Zitto Kabwe kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA endapo....

Pasco ulimuuliza ikulu anataka kwenda kufanya nini huyo zito?
 
Last edited by a moderator:
Pasco asante kwa taarifa,
Nimependa zaidi suggestion ya kutumia ZZK.
Kwakweli sisi waTanzania tuko nyuma yake, muda wa ukombozi unakaribia
 
Ulimuuliza kuhusu kashifa inayomnyemelea ya kula rushwa ya kumtetea mhando na wife yake?
Ndo maana mimi sioni sababu ya CHADEMA kubadili mgombea urais. Kama aliweza kupata asilimia 46% pamoja na madongo yote aliyorushiwa kwa 2015 CCM watakuwa hawana jipya tofauti na wakimweka mgombea mwingine
 
Pasco mbona maelezo yako hayakamilishi mtego uliouweka katika heading yako? ... "only if"
Hata hivyo binafsi sijaona kipya hapa ulichoripoti kwakuwa huo utaratibu aliokueleza Zitto ni utaratibu wa kichama ambao mwanachama yeyote anayetaka kupeperusha bendera ya Chadema lazima aupitie.

Naomba umshauri kwamba sasa inatosha, hakuna maana yoyote kila mara kutangaza nia yake ya kugombea uraisi kwakuwa tumeshamsikia, sasa ni muda muafaka aelekeze nguvu zake katika kujenga chama. Muda wa kuwazungumza wagombea uraisi utakapofika tutawaona na kuwasikia wengi sana, huu ukimya wao haumaanishi kwamba ni yeye pekee anayetamani kupewa idhini ya kukaa magogoni.

Tuna operation sangara pamoja na M4C, huu ndio muda muafaka tumuone akiwekeza nguvu zake kusukuma mbele mikakati ya chama kuchukua dola 2015.
 
Last edited by a moderator:
aende zake huko . Nani ampe urais huyo ndumilakuwili, akapige deal na Mhando huko sisi CHADEMA hatutaki wanafiki kama Zitto. Wakati wengine wanajenga chama chenyewe kinaota urais! pande za Ziwa Victoria hatukufagilii wewe Zitto. Dr. Slaa daima otherwise back to magambas
 
Sio walevi wote wanaovua nguo na kutembea uchi barabarani.Hata wanaodhani ni timamu hufanya hivyo hivyo
 
Umesomeka vizuri. Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu sana, nikisoma maoni ya wengi humu wanaopingana na Zitto's bid ni kwamba wanahofia chama chao kisisimamishe mgombea ambae ataenda kuwa Rais kivuli wa CCM. Binafsi sina ushahidi wowote kwamba Zitto anatumika na CCM lakini kama anataka kufanikisha azama yake ya kuwa Rais wa taifa letu, ni muhimu sana akaanza kazi sasahivi ya kuwaondoa mashaka watanzania juu ya hisia hizi ambazo inawezekana kabisa ni hisia potofu.
 
Pasco Kwa kweli kama atafata taratibu na chama chake kikiona kuwa anafaa kupeperusha bendera hata mimi namuunga mkono.. labda anaweza kuwa mkombozi wa Watanzania.. Naamini viongozi na wanachama wa CDM wako makini na wanafanya mambo kwa uhakika so watafanya maamuzi ya uhakika katika hili... Hata kama ana kasoro kila binadamu anazo za kwake.. huyu kijana namwona kama anafaafaa hivi......
 
Last edited by a moderator:
Si Kabwe, si Membe, si Slaa, si Sitta, si Pinda; bado tuna kazi kubwa ya kutafakari kwa makini ama sivyo nchi hii itazidi kudidimia!
 
kama kawaida wabongo tulivyo! hawa wanaotajwa humu ni tofauti na watakaoingia magogoni 2015!
 
"Presidential hopeful" halafu jina lake linakinaisha kwa kutajwa sana, what a contradiction! Hapo kwenye suggestion ya zzk kwangu mimi unanikumbusha zana za kilimo hiki kilikuwa ni kiwanda maarufu huko mbeya ua unataka kuunganisha na sera ya kilimo kwanza maana watu wanaotumiwa wana mambo makubwa kwelikweli kuwavutia na kuwafurahisha ma paymasters wao.
 
Update 1.

Sifa za kiongozi kwa mujibu wa mmoja wa Ma Great Thikers wakuu na wa ukweli humu JF.

Mkuu Pasco,
Kama umenisoma vema nimesimama katika hoja ya kuwa kutangaza nia ya urais si kosa. Ni haki kabisa na kwa namna yoyote ile inabaki kuwa haki ya mtu.

Nikumbushe kuwa katika uongozi kuna mambo mengi sana yakuzingatia.
Baadhi ya vitu vinavyomtengeneza kiongozi ni kama Charisma(haiba), popularity(umaarufu), intellectual (weledi) n.k.
Ukicheza karata vema kwa vitu hivyo unaweza kufanikiwa katika siasa.

Muhimu sana ni 'intellectual' ambayo si degree tu, bali kiongozi anavyoweza kuji-present, present his or her ideas, communication, emotion nk.
Lakini pia katika siasa kuna kitu wanasema ni 'political strategy' mkakati wa kisiasa na huu hufungamana sana na timing

Unaweza kuwa na vitu vyote lakini ukashindwa kufikia matamanio kwakukosa kitu kidogo tu, political strategy.
Sijui kama nimeeleweka!

ZZK ana
1.Charisma(haiba)
2. Popularity(umaarufu)
3. intellectual (weledi)
4. 'Political strategy' mkakati wa kisiasa
5. Timing
 
Cdm na jf kama watu hawajui , imejaa jopo la watu walio kamilika mpaka inatia raha. Kama wewe ni snitch tutakufahamu hata bila ramli.
 
Wanabodi,

MY Take.
ZZK anazo sifa zote za rais tumtakaye kwa mujibu wa sifa zilizoainishwa na wana jf wenzetu, Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji, na muda muafaka ukifika, ZZK atakapo tupa karata yake, miongoni mwa endorsment atakazo pata, ni ya Pasco wa JF!.

Kwa vile mimi sina chama, sio mwanachama, mshabiki, wala mkereketwa wa chama chochote, kwa Chadema nitaiunga mkono bid ya ZZK!. Kwa CCM bado namshabikia sana EL asimamishwe, na kama ni kweli afya yake ni mgogoro kuhimili mikiki mikiki ya 2015, then namshabikia Membe!. Kwa CUF na NCCR Mageuzi, nawashauri, wasi waste time and money kwenye presidential bid ili kuzipunguza kura za ushindi, kwa 2015, it won't work!.

Wale mnaendelea kumbeza ZZK, endeleeni, ili kwa sisi tuliofuatilia safari ya Barak Obama, toka alipoanzia, alipo pitia na hatimaye hapo alipofikia, mtakubaliana na mimi kuwa hii bid ya ZZK, siyo ya kubezwa hata kidogo!.
"Where there is a will, there is a way!".

NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.

Mtu mzima Pasco,
Heshima mbele,
Hivi kutoa endorsement kabla hata hujajua jopo zima la wagombea, huoni kwamba unaweza kuwa unajiandalia mazingira ya kujilaumu?

Halafu toka lini swala serious kama urais likawa swala la kishabiki? Unajua mkuu ushabiki hutumia moyo zaidi ya ubongo. Mimi ni shabiki wa Yanga na sina sababu yoyote objective ya kuwa Yanga zaidi ya moyo wangu kuridhishwa tu na Yanga. Hivi mkuu kweli urais tunaufanya kama Simba na Yanga? Are we on the right track?
 
Jamani eee!hizi thread za zitto na urais zimetuchosha sasa!hebu jadilini mambo mengine,mwacheni huyo mwenye ndoto za kuwa Amiri jeshi. Aendelee kuziota!.
 
Back
Top Bottom