meles alipochaguliwa kuwa
kiongozi wa chama cha TPLF
mwaka 1985, Ethiopia ilikuwa
kwenye ramani ya dunia kama
taifa lililoshindwa kulisha
watu wake. Dunia nzima kulikuwa na kampeni za
kusaidia kuondoa njaa nchini
humo, ambayo iliua zaidi ya
watu milioni moja. Wakati mauaji ya kimbari
nchini Rwanda yaliua watu
milioni moja kwa mapanga na
mashoka, njaa iliua watu
kama hao, hasa katika
maeneo ya Tigray na Wollo kwa sababu ya uzembe wa
Serikali ya Mengistu. Mmoja
wa wajumbe wa Kamati Kuu
wa chama cha Mengistu
kilichokuwa kinatawala
wakati ule (Workers Party of Ethiopia), Dawit Wolde
alimtahadharisha Mengistu
kuhusu hali mbaya ya
wananchi, na kwamba serikali
ilipaswa kuchukua hatua na
kujibiwa ‘kulikuwa na mabaa ya njaa miaka yote kabla sisi
hatujatawala’. Hiyo ni namna
uasili (nature) inafanya kazi
yake. Kuingilia uasili ndiyo
maana leo tumefikia watu
milioni 40 (Meredith in The State of Africa). Mengistu
alilewa madaraka kiasi cha
kusahau kwamba siku moja
kabla ya kumvua madaraka
Mfalme Haile Selasie
walimwonesha filamu (The hidden famine) ya namna yeye
alivyokuwa anastarehe na
pombe aghali na kulisha
nyama mbwa wake ilhali
wananchi wake walikuwa
wanakufa kwa kukosa chakula katika baa la njaa la
mwaka 1984 katika Wilaya ya
Wollo. Haile Selasie baada ya
kuonesha filamu hiyo
alipoteza fahamu kwa
mawazo na siku iliyofuata
tarehe 12 Septemba 1974
akavuliwa ufalme na vijana watatu wanajeshi akiwemo
Mengistu Haile Mariam.
Mengistu huyo huyo akiwa
Rais wa Ethiopia akawa
anajenga hoja kwamba njaa ni
tukio la asili ili ‘kubalance’ idadi ya watu nchini mwake!
Haya ndiyo mazingira ambayo
Meles alichaguliwa kwayo
kuongoza mapambano ya
ukombozi akiwa na umri wa
miaka 29 tu. “Naomba vitabu vya uchumi,”
ndilo ombi pekee Meles alilitoa
kwa mwanahabari wa kigeni
aliyekwenda kumfanyia
mahojiano mara baada ya
kuchukua uongozi wa taifa lake. Mwanahabari huyo alimwuliza
ni msaada gani anataka
kutoka kwa nchi za magharibi
ili awaambie kupitia habari
yake anayokwenda kuandika.
Meles alijua kwamba ana ajenda moja kubwa nayo ni
kuondoa njaa. Kuondoa
umasikini nchini mwake.
Ajenda hii aliifanyia kazi kwa
nguvu zake zote kipindi chote
ambacho yeye alikuwa rais na baadaye Waziri Mkuu wa
Ethiopia. Nakumbuka tulikuwa
tunatania mtu yeyote
aliyekondeana kwa kusema
‘ana njaa kama Ethiopia’ na
hiyo ndiyo ilikuwa picha
inayokuja machoni mwa watu wengi duniani kuhusu
Ethiopia. Meles hakumaliza
shida zote za Ethiopia, lakini
alipambana nazo.
Alizipunguza. Amelitoa taifa
lake kutoka taifa la kupigiwa mfano kwa njaa na umasikini
kwenda taifa la kupigiwa
mfano kwa maendeleo. Katika kipindi cha miaka
ishirini ya utawala wake
hatujasikia baa kubwa la njaa
kama ilivyozoeleka kila
muongo nchini humo.
Mwanahistoria mmoja nchini humo alionesha kuwa kila
muongo ulikumbwa na njaa
kali nchini Ethiopia; 1958,
1966, 1973 na 1984. Lakini
toka Meles achukue uongozi
wa taifa la Ethiopia hatukusikia njaa miaka ya
tisini wala miaka ya 2000. Ninaamini watakaomrithi
Meles watahakikisha kuwa
hakuna njaa tena ya kiwango
kile nchini Ethiopia kwa
miongo mingine yote ijayo. Mafanikio haya yanatokana na
sera na maamuzi thabiti na ya
dhati kutoka kwa kiongozi.
‘Sitaki njaa nchini kwangu’.
Pia usimamizi thabiti wa
maamuzi sahihi yaliyotolewa. Meles aliamua kupambana na
umasikini na kujenga taifa
lenye nguvu za kiuchumi.
Aliamua mapema kabisa
kukataa ushauri wa IMF na
Benki ya Dunia wa kuufungua uchumi wa Ethiopia haraka
sana (liberalisation). Yeye na
wenzake waliamua
kuufungua uchumi kidogo
kidogo kulingana na ratiba
waliyojiwekea wao wenyewe. Kutokana na hali
hiyo sehemu kubwa ya
uchumi wa Ethiopia
imeshikwa na wao wenyewe
wananchi wa Ethiopia. Meles amejenga miundombinu
kuunganisha uchumi wa nchi
na hivyo kufungua masoko ya
ndani licha ya yeye
mwenyewe kusisitiza sana
mauzo ya nje. Kutokana na maamuzi yake, hivi sasa
Ethiopia itaanza kuuza nje
viatu vya ngozi
vilivyotengenezwa nchini
humo vyenye thamani ya dola
za Kimarekani bilioni nne. Hii ni sawa na mara mbili ya
mauzo ya dhahabu yote ya
Tanzania kwenye soko la
dunia. Ethiopia haina mafuta wala
madini ya kutosha kama
Tanzania, lakini uchumi wake
umekuwa ukikua kwa zaidi ya
asilimia kumi kwa miaka saba
mfululizo. Ndiyo maana Meles ameweza kupunguza
umasikini kutoka asilimia 45
ya watu waliokuwa wakiishi
kwenye dimbwi la umasikini
mwaka 1991 mpaka asilimia
29 mwaka 2011. Katika kipindi kama hicho (1991 –
2011) umasikini Tanzania
ulishuka kutoka asilimia 37 ya
watu kuishi kwenye dimbwi
la umasikini mpaka asilimia 35
tu. Tanzania iliamua kufuata sera za kufungua uchumi wa
nchi kwa haraka kama
walivyoshauri IMF na Benki ya
Dunia. Wakati Meles anaaga dunia,
ameacha mradi mkubwa sana
unatekelezwa nchini mwake.
Mradi wa kuzalisha umeme
10,000 MW, Grand Millenium
Project. Lengo lake ni kuzalisha umeme wa kutosha
kufanya mabadiliko makubwa
ya maisha ya wananchi wa
Ethiopia na pia kuuza nchi
jirani (Diplomasia ya Nishati).
Benki ya Dunia ilikataa kufadhili mradi huu, yeye
akaamua kila Muethiopia
kutoa fedha za kufadhili mradi
huu. Wananchi wa Ethiopia
wote kila mmoja akajitolea
mshahara wake wote wa mwezi mmoja na fedha hii
kugeuzwa kuwa dhamana. Pia
wananchi wa Ethiopia
wanaoishi nje ya nchi nao
waliruhusiwa kununua
dhamana hizi na kufadhili mradi huu kabambe. Mradi
unatekelezwa kwa fedha za
Waethiopia wenyewe. Nina imani kuwa mradi huu
utaendelezwa na viongozi
wapya wa Ethiopia. Uzuri ni
kwamba Meles alilea kizazi
kipya cha uongozi. Aliamua
kuchukua vijana wa rika mbili chini yake na kuwapa
majukumu na kuwalea
kiuongozi ili waweze kuwa
tayari kurithi mikoba ya
viongozi wanaomaliza muda
wao. Waziri Mkuu mpya wa
Ethiopia ana umri wa miaka
kumi chini ya Meles. Meles alijua umuhimu wa
kuandaa viongozi wa
baadaye. Yeye hakuandaliwa.
Mazingira ya ugandamizwaji,
unyanyasaji na umasikini
yalimwita kuchukua majukumu ya kiuongozi
akiwa kijana mdogo sana wa
miaka 19 alipoamua kujiunga
na jeshi la ukombozi, miaka 29
alipochaguliwa kuongoza jeshi
la ukombozi na miaka 36 alipochaguliwa kuwa rais na
baadaye waziri mkuu wa taifa
lake. Meles ana makosa yake kama
binadamu. Amelaumiwa sana
na mataifa ya magharibi
kuhusu rekodi yake ya
masuala ya haki za binadamu
na kidemokrasia. Lakini pia amelaumiwa na baadhi ya
wanaharakati kwa kuuza
ardhi ya wananchi kwa
makampuni ya kilimo ya
mashariki ya kati na mashariki
ya mbali kama China. Hata hivyo sijawahi kusikia tuhuma
zozote za Meles kuhusu ufisadi
na kujilimbikizia mali. Siku
zote aliamini kuwa cheo ni
dhamana na hakutumia cheo
chake kwa faida yake tofauti na viongozi wengi sana wa
Kiafrika. Hapa nchini kwetu
tunashuhudia watu
wakitumia nafasi zao za
uongozi kulimbikiza mali.
Watu wana tamaa iliyokithiri
ya mali. Ufisadi imekuwa ni hulka na sasa ufisadi
unahusisha nafasi yoyote ya
uongozi. Hata tuhuma za
ufisadi na rushwa zimekuwa
za kawaida mno mpaka
unakuta wala rushwa wanatuhumu viongozi wenye
maadili ili mradi tu ionekane
rushwa ni ya kila mtu wa kila
chama. Imekuwa kama wezi
kuungana kumkimbiza polisi. Meles hakutaka Ethiopia ifikie
hali hii. Alipambana na rushwa
yeye mwenyewe kwa
kujiwekea viwango vya
kutokuwa na mawaa ya
rushwa au matumizi mabaya ya ofisi ya umma. Meles Zenawi ameacha mfumo
wa uchumi ambao haujapata
fursa ya kujadiliwa vya
kutosha. Mfumo ambao
umeiweka Ethiopia kuwa
moja ya mataifa yatakayokuwa na nguvu
kubwa ya kiuchumi katika
bara la Afrika ndani ya
muongo mmoja na nusu ujao.
Alipambana na umasikini kwa
dhati na kwa nguvu inayostahili. Ametimiza
wajibu wake. Natamani kuwa Meles maana
ameishi anachoamini kwa
kupambana na ufisadi bila
yeye kuwa fisadia na kutumia
vibaya ofisi yake ya umma. Nitaishi kuwa Meles maana
adui wetu nambari moja ni
umasikini, umasikini wa
vijijini. Meles alitangaza
mwaka 1991 kuwa, ‘our first
enemy is poverty and backwardness’ na
akapambana na adui
umasikini kadiri ya uwezo
wake. Hakuna namna bora
zaidi ya kumuenzi Meles zaidi
ya kutenda yale mema aliyoyatenda na kurekebisha
yale aliyoyakosea. Nilipata fursa ya kukutana na
Meles mara moja. Nilikutana
naye nchini Nigeria katika
mkutano kuhusu mashirikiano
ya kiuchumi kati ya nchi za
Ulaya na nchi za Kiafrika mwaka 2009. Baada ya
mkutano ule niliamua
kumsoma Meles na misingi
anayosimamia. Ni kama
nilimwona Mahathir Mohamad
wa Malaysia ndani ya Meles Zenawi kwa namna ya
utendaji wao na uwezo wao
wa kujenga hoja. Isipokuwa
tu Meles hakumaliza shahada
yake ya udaktari na Mahathir
alimaliza yake. Ni dhahiri kwamba Meles
Zenawi alikuwa ni kiongozi
mwenye uwezo mkubwa
sana kiakili pengine kuliko
viongozi wote wa kizazi cha
pili barani Afrika. Uwezo wake wa Akili uliwatisha viongozi
wa mataifa ya Magharibi.
Walimwogopa. Wenzake wa
Afrika walimheshimu.
Alikuwa sauti ya Afrika kutoka
Addis Ababa, Makao makuu ya Afrika. Upumzike kwa amani
Meles.
 
Kwani kufanya kazi za kitaifa ni kosa. Kwa mawazo yako, kwa vile ni Mbunge wa CHADEMA basi hatakiwi afanye shughuli za kitaifa.

Mkuu siasa sio chuki, nadhani Zito amepata baraka zote toka kwa Viongozi wake. Suala la Zito kutoka nje na JK, linamjenga sana kidiplomasia na kuelewa siasa za nje zinavyoendeshwa.

Nafikiri ktk siasa zilizokomaa upinzani sio uadui wala siyo vita. Hivyo sioni sababu ya kuchukia kama hjyo dogo atakuwa amesafiri na mkulu wa nchi.

Upinzani sio vita, tujaribu kubadilika! Bado hajaenda kwenye tukio baya kumbuka ni msiba huo.

Tatizo la Zitto siyo kusafiri na Kikwete, tatizo ni kwa nini yupo benet sana na Viongozi kwa CCM kuliko viongozi wake ndani ya Chama? Nyie mnasema siasa siyo chuki wala uadui mbona Dk Slaa, Mnyika na Lema wanawindwa kwa sababu za kisiasa? Iweje na JK nae analindwa na msafara kama siasa siyo uadui? Acheni kupotosha. Siasa ina create maadaui na kama usipojipanga vizuri huchukui round. Ndiyo maana Dk Slaa anatembea na Bastola na Board Guard wa kutosha!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
ZZK aliweka wazi muda mrefu kwamba Zenawi ni Idol wake katika siasa na uongozi barani Afrika. Ameandika makala ndefu kuelezea namna anavyotamani kuishi kama marehemu Zenawi. Kwa hiyo kuhudhuria mazishi ya Zenawi hakuna tabu wala haipaswi kuingizwa fitina yeyote ya kisiasa.

Tunachopaswa kuhoji ni kwa nini JK anahudhuria kila msiba wa kiongozi mkubwa wa kisiasa, ndani na nje ya nchi, wakati kuna Makamu, PM, Waziri wa mambo ya nje nk. Kwa hili tunapaswa kumuhoji JK.
 
Hivi kwanini zitto hashiriki m4c? Yeye namuona yupo kivyake tu..


Aibu ndio inamtesa Unajua mtu aki ku betray ukamjua lazima akukwepe na ndicho anafanya anachofanya zitto, Unajua huko ni rahisi kuwa na faragha na Mkuu magogoni paparaz wengi na ukizingatia siasa sio uadui japo Naamini watakuwa na serous talk na JK.
 
Yeah man!! labda kaenda kwa gharama zake au kwa kukaribishwa na JK ama kaenda kama naibu kambi ya upinzani,,nani kagharamia safari

Mkuu Hata wewe ingekuwa una rafiki magogoni ungeenda bure umesahau kuwa bajaji la JK huwa linakula vichwa Kama Mia? Kuhusu garama unauliza tena wakati ukifanya kazi Kanisani unakula Kanisani? Ukienda na boss wako bar nani analipa bill? Invoice inaenda magogoni
 
et2.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo leo
ikulu ya Addis Ababa
kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi anayetarajiwa kuzikwa kesho.
Wengine katika picha ni baadhi ya wajumbe waliofuatana na Rais Kikwete watakoshiriki mazishi ya kiongozi huyo.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde, Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini
Ethiopia Jenerali Mirisho Sarakikya, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe.Joram Boswaro,
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe na Waziri wa Kazi wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.

Picha kwa hisani ya Ikulu!!
 
Kulingana na vyanzo vyangu vya kuaminika Zitto ni confirmed double-dealer, tena kitambo tu.

Kijana kapewa bei akauza utu wake na future yake kisiasa ktk Tanznaia ijayo. Hawezi tena kuaminiwa au kupendwa kama awali kwani keshalambishwa asali na JK/CCM sasa amekuwa ktk harakati za kuchonga mzinga.

Mithali hizi kwa masikitiko zimetimia kwa Zitto:-

"Ivumayo ......"

"Mgema akisifiwa......"

NA

"Mtaka vyote kwa pupa....HUKOSA VYOTE."
 
Tatizo la Zitto siyo kusafiri na Kikwete, tatizo ni kwa nini yupo benet sana na Viongozi kwa CCM kuliko viongozi wake ndani ya Chama? Nyie mnasema siasa siyo chuki wala uadui mbona Dk Slaa, Mnyika na Lema wanawindwa kwa sababu za kisiasa? Iweje na JK nae analindwa na msafara kama siasa siyo uadui? Acheni kupotosha. Siasa ina create maadaui na kama usipojipanga vizuri huchukui round. Ndiyo maana Dk Slaa anatembea na Bastola na Board Guard wa kutosha!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
Mkuu wa PhD! ungeangalia solutions nilizoweka nadhani ungenielewa. Nimeangalia ktk positive and negative sides ya uhusiano wao na janja ya CCM.
 
WAKUU!

Namshangaa huyu Mh. Zitto Z. Kabwe. Wakati wa mkutano wa M4C Morogoro tuliambiwa angehudhuria. Baadae mawasiliano kati yake na Makamanda waliokuwa kwenye harakati za ukombozi yakapotea. Leo hii katia timu Addis na Mkulu.

Makamanda, hii ime kaa je? wakati Makamanda wengine wakiendeleza harakati za kuwakomboa waTanzania huyu Mh. mbona yupo beneti na Magogoni sana?

Ni kuuliza tu Makamanda.

M4C movement for chaga na yeye ni muha wa kigoma sasa unataka akafanye nini huko?
 
et2.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo leo
ikulu ya Addis Ababa
kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi anayetarajiwa kuzikwa kesho.
Wengine katika picha ni baadhi ya wajumbe waliofuatana na Rais Kikwete watakoshiriki mazishi ya kiongozi huyo.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde, Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini
Ethiopia Jenerali Mirisho Sarakikya, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe.Joram Boswaro,
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe na Waziri wa Kazi wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.

Picha kwa hisani ya Ikulu!!

Hata lema alikuwa uingeleza anataka ukameroon
 
Mbowe na Sugu wako marekani wanafanya matamasha ya muziki sugu anaimba mbowe ni DJ wake.
 
WAKUU!

Namshangaa huyu Mh. Zitto Z. Kabwe. Wakati wa mkutano wa M4C Morogoro tuliambiwa angehudhuria. Baadae mawasiliano kati yake na Makamanda waliokuwa kwenye harakati za ukombozi yakapotea. Leo hii katia timu Addis na Mkulu.

Makamanda, hii ime kaa je? wakati Makamanda wengine wakiendeleza harakati za kuwakomboa waTanzania huyu Mh. mbona yupo beneti na Magogoni sana?

Ni kuuliza tu Makamanda.

Nae kashajimegea chake na anaona mkielimika atakula wapi baadae?
 
Aibu ndio inamtesa Unajua mtu aki ku betray ukamjua lazima akukwepe na ndicho anafanya anachofanya zitto, Unajua huko ni rahisi kuwa na faragha na Mkuu magogoni paparaz wengi na ukizingatia siasa sio uadui japo Naamini watakuwa na serous talk na JK.

zitto zuberi angeitwa yohana au john haya yote yasingemfika.hana usaliti wowote,kinachomsaliti ni hilo jina tu.
 
sioni kama kuna tatizo hata kama Zitto ataamua lunch yake awe anapata nyumbani kwa JK.
Hakuna tatizo hata kidogo. tatizo watu tuna'over look sana.
 
Back
Top Bottom