Zitto Kabwe kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA endapo....

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,

Nimekuwepo Dodoma kwa haya na yale na miongoni mwa mengi, nimepata fursa kuzungumza na ZZK kuhusu his presidential bid ya 2015!.

Ame confirm bila kuuma maneno kuwa ni kweli yeye ni "Presidential Hopeful" na kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, atatupa karata yake kwenye "presidential bid" kupitia tiketi ya Chadema!.

ZZK amethibitisha kuwa atazingatia sheria, taratibu na kanuni zote za kuomba kuteuliwa kupitia chama chake cha Chadema na kunihakikishia kuwa iwapo hatapitishwa, atamuunga mkono kwa asilimia 100% mgombea yoyote atakayepitishwa na chama chake cha Chadema!.

Kauli hiyo ya ZZK, ni uthibitisho kuwa mwamuzi wa mwisho wa ni nani atasimamishwa kupeperusha bendera ya Chadema kwenye urais wa 2015, utafanywa na Chadema na sio ZZK.

Sifa za kiongozi kwa mujibu wa mmoja wa Ma Great Thikers wakuu na wa ukweli humu JF.

Mkuu Pasco,
Kama umenisoma vema nimesimama katika hoja ya kuwa kutangaza nia ya urais si kosa. Ni haki kabisa na kwa namna yoyote ile inabaki kuwa haki ya mtu.

Nikumbushe kuwa katika uongozi kuna mambo mengi sana yakuzingatia.
Baadhi ya vitu vinavyomtengeneza kiongozi ni kama Charisma(haiba), popularity(umaarufu), intellectual (weledi) n.k.
Ukicheza karata vema kwa vitu hivyo unaweza kufanikiwa katika siasa.

Muhimu sana ni 'intellectual' ambayo si degree tu, bali kiongozi anavyoweza kuji-present, present his or her ideas, communication, emotion nk.
Lakini pia katika siasa kuna kitu wanasema ni 'political strategy' mkakati wa kisiasa na huu hufungamana sana na timing

Unaweza kuwa na vitu vyote lakini ukashindwa kufikia matamanio kwakukosa kitu kidogo tu, political strategy.
Sijui kama nimeeleweka!

ZZK ana
1.Charisma(haiba)
2. Popularity(umaarufu)
3. intellectual (weledi)
4. 'Political strategy' mkakati wa kisiasa
5. Timing

Na hii ni sehemu tuu ya mchango wa Great Thinker mwingine mheshimiwa sana kuhusu sifa za kiongozi atakayetufaa kwa 2015, nimeedit kwa kupunguza zile sifa mimi nilizoziona sio necessary na kubakisha zile za muhimu tuu ambazo zote ZZK anazo!.

Sifa za huyu mtu ambaye tunataka aje na kuwa Rais wetu sifa moja - MTU WA WATU.
a. Anayetokana na Watu: watu (wananchi) wanamtambua uwezo wake, vipaji vyake na ni wao ndio wanamsukuma kuwatumikia. Na yeye akitambua uzito wa utumishi huo anatambua uzito (the gravity) ya wito wa kuwatumikia watu. Kwa hiyo anakuwa ni 'hero' anakubali kuwatumikia basi huyo anakuwa ni kiongozi wa 'watu'.

b. Anayeongozwa na utu wake: Kiongozi wetu ajaye ni lazima aongozwe na kitu kimoja kinachotuunganisha wote - utu wetu. Hatutaki wala kustahili kiongozi anayeongozwa na "uenzetu huu" unaoangalia dini, kabila, rangi, hali ya maisha, elimu au ujiko wa kisiasa. Mtu wa watu ni yule anayejali UTU WA WATU wote.

c. Anayewejabika kwa watu: Sasa kiongozi ajaye si yule ambaye anatoka kwa watu au anaongozwa na utu wa watu wote bali zaidi ni yule anayewajibikwa kwa wananchi wake. Tunataka kiongozi ambaye anatambua na kukubali kuwa yeye ni mtumishi wa wananchi.

Tunaposema "mtu wa watu" hatumaanishi hatumaanishi yule mwenye kugongewa, kupongezwa au kushangiliwa na watu. Bali yule ambaye anatoka kwa watu, anajali utu wa watu wote na anatambua kuwa anawajibika kwa watu.

Huyu ndiye MTU WA WATU!.

Pia Mkuu sana, ametusisitiza kiongozi ajaye, awe na uwezo.
Mwaka 2015 Watanzania wanahitaji Rais ambaye atavunjilia mbali sera zilizoshindwa za CCM, kuifumua mifumo mibovu ya kiutawala iliyodumu kwa miaka karibu hamsini sasa na kutupa uongozi wa kutufanya tujiamini kuwa tunaweza na akatuongoza katika kujenga taifa la kisasa lenye kujali utu wa watu na siyo vitu vya watu.

Tunahitaji rais na pamoja naye viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. RAIS ajaye wa Tanzania ni lazima awe na UWEZO; UMRI wake usihusishwe kabisa na uwezo huo.
MY Take.
ZZK anavyo vigezo, anao uwezo na anazo sifa zote za rais tumtakaye kwa mujibu wa sifa zilizoainishwa na wana jf wenzetu, Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji, na muda muafaka ukifika, ZZK atakapo tupa karata yake, miongoni mwa endorsment atakazo pata, ni ya Pasco wa JF!.

Japo mimi nina chama, lakini niko kama Mwalimu Nyerere, ni mwanachama tuu na sio mshabiki, wala mkereketwa wa mtu yoyote, Chama changu kikitusimamishia mtu wa hovyo, nitaiunga mkono bid ya ZZK!. Kama CCM bado namshabikia sana EL asimamishwe, na kama ni kweli afya yake ni mgogoro kuhimili mikiki mikiki ya 2015, then namshabikia JPM!. Kwa CUF na NCCR Mageuzi, nawashauri, wasi waste time and money kwenye presidential bid ili kuzipunguza kura za ushindi, kwa 2015, it won't work!.

Wale mnaendelea kumbeza ZZK, endeleeni, ili kwa sisi tuliofuatilia safari ya Barak Obama, toka alipoanzia, alipo pitia na hatimaye hapo alipofikia, mtakubaliana na mimi kuwa hii bid ya ZZK, siyo ya kubezwa hata kidogo!.
"Where there is a will, there is a way!".

NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.
Pasco
 
nathubutu kusema ni bora tutawaliwe na fisadi kichwa cheupe kuliko huyo ndumilakuwili kuwa rais...
 
Wanabodi,


Nimekuwepo Dodoma kwa haya na yale na miongoni mwa mengi, nimepata fursa kuzungumza na ZZK kuhusu his presidential bid ya 2015!.

Ame confirm bila kuuma maneno kuwa ni kweli yeye ni "Presidential Hopeful" na kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, atatupa karata yake kwenye "presidential bid" kupitia tiketi ya Chadema!.

ZZK amethibitisha kuwa atazingatia sheria, taratibu na kanuni zote za kuomba kuteuliwa kupitia chama chake cha Chadema na kunihakikishia kuwa iwapo hatapitishwa, atamuunga mkono kwa asilimia 100% mgombea yoyote atakayepitishwa na chama chake cha Chadema!.

Kauli hiyo ya ZZK, ni uthibitisho kuwa mwamuzi wa mwisho wa ni nani atasimamishwa kupeperusha bendera ya Chadema kwenye urais wa 2015, utafanywa na Chadema na sio ZZK.

MY Take.
ZZK anazo sifa zote za rais tumtakaye kwa mujibu wa sifa zilizoainishwa na wana jf wenzetu, Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji, na muda muafaka ukifika, ZZK atakapo tupa karata yake, miongoni mwa endorsment atakazo pata, ni ya Pasco wa JF!.

Kwa vile mimi sina chama, sio mwanachama, mshabiki, wala mkereketwa wa chama chochote, kwa Chadema nitaiunga mkono bid ya ZZK!. Kwa CCM bado namshabikia sana EL asimamishwe, na kama ni kweli afya yake ni mgogoro kuhimili mikiki mikiki ya 2015, then namshabikia Membe!. Kwa CUF na NCCR Mageuzi, nawashauri, wasi waste time and money kwenye presidential bid ili kuzipunguza kura za ushindi, kwa 2015, it won't work!.

*NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.

ungezingatia hayo kwenye RED (NYEKUNDU) nadhani na wewe ungetulia kimya. lakin kwa kuwa hujazingatia hayo , basi na wewe umetumwa na huyo ZITTO.
 
2015,bado sana!zzk anatakiwa atumie busara na kutengeneza njia kwanza,na siyo kuropoka na kutafuta u'popular'!cdm inavichwa vingi vya maana vinavyofaa kabisa for presidecy,but vimetulia!why zzk?there must be something under the carpet!tuweni makini na huyu jamaa,na busara za kumkaripia zisipotumika huyu jamaa ataharibu chama na kudhoofisha nguvu na njia ya ushindi kwa chadema 2015.
 
Pasco,
wewe unasema siyo mwanachama wkt unamsapoti Lowassa, halafu unatuletea uzushi hapa ili utugawe wanachadema? nenda zako na ccm yako. CHADEMA hawahitaji wewe uwaambie nani anafaa kuwa mgombea wao bali wana taratibu zao. Kama taratibu zikifuatwa hakuna shida. Wewe kwanza ni mchumia tumbo sijui(waandishi makanjanja) wanaoingia kwenye mikutano bila mwaliko. Labda Lowassa au Zitto amekuhaidi Post tutajuaje? Si unakumbuka kipindi cha uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ulivyokosa msimamo, mara useme Sioi mara Nassary. Usituletee mambo ya Sheick Yaya ndani ya CHADEMA, hayo unaweza peleka CCM, kwani CHADEMA kuna utaratibu na tuna umoja. Na kamwe CCM kwa propaganda zao hamtaweza kukigawa CHADEMA.
 
@Pasco 3 years to come ni muda mrefu na mengi yanaweza kutokea. Politics can change and take a complete turn kiasi kwamba hata endorsement yako ikabadilika.

I prefer the fact kuwa: We cross the bridge when we are there. Time will tell. Time. Timex.
 
mbona wewe Pasco na huyu zito wako mnawashwa sana na uraisi? hivi Mungu amewagonga mihuri kuwa mtakuwa hai hiyo 2015? hivi hamna kazi nyingine za maana za kufanya na kuona hili ni dili sana?
 
Last edited by a moderator:
Habari ya ovyo, tena ya kiimla na yenye nia zile zile za kuchumia tumbo kwa gharama ya ukombozi wa TZ.
 
Back
Top Bottom