Ni kweli mkuu lakini nijuavyo mimi Mh.Zitto pia alihakikishiwa usalama wake kwa kuwa zile info hazijatoka mbali sana na kwa wanaCCM so he will be safe!Hofu yangu ni kwamba kama hizo document bado hajashare na mtu, basi usalama wake unaweza kuwa hatarini sana. Najua hao walio mbioni kutajwa ni watu wenye influence kubwa kwenye majeshi ya nchi na hata usalama wa taifa. Kwahiyo hawashindwi kumfanya chochote, na bado wakawa na imani kwamba litapita kama upepo. Kwa upande mwingine naona kama kwa usalama wake Zito alipaswa kuyataja hayo majina. Kwa kutokutaja amejiweka pabaya zaidi kiusalama.