Zitto aliponda baraza la mawaziri kuhusu CHC

Mbubge wa MwibaraN Mh Lugala ameichana chana serikali ya chama chake kwa kutaka kuiibia nchi kwa kuiingiza CHC kwenda TR na kuifanya isiwajibike wakati TR hawajui hata mashirika mangapi yako chini yake na wala hawana cerificte zake. Moto umewaka sana na sasa Hamad Rashid wa CUF anaendelea kurusha madongo kwa serikali. Baraza la mawaziri limeumbuka na Mkullo anaabgalia chini na koti linampwaya kwa aibu!

Huyu si CCM B?
 
Zitto umetumia taaluma yako ya Uchumi vizuri,Nimeshangaa sana Msajili wa hazina hana Records Muhimu za mashirika anayoyasimamia? finance minister nae ame-behave very unprofessionally leo,hii ilikua aibu!

Ben ukishangaa ya Mussa je ya Farao yatakuwaje
kama mkuu wa nchi na waziri wake mkuu hawajui ni kwa nini watanzania ni maskini sembuse Msajili wa Hazina ajue hisa za Serikali kwa mashirika ziko wapi na ni ngapi mbona unampa kazi ngumu sana
 
Mbunge wa mwibara kanyea ugali , hana chenga wala nini. Kaongea ukweli mtupu. Shame to magamba kimyaaa. Mkulo koti linambana sasa. Maslahi za taifa kwanza.

Safi sana CDM juu juu zaidi wabunge kama hawa ndio tunaowahitaji sio wa kusinzia safi sana.
 
Nimeipenda kauli ya zitto "simumunyi maneno....na ninarudia tena baraza la mawaziri limeshinikizwa na ma robbist na tusikubali kuendeshwa na ma robbist"
 
kama Msajili wa hazina hana records muhimu za mashirika anayosimamia, vile vile katibu mkuu na hatimaye waziri wa Fedha hana taarifa sahihi. Basi hiyo ni khatari kubwa sana kwa mustakabali wa nchi. Bila shaka kuna ulaji mzito hapo ndio maana hawataki kuweka mambo hadharani.

Nashauri viongozi wote wakuu wa Wizara hio ya Fedha kuanzia waziri, Katibu mkuu na watendaji husika wafukuzwe mara moja na kushitakiwa kwa kuficha ukweli.

Poleni sana WaTanzania. kazeni buti na kuikomboa nchi yenu
 
Du Nimefarijika kuona tuko na Zitto humu kwenye hii thred. Bilashaka anatufuatilia kwenye mobile yake. Mh Zitto tujuze mkuu toka huko mjengoni. Huku tupo makini tunafuatilia kupitia FJ
2011-06-23_1231.png

2011-06-23_1231.png
 
Zito endelea kuwanyima usingizi hao,napenda unavyojenga hoja kwa ujasili.Halafu huyo mama kazi itamshinda.
 
Wadau naona mama anaanza kurejea kwenye rythm ya SS(standard and speed) ingawaje bado lakini kuna some changes.Mjadala wa leo ulikuwa mgumu sana kwani TR na CHC ni baba na mtoto, leo baba alikuwa anaumbuliwa, lakini kikubwa zaidi waumbuaji ni kina Zitto ambao mama makinda alikuwa anawa-hate sana before , lakini tangu jana ameanza kuonyesha kuwa FIRM.Keep it up mama utarejea kwenye standard
 
Issue sio kuwanyima usingizi maana si uliona majuzi Wasira alikua amelala pamoja na mchakamchaka. Zitto send them a clear message on how wrongly they are taking our country na hiyo proof wanayotaka muwape hivi mkiwapa watachukua hatua gani? mbona maelezo ya Mhe. Lema imekua archived na walishupalia athibitishe kwamba kiongozi mkubwa amelidanganya bunge?sema Zitto hata kama hawatasikia watanzania tunayasikia...........
 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma na mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe (Chadema) amewasha moto bungeni asubuhi hii.

Zitto ameliponda baraza la mawaziri kuwa wamechakachua ripoti ya kamati yake na hivyo amewataka kuleta ripoti halali ya kamati hiyo. Kwa kweli hali ni tete bungeni. Lukuvi alijaribu kusimama akaambiwa akae chini kwani yeye sio spika. Zitto amedai yeye hafinyangi maneno.

Ngoja tuone. Yaani ni balaa ndani ya ukumbi wa bunge.
Kilichonifurahisha leo ni utulivu usiotarajiwa wa huyu Spika aliyeteuliwa na kina Magamba kutetea maslahi ya vibakauchumi. Leo ame Behave tofauti na siku nyingine ambapo huonekana kama ngome ya wahujumu wa nchi hii. Leo ameonyesha utulivu, amezima "Vurugu" za kina Lukuvi na wenzake na kuyaweka mambo sawa. Pamoja na Zitto kupewa hadi tarehe 29 kuthibitisha tuhuma, Waziri Mkullo a.k.a. Mmalawi alionekana wazi kuchanganyikiwa na alikuwa mpooole sana hadi kukubali kurekebisha kipengele kilichokuwa kikibishaniwa.
My Take:
Mama huyu amshazisoma alama za nyakati na pole pole anaelewa kwamba kuwakingia kifua mafisadi wa CCM ni sawa na kuukingia kifua mkuki wa moto. Nampa pole kwa sababu Bunge analoliongoza sasa ni gumu kuliko hata lile la mtangulizi wake Sitta.
Hakuna kulala mpaka kieleweke.
Viva CHADEMA, Viva Zitto Kabwe. A Luta Continua. God Bless Tanzania.
 
unajua 2fike mahala 2we kama watu wazima wenyefikara na uchungu wa nch yetu, kama mbunge wa mwibara, uyo rukuvi anachofanya akiendani na hadhi aliyonayo amekuwa kama mama wa ginigi anataka kuwanywesha watanzania unga wa ndere? zito big up kazeni uzi sisi watanzania tunaimani na ninyi sana 2 na tupo tayari uwa pamoja na hao yanga(ccm) wanao jua wanafanya nini .nachukia kumwona mbunge anatoa hoja kwa kumponda mbunge mwenzake ohoo eti anatafuta amaarufu wa kisiasa? how? wakati mpaka hapo alipo mjengoni ni maarufu kwani kapitishwa na mafisadi au watanzania wenye reson?
 
CHC inaangalia mali zipi zilizobaki? Majengo karibu yote ya ilyokuwa NBC ya ukweli yaliuzwa.

if i giot them right CHC inasimamia mashirika yoote yaliyouzwa ambayo with them serekali have less than 50 % share..

kitu ambacho zitto na wajumbe wenzake wa kamati wameelezea jinsi serekali ilivyo na mpango wa siri wa kuyapoteza mashirika na hisa zake kama walivyofanya hadi sasa kwa airtel - kwa kuiua CHC na kuhamishia majukumu yake kwa Treasury Register TR...

kwamba TR hana hata document zinazoonyesha mchakato wa hisa...

not only that kuwa TR kikawaida huwa hana balance sheet ambayo inaonyesha / inasaidia tracking ya finances

hivyo baada ya muswada wa serekali ambao ulikuwa unaitaka CHC iwe ya mpito na ife baada ya miaka mitatu kisha kukabidhi shughuli zake kwa laizyfaire TR ilikuwa na lengo na kujigawia mali za umma...

hivyo mpango huu ambao zitto ameuita kuwa ana uhakika kuwa umeamuliwa kilobbist na baraza la mawaziri ulikuwa na lengo hilo...

Zitto mara kadhaa ametakiwa kuprove na mkuchika na lukuvi kuwa aprove hiko kitu...

makinda aklijaribu kumrtetea Zito lakini akang'ang'ania ana uhakika kuwa kuna lobying imefanyika...

na hivyo kama si kweli serekali iseme hili jambo lilicrop up tokea wapi..maana hata mapendekezo ya bunge na kamati yake ambayo iliishakutana na waziri haikusema hivyo....

lukuvi akang'ang'ania kuwa zito bado adhibitishe

lissu akaingilia kutoa taarifa kwa kanuni kuwa serekali ambayo ndiyo inalaumiwa na imetakiwa kutoa statement what happened should act...spika akamwokoa lukuvi kuwa bunge haliingilii utendaji wa serekali...

hatimaye wabunge wa CCM ambao leo naomba tuwapongeze waliokuwa kwenye kamati waliongea kwa uchungu kusisitiza ya zitoo..(MAKOFI TAFADHALI)

WAzee wa kupiga CHENGE na MKONO walikuwa wanahaha pembeni ya mkulo wakimshawishi jinsi ya kupinda..

hatimaye Mkulo akaambiwa arekebishe..na akarekebisha kuwa

1. CHC itafanya kazi kwa miaka mitatu YA MPITO na kuangaliwa uhitaji.....

zITTO AKAINGILIA KATI KUWA ISIWE YA MPITO, serekali ikakubali kuondoa neno mpito...

2. waziri akaondoa sehemu ya sentensi "kuhamishiwa shughuli kwa TR"

MAKOFI TENA TAFADHALI KWA CHADEMA, ZITTO, TUNDU LISSU...NA WAJUMBE WA KAMATI YA mashirika ya umma chini ya mh zitto...

naomba kuwasilisha!
 
Laiti kama Wabunge wote wangesimamia Maslahi ya Taifa Nchi ingekuwa mbali sana,Leo nimeamini Shujaa mmoja akifa wanazaliwa kumi tulikuwa na kina Mwakyembe,Sitta wote wakatusaliti leo nimeona ujio wa Shujaa mpya Mbunge wa Mwibara ccm huyu kaonyesha uzalendo wa khali ya juu bila kujali itikadi za Chama chake huu ni Ujasiri wa Khali ya juu nampongeza sana na Mungu atamlipia kwenye Maslahi ya Taifa tuliangalie Taifa.Big up Zitto kwa kazi nzuri saiv kuna Traitor mpya Hamad Rashid wa Cuf mchango wake ni wakinafiki na hana Uzalendo hata kidogo.
 
kama Msajili wa hazina hana records muhimu za mashirika anayosimamia, vile vile katibu mkuu na hatimaye waziri wa Fedha hana taarifa sahihi. Basi hiyo ni khatari kubwa sana kwa mustakabali wa nchi. Bila shaka kuna ulaji mzito hapo ndio maana hawataki kuweka mambo hadharani.Nashauri viongozi wote wakuu wa Wizara hio ya Fedha kuanzia waziri, Katibu mkuu na watendaji husika wafukuzwe mara moja na kushitakiwa kwa kuficha ukweli.Poleni sana WaTanzania. kazeni buti na kuikomboa nchi yenu
Mkuu hilo neno "kufukuza" na "kujiuzulu" hayatumiki tena hapa jamvini na ktk inji hii. Utamaliza wino bureee!! Hakuna msamiati huo tena chini ya Magambaz...!
 
Back
Top Bottom