Zitto Kabwe alikuwa na nafasi gani ndani ya ACT Wazalendo?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
zito.jpg

Haya wajuba wazee wa siasa za Bongo muje munieleze vizuri. Zitto Kabwe alikuwa na nyadhifa gani ACT Wazalendo?

Wanahabari wetu wanaishia tu kutuambia kuwa alikuwa kiongozi wa chama.
 
Simply, nafasi aliyokuwa nayo Zitto pale ACT ilikuwa ni fake, hakuna popote kwenye mfumo wa kidemokrasia hapa duniani utamkuta kiumbe anayeitwa "supreme leader" huu ni ulafi tu wa madaraka wa Zitto aliotoka nao Chadema akaona akakate kiu yake ACT.

Bahati mbaya tena, ameondoka kwenye cheo chake lakini ameacha udikteta chamani, huyu supreme leader anaweza vipi kuwa sawa na wanachama wengine kwenye mambo ya kimaamuzi ndani ya chama chao?

Kama hatakuwa sawa na wengine, yeye awe na kura ya "veto" basi hicho chama sio cha wanachama kwasababu maamuzi yao hayaheshiwi, hicho chama ni mali binafsi ya "supreme leader" hata kama sasa hivi wametoa hiyo nafasi kwa mwingine.

Zitto baada ya kuona kiu yake ya kujiweka juu ya wengine aliyoikosa Chadema amefanikiwa kuikata akiwa ACT, alitakiwa kuondoka uongozini na hicho cheo chake, lakini kwa kuondoka yeye na kukiacha hicho cheo, iko siku kitawatokea puani mbele ya safari.

NB.
Nimeona kwenye katiba yao ACT Zitto anaenda kukamata cheo cha "mshauri mkuu wa chama", hivi huyu kiumbe unaweza vipi kusema amejiuzulu? mimi nachoona hapo ametokea kwa mlango wa mbele, kisha akazungukia kwa mlango wa nyuma kurudi ndani!.

Hao wanaomtaka Mbowe ajifunze kwa Zitto nawaona hawajielewi kabisa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Simply, nafasi aliyokuwa nayo Zitto pale ACT ilikuwa ni fake, hakuna popote kwenye mfumo wa kidemokrasia hapa duniani utamkuta kiumbe anayeitwa "supreme leader" huu ni ulafi tu wa madaraka wa Zitto aliotoka nao Chadema akaona akakate kiu yake ACT.

Bahati mbaya tena, ameondoka kwenye cheo chake lakini ameacha udikteta chamani, huyu supreme leader anaweza vipi kuwa sawa na wanachama wengine kwenye mambo ya kimaamuzi ndani ya chama chao?

Kama hatakuwa sawa na wengine, yeye awe na kura ya "veto" basi hicho chama sio cha wanachama kwasababu maamuzi yao hayaheshiwi, hicho chama ni mali binafsi ya "supreme leader" hata kama sasa hivi wametoa hiyo nafasi kwa mwingine.

Zitto baada ya kuona kiu yake ya kujiweka juu ya wengine aliyoikosa Chadema amefanikiwa kuikata akiwa ACT, alitakiwa kuondoka uongozini na hicho cheo chake, lakini kwa kuondoka yeye na kukiacha hicho cheo, iko siku kitawatokea puani mbele ya safari.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nimekuelewa sana
 
Mfumo wa uongozi katika ACT-Wazalendo siyo wa ajabu maana vipo vyama huko duniani vina mfumo huo, mfano ANC ya Afrika Kusini. Kwamba, anakuwepo Mwenyekiti wa Chama na pia kuna Kiongozi wa Chama. Lengo hapa ni kugawa madaraka iwapo chama kitashika dola. Kwa mfumo huu Kiongozi wa Chama anategemewa kukiongoza chama katika kugombea nafasi ya u-Rais, na ikitokea akashinda, anakuwa tofauti na Mwenyekiti; hapa wanaepusha Rais wa nchi kuwa Mwenyekiti wa Chama. Kwa mfumo huu imekuwa ni rahisi kwa ANC kumdhibiti Rais wao akifanya madudu akiwa madarakani. Haya yametokea kwa Thabo Mbeki na hata Jacob Zuma.
 
Kiongozi wa chama kwa ACT ndiyo mkuu wa chama ndiyo Mwenyekiti

Ni Mkubwa kuliko Mwenyekiti. Ni Supremo Leader kama vile Ayhatolla kule Iran.

Kisiasa amefanya kosa kubwa sana ambalo atalijutia huko mbeleni. Akamulize Mabere Marando yaliyomkuta NCCR Mageuzi ..... Au Maalim Seif kule CUF ..... Historia huwa inajirudia.
 
Atakoma
 
Kiongozi wa chama ni kama Ayyatollah wa Iran.
Huu mfumo Zito ameiga Iran Mwenyekiti anakuwepo ila Kiongozi anakuwa na nguvu zaidi. Hata Iran Rais wa Iran hawezi mfanya kitu Ayattolah.

Mfumo wa kiduanzi sana wa walafi wa madaraka
Zitto ni mdini sn alienda kucopy Iran
 
Back
Top Bottom