Zitto aliponda baraza la mawaziri kuhusu CHC

Hao wameshazoea kutuletea uongo bungeni naona siku nyingine watakuwa seriously...........ndio kawaida yao hao.....
 
Wabunge wa chadema vivaaaa, moto tunauona, please ongezxeni crdt za kuonyesha uwezo wa kuongoza nchi kuanzia msimu ujao,
 
Taarifa yako nzuri, lakini elewa kuwa vifupisho hivyo havieleweki na kila mtu na wala si standard!...right?
Mkuu uko sahihi mi ni mojawao nisiyejua chc nikawa naendelea kusoma comment za wana jf labda kuna atakayetoa msaada tutani
 
Zito anaonekana ana mzaha bungeni lakini mambo yake yako juu sana. Kwanza sijawahi kumuona anasinzia bungeni all the time yuko active. Anafatilia vilivyo mijadala ndiyo maana anapata maswali ya mara mara. Hayo magamba yanazidi kusinzia bila ya kujua kuwa wenzao wako serious na kazi yao .Zito ,Tundu Mnyika naomba muendelee kuyapeleka magamba mpaka yaamuke. Pia naomba muamshe mbunge wangu Kevin Donard maximilian jimbo la Geita. Mwambieni hicho kimywa chake wanageita wanamsubiri kwa hamu sana.
font color yako mkuu haifai kabisa labda kama hutaki watu wasome ulichokiandika...
 
Hao wameshazoea kutuletea uongo bungeni naona siku nyingine watakuwa seriously...........ndio kawaida yao hao.....
Mkuu yaani walichokifanya kama ing'ekuwa nchi zingine leo kuna mtu angeachia ngazi....lakini kwa hapa bongo litapita na maisha yataendelea...
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe(Chadema) jana alichafua hali ya hewa bungeni na kuzua mvutano mkubwa kati yake na mawaziri baada ya kueleza kuwa baraza la mawaziri limeshawishiwa na watu kulifuta Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa faida ya wachache.
Zitto alitoa kauli hiyo iliyomgharimu na kutakiwa kuithibitisha ifikapo Juni 29 mwaka huu, wakati akichangia azimio la serikali la kuongeza muda wa uhai wa shirika la hilo lililosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo.

Akiwa mchangiaji wa kwanza katika mjadala huo, uliosomwa baada ya kipindi cha maswali na majibu, Zitto alirudia mara tatu kauli hiyo na kuwataka wabunge wasikubali kupitisha azimio hilo kwa kuwa ni 'wizi kwa rasilmali za taifa'.
Hoja ya kuliongezea muda CHC wa miaka mitatu na baada ya hapo lifutwe na kazi zake apewe Msajili wa Hazina (TR) sio bure, baraza la mawaziri limeshawishiwa ili watu fulani wanufaike," alisema Zitto na kuongeza: Mapendekezo hayo yaliletwa kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na zote ziliyakataa... Tukasema CHC iongezewe muda zaidi ili ifuatilie madeni na mali za mashirika kadhaa ambayo zimeonekana kuliwa.
"Ukitaka kuifuta leo, Mheshimiwa Spika, madeni ya mashirika ya umma yatapotea na naamini kuna watu wanafurahia jambo hilo kwani watanufaika. Tumewaagiza CHC wafuatilie madeni hayo, halafu hata kabla hawajaanza kazi, tunasema tunataka kulifuta baada ya miaka mitatu, siyo sahihi CHC ni jicho letu la kufuatilia ubadhirifu katika mashirika ya umma."

"TR (Msajili wa Hazina) ana majukumu mengi na tayari tumeona ameshindwa kufuatilia mashirika mengi. Kuna mashirika 25 na taasisi zingine kadhaa hana hati ya mashirika hayo wala hajui mali. Unawezaje kumwongezea majukumu kama huo siyo mpango wa watu kutaka kutuhujumu?"
"Naombeni waheshimiwa wabunge kwa umoja wetu, bila kujali tofauti za itikadi zetu, tulikatae azimio hili, limeletwa baada ya mawaziri kupitiwa na ma-lobbyist(washawishi). Halina manufaa kwa taifa, ni wizi na uporaji wa mali ya umma. Tuliliagiza shirika hilo lisaidie kufuatilia ubadhirifu kwenye mashirika ya umma, sasa leo tunataka kuiondoe hope (matumaini )yote kwa azimio hilo! Tusikubali,"

Baada ya kauli hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kapteni George Mkuchika alisimama na kuomba mwongozo wa spika, kisha akasema: "Mheshimiwa spika, natumia kanuni inayozuia mbunge kutoa maneno ya kuudhi na lugha chafu bungeni." Mimi ni mjumbe wa baraza la Mawaziri, sijafikiwa na mtu na pia naamini hakuna mmoja wetu aliyepitiwa. Mheshimiwa Zitto umetudhalilisha wabunge wenzio. Spika naomba mwongo wako."

Spika Anne Makinda akasema, "Waheshimiwa wabunge, kwa kuwa azimio hilo limekuja kwa dharura, naomba kwanza tusiingize mambo ambayo yatachelewesha utekelezaji wake. CHC inatakiwa kufa ifikapo Juni 30, sasa leo tupitishe kwanza muda huo ulioombwa halafu mijadala mingine iendelee baadaye. Mheshimiwa Zitto endelea."Zitto akaendelea, "Nasisitiza kwamba baraza la mawaziri limepitiwa na kufanyiwa lobbying (ushawishi). Ila, ninachosema ni wabunge kuwa makini na kutokubali kupitisha azimio hili kwa kuwa tunawapa ulaji watu,"

Baada ya kauli hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge), Wiliam Lukuvi aliomba tena mwongozo wa spika na kusema, "Nasikitika kusema kuwa hata baada ya wewe mheshimiwa spika kutoa mwongozo katika suala hilo, yeye (Zitto) ameendelea kurudia, maana yake kwamba ana hakika na kile anachokisema. Sasa, naomba atoe ushahidi." Spika alionekana pia kutojali ombi hilo na badala yake akamtaka Zitto aendelee kutoa hoja yake.

"Napenda kurejea kwamba, maamuzi haya ni ushawishi wa lobbyists, Kama sivyo, serikali ilete hapo mbele pendekezo la kamati lililoitaka liipe miaka mitatu shirika hilo na baadaye lifutwe na kazi zake zichukuliwe na TR. Tusiruhusu baraza la mawaziri kuendeshwa na lobbyists,"alisisitiza Zitto.
Baadaye Lukuvi aliomba tena mwongozo wa spika na kusisitiza Zitto atoe ushahidi akisema, "Cabinet (Baraza la mawaziri), kamati za bunge kazi yake ni kuishauri baraza la mawaziri na ushauri huo siyo lazima usikilizwe."

"Cabinet (Baraza) halifanyi kazi kwa shinikizo la mtu. Sasa, tunamtaka mheshimiwa Zitto aseme ni kina nani waliorubuniwa katika cabinet, na wamerubuniwa na nani? Baraza la mawaziri ni kikao huru ambacho hakina uhusiano wowote na watu wengine."

Lukuvi alipomaliza kuzungumza alisimama, Tundu Lissu (Mbunge wa Singida Mashariki- Chadema) na kuomba mwongozo wa spika akisema, "Mheshimiwa Spika, Kanuni ya 63 (3 )na (4) inaeleza kuwa mtu wa kwanza mwenye wajibu wa kuthibitisha hilo ni serikali. Lukuvi athibitishe kwa kiwango cha kuliridhisha bunge na baadaye Zitto ajitetee."

Malumbano hayo yalimwamsha Spika Makinda kwenye kiti chake na kueleza, "Nyie watu mnapenda sana kubadilisha mambo. Baraza la mawaziri haliwajibiki kwa bunge. Anayetakiwa kuthibitisha hapo ni Zitto na sasa namtaka alete uthibitisho huo, Juni 29 mwaka huu."Katika mjadala huo Zitto aliungwa mkono na wabunge kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Dk William Mgimwa wa Kalenga ambaye alilieleza Bunge kuwa azimio hilo la serikali ni kinyume na makubaliano ya Kamati ya Fedha na Uchumi.

"Hoja ya CHC kupewa miaka mitatu na baadaye kazi hizo zipelekwe kwa TR ni kinyume na makubaliano. Kwenye kamati tulisema hili lisifanyike ili TR asije aka-compromise, na huu ni usalama kwa shirika hilo," alisema.

Naye Mbunge wa Mwibara , Alphaxard Lugora (CCM) akichangia hoja hiyo alisema, "Mimi ni mbunge wa CCM na ni mjumbe wa Kamati ya Mashirika ya Umma. Lazima katika jambo hilo wabunge tuwe na uchungu na mali ya Watanzania. Nimepitia mashirika hayo na nimeona yanavyoliwa, TR hana hata certificate (cheti ) za hisa, nchi hii imefika pabaya."

Aliendelea, "Ubinafsishaji ni unyonyaji kwa Watanzania. Spika, ukiona mashirika yanafungwa na kuhamishwa majukumu, ujue kuna wizi unataka kutendeka. Kazi za CHC kuanza kufanywa na Hazina wakati tumeipa kazi ya kufuatilia madeni na mali zetu, huku ni kupotosha institutional memory (kumbukumbu za taasisi) kwa sababu kuna wizi unataka kufanyika."

Kwa mujibu wa Lugora, wabunge ni wawakilishi wa wananchi hivyo chochote kinachoanzia bungeni kikiharibika wao ndio wa kwanza kulaumiwa. Alisema ni bora CHC ikapewa kazi hiyo moja kwa moja au kwa kipindi cha miaka mitano ili ikamilishe kazi ya kufuatilia madeni hayo ya masharika ya umma yaliyobinafsishwa.

"Ushauri wangu, serikali ikubali kuwapa muda zaidi, iwe ya kudumu madeni yetu yatapotea bure. Kwa nini TR asichukue kazi za NSSF? Kuna nini CHC? Kama mashirika haya tunayoyaangalia wabunge yana wizi, yale ambayo hatuyachunguzi, kukoje?"
Baada ya malumbano hayo, Spika alimwita Waziri Mkulo kumalizia hoja yake na baadaye wakakubaliana kuwa shirika hilo lipewe muda huo wa miaka mitatu, kuanza Julai Mosi hadi Juni 30, 2014. Lakini, katika kipindi hicho serikali itakuwa inalichunguza shirika hilo na kupeleka ripoti yake bungeni kabla ya kufanya mabadiliko mengine yoyote.
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), amedai kuwa Baraza la Mawaziri limerubuniwa na watu wenye maslahi ya kuliua Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC), hivyo kubadili mapendekezo ya Bunge ya kulipa muda wa kutosha shirika hilo kukamilisha kazi zake.

Kwa kauli hiyo, Zitto ameingia matatani baada ya mawaziri kumtaka athibitishe ukweli wake na Spika wa Bunge, Anne Makinda amempa siku saba awasilishe ushahidi kwamba Baraza la Mawaziri lilishawishiwa kubadili uamuzi huo na watu ambao hakuwataja.
 
Hongera sana Zitto kwa kuwang'ang'ania; ng'ombe wa kilimo unaweza ukamfunga nira na jembe la pilau kulima lakini usije ukadhani atalima tu kwa sababu umemuwekea jembe. Wakati mwingine (kama siyo mara zote) lazima umchape chape kidogo ili aende hasa kwenye udongo mgumu! Leo Zitto kawachapa.
 
Kamata haoooooooooo! Wezi haoo lukuvi shule si amechakachua,uwezo wake wakufikiri ni mdogo sanaaa..........................
 
Hii imekaa vizuri sana Mdogo wangu Zitto na Mbunge wa Watanzania wote endelea kusema bila woga watakufukuza mpaka watachoka na hatimaye UKWELI UTAKUWEKA HURU.Haya shime wapenda ukweli wote tuendelee kumuombea kijana wetu ili azidi kutuelimisha niliwahi kuchangia kuwa huyu kijana anajua mengi maovu ya serikali na atazidi kutufumbua watanzania SAAFIII SAAANAAA.
 
*Atoa tuhuma nzito kwa Baraza la Mawaziri
*Spika Makinda ampa siku saba kuthibitisha


Na Grace Michael, Dodoma

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, (CHADEMA), ameingia katika mgogoro mwingine bungeni, baada ya kutoa tuhuma nzito dhidi ya
Baraza la Mawaziri kuwa maamuzi yake yanatokana na ushawishi wa watu wenye nia ya kuua mashirika ya umma.

Kutokana na kauli hiyo Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda, alilazimika kumpa mbunge huyo siku saba kuanzia jana kuthibitisha kauli yake.

Bw. Zitto alitoa tuhuma hizo bungeni jana, wakati akichangia azimio la kuongeza muda wa uhai wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).

Mbunge huyo alipinga azimio hilo lilitaka kuongezwa kwa muda wa miaka mitatu kwa CHC moja kwa moja kwa kutoa sababu mbalimbali.

“Jamani tulikubaliana vingine kabisa katika Kamati,leo kilicholetwa hapa ni kitu kingine. Kamati ya Fedha na Uchumi ilijadili na kutaka shirika hili lipewe muda zaidi kutokana na majukumu yaliyo mbele yake lakini hiki kilicholetwa hapa ni kitu kingine,”

“Wabunge kataeni haya maamuzi ya Baraza la Mawaziri, yametokana na kurubuniwa na watu wenye lengo la kuua CHC kwa ajili ya maslahi yao,"alisema Bw.Zitto na kuongeza

"Ikumbukwe kuwa chombo hiki kinaangalia mali za umma na mashirika lakini pia kuna kesi mbalimbali za watu ambao wanadaiwa na mashirika hivyo kwa kuja na hoja hii ni sawa na maandalizi ya wizi,” alisema.

Baada ya maneno hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. George Mkuchika, aliomba mwongozo wa spika kutaka Bw. Zitto athibitishe kauli yake.

Katika maelezo yake kwa Spika Waziri huyo alisema kauli ya Bw. Zitto imewadhalilisha mawaziri ambao wanafanya kazi kwa maadili na kwa kuzingatia maslahi ya nchi.

Alisema kauli ya maamuzi ya Baraza la Mawaziri kutokana na kurubuniwa yanaleta picha mbaya kwa watanzania ambao wao wamewaamini watendaji hao wakuu wa serikali.

Pamoja na maombi ya Bw. Mkuchika, Spika Makinda aliingilia kati na kumtaka Bw.
Zitto ajikite kwenye hoja na kutahadharisha kuwa kinachotakiwa ni wabunge kupitisha muda huo kisha utaratibu mwingine ufuatwe kujadili suala hilo kwa kuwa amebaini kuna hoja za msingi.

“Jamani tunachotakiwa kufanya hapa ni kuipa uhai kwanza CHC na baada ya hapo tutaangalia utaratibu mwingine kwa kuwa tukianza kubishana uhai wake utakufa...ni kweli hoja mnazozitoa ni nzito na za msingi,” alisema Bi. Makinda.

Hata hivyo Bw. Zitto aliporuhusiwa kuendelea, aliendelea kusisitiza kauli yake kuwa maamuzi ya baraza hilo yanatokana na ushawishi wa watu wasio na malengo mema na mashirika pamoja na mali za umma.

“Siwezi nikafinyanga maneno hapa, nina uhakika na ninachokisema, maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni matokeo ya malobbiest, kama serikali mnabisha leteni hapa mapendekezo ambayo yaliwasilishwa katika Kamati ya Makatibu wakuu na baraza la mawaziri...nasema tusiruhusu haya maamuzi ya mawaziri ambayo yametaliwa na mawazo ya malobbyist,” alisisitiza Bw. Zitto.

Kutokana na msimamo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Willium Lukuvi, alisimama na kuomba mwongozo wa spika kutaka kauli hiyo ithibitishwe kwa kutajwa mawaziri waliopitiwa na kurubuniwa.

Baada ya Bw. Lukuvi kuomba mwongozo huo Bi. Makinda alimpa Bw. Zitto muda wa siku saba kuthibitisha kauli hiyo.

“Mpaka tarehe 29, mwezi huu uwe umethibitisha hayo uliyoyasema,” alisema Bi. Makinda.

Pamoja na hatua hiyo ya Bw. Zitto, mjadala huo ulionekana kuwagusa wabunge wengi wakiwemo wa Chama tawala ambao walipingana na azimio hilo.

Katika michango yao wabunge hao walipinga kipengele cha muda na pendekezo la majukumu ya CHC kupelekwa kwa Msajili wa Hazina.

Mbunge wa Mwibara Bw. Alphaxard Lugola (CCM) alisema kitendo cha kuweka muda huo ni kutoa mwanya wa maandalizi ya wizi wa mali za
mashirika ya umma ambayo yamekuwa yakitumiwa na wachache kujitajirisha.

“Mimi ni mbunge wa CCM lakini katika hili napingana kabisa, napata fursa ya kuchungulia na kuwahoji walioko kwenye mashirika ndio maana nina uchungu, fedha zinaliwa bila sababu ya msingi...hicho kipengele cha majukumu ya CHC kuwa chini ya Msajili wa hazina ambaye hata ukimuuliza ana mashirika mangapi hajui itakuwa ni kuwafikisha watanzania mahala pabaya,” alisema alisema.

Alisema utaratibu wa kuhamisha madaraka ni njia au mwanya wa wizi na kwamba imefikia wakati maamuzi yanayotolewa na bunge yasipuuzwe na serikali kwa kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki watanzania.

Waziri alilazimika kuondoa kipengele cha majukumu ya CHC kuhamishiwa kwa Msajili wa Hazina na kueleza kuwa muda wa miaka
mitatu itafanya tathmini ya kiutendaji inayofanywa na CHC ili kuona namna nyingine ya kufanya.
 
shukran kwa kutujuza kinachoendelea bungeni...... tunahitaji wabunge kama Mh, Zito bungeni.. hivi vikao vinayoendelea CDM wanaanza kuniteka taratibu sifurahishwi na sisa zao nje ya bunge lakini wakiwa bungeni nafurahishwa na wanayoyafanya ... inaonesha wazi wapo pale kwa ajili ya wananchi ...
 
Miongozo mingi imeisha tolewa kwa mfano. Pinda alisema uongo Lema akaambiwa athibitishe spika akapiga chenga. Tundu lisu vile vile chenga ya nguvu. Mchungaji msigwa dhidi ya pinda chenga kali. Hawa ni chadema bwana si chama cha magamba.
 
nina mashaka na spika kwenye maamuzi kwanini kila siku hoja za wabunge wa upinzani anataka zithibitishwe?????nimekumbuka ile ya lema na mauaji ya arusha, pili ile ya tundu lissu na tatu ile ya mchungaji msigwa nae aliambiwa athibitishe hv huyu mama kweli kwa mtindo huu wa kila kitu thibitisha tutafika kweli?baadae ataambiwa nchi inauzwa atasema thibitisha na akipelekewa vithibitisho hatolei maamuzi kwa mfano ile ishu ya lema na mauaji ya arusha hadi leo hii hatujui aliamua nini huyu spika!
 
Sijajua nini kitatokea! Hawa cdm wakifurukuta mtaani ni KESI! Bungeni ni KUTHIBITISHA. I am watching.
 
Hapa Zitto katoka! Nimeipenda wabunge wakiwa hivi hakuna chama kitaleta upuuzi nchini serikali lazima itakuwa makini. Na ikishakua makini watanzania tutabadilika. Ninawasihi wabunge wote bila kujali chama wasiache kuona mambo muhimu kama haya na wakishayaona waache kabisa kutetea chama kwa kuwa tu ni chama, watetee maslahi ya Taifa!
 
Hapa Zitto katoka! Nimeipenda wabunge wakiwa hivi hakuna chama kitaleta upuuzi nchini serikali lazima itakuwa makini. Na ikishakua makini watanzania tutabadilika. Ninawasihi wabunge wote bila kujali chama wasiache kuona mambo muhimu kama haya na wakishayaona waache kabisa kutetea chama kwa kuwa tu ni chama, watetee maslahi ya taifa!

Mkuu wabunge wa CCM wapo pale kutetea maslahi ya Chama wala sio kutetea maslahi ya wananchi. Wanashindwa kujua kwamba kutoikosoa serikali kwao ndiko kunakipeleka chama kaburini kwani serikali iliyo madarakani ni ya chama hicho hicho. Hawa walipashwa kuwa wakali ili serikali itekeleze kwa ufanisi ilani ya chama chao na hivyo kurudisha imani ya wananchi kwa chama, lakini wanatenda kinyume.

Sikio la kufa halisikii dawa!!!!!

Tiba
 
Kwa bunge hili mh. Lukuvi ambaye ni chief wheap wa ccm ana kazi ya ziada ya kuomba miongozo na anapaswa kuwa makini sana asikurupuke vinginevyo atajikuta anaomba miongozo ambayo mwisho wa siku itaiumbua serikali ya ccm.
 
Wadau chunguzeni Kuna nguvu iliojificha nyuma ya pazia hawa magamba Wanauwa nchi yetu kwa Rushwa.
 
Mara nyingi huyu spika anasema thibitisha wakithibitisha anaficha hiyo taarifa yaani huyu mama kilaza kweli sijui wa nini huyu yeye mwenyewe si aliloby
 
Back
Top Bottom