Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,695
- 1,696
Update 1.
Sifa za kiongozi kwa mujibu wa mmoja wa Ma Great Thikers wakuu na wa ukweli humu JF.
ZZK ana
1.Charisma(haiba)
2. Popularity(umaarufu)
3. intellectual (weledi)
4. 'Political strategy' mkakati wa kisiasa
5. Timing
@Pasco umewahi kusikia usemi "Show me your friends and I will tell you who you are?"
1. Zito ana haiba ni sawa ila hujasema haiba yake inatokana na nini? Can you tell?
2. Popularity sawa. Lakini unatokana na nini? Kuwa Rais umaarufu wako unatakiwa utokane na watu kwa jibnsi unavyowatumikia. Papa Msofe, Diamond, Wema sepetu nk wote ni maarufu pia.
3. Weledi si intellectual. Weledi ni Professionalism. Ukiweka wazi supporting arguments zako huenda tukakuelewa.
4. Strategy . . . . Mikakati inaweza ikafanya kazi au isifanye. Mikakati hubadilika kutokana na mazingira. Labda ufafanue.
5. Timing? Mifano inatakiwa.
Kuwa Presidential Material unatakiwa uwe ni Mtu wa Watu kama MKJJ alivyogusia kidogo. It is all about Good Leadership. Kiongozi wa Watu ni Kiongozi wa namna gani?
1. Kiongozi wa watu ni yule ambaye akisema watu wanamsikiliza no matter kama ana position au hana. Mandela aliongoza akiwa gerezani.
2. Kiongozi wa watu ni yule ambaye anapigania maslahi ya watu wake no matter what. Japokuwa kuna baadhi ya sheria dhalimu, Kiongozi wa kweli ataweka mbele maslahi ya watu wake bila kujali sheria au kanuni even if it means kuitwa dictator.
3. Kiongozi wa watu ni yule ambaye analeta mabadiliko kwa ku-influence au kushawishi na watu wakakubali kwa hiari kwa moyo mkunjufu. Haitaji kutumia nguvu, sheria wala, hila au vyombo vya dola kuwashawishi watu.
4. Kiongozi wa watu ni lazima awe Muadilifu na uadilifu wake uwe wa asili unaotokana na utu wake na wala si wa woga wa yeye asije kuonekana si muadilifu (Unafiki)
5. Kiongozi wa watu anaongozwa na utashi na dhamira ya kweli ya kuwatumikia watu wake. Hana ajenda ya siri. hategemei fadhila wala malipo wala gains zozote: Mahatma Gandhi was such a leader.
6. Kiongozi wa watu lazima awe mbunifu wa kutatua matatizo ya watu wake. Awe na ndoto na maono ya nini hasa angependa awafanyie watu wake. Ni lazima aguswe na matatizo ya watu wake na ayachukulie kama ni matatizo yake binafsi.
7. Kiongozi wa watu, hana makundi kwa kuwa anaongozwa na dhamira na utashi wa kutumikia watu wake.
8. Kiongozi wa watu yuko tayari kuwasikiliza watu wake na kujirekebisha pale anapokosea kwani yeye ni sehemu ya hao watu.
9. Kiongozi wa watu atajitahidi kuwa na timu ya viongozi walio na sifa zinazofanana na zake na si viongozi wa kupewa shukrani au ambao anawafahamu kwa namna moja au nyingine.
10. Kiongozi wa watu, anaongoza watu na si taasisi, shirika, wizara nk. na hivyo anatakiwa awe na hekima katika kuwaongoza na kufanya maamuzi.