Mzawa Halisi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 637
- 361
Umesomeka vizuri. Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu sana, nikisoma maoni ya wengi humu wanaopingana na Zitto's bid ni kwamba wanahofia chama chao kisisimamishe mgombea ambae ataenda kuwa Rais kivuli wa CCM. Binafsi sina ushahidi wowote kwamba Zitto anatumika na CCM lakini kama anataka kufanikisha azama yake ya kuwa Rais wa taifa letu, ni muhimu sana akaanza kazi sasahivi ya kuwaondoa mashaka watanzania juu ya hisia hizi ambazo inawezekana kabisa ni hisia potofu.
Mchambuzi,
Zitto mwenyewe ndiyo amechangia hizo hisia. Mwaka 2007 wakati wa issue ya Buzwagi, ZZK alikuwa shujaa wa vijana wengi wa kitanzania, lakini matendo yake ya karibuni yamemfanya kuwa mwanasiasa questionable.