Zitto aliponda baraza la mawaziri kuhusu CHC

nkosikazi

JF-Expert Member
Mar 11, 2010
361
336
Zitto ameliponda baraza la mawaziri kwa kutaka CHC yaani consolidated holdings kwa kutaka kuongezewa muda wa miaka mitatu badala ya mapendekezo ya kamati yake iliyotaka lipewe unspecified time ili liweze kuangalia interests za nchi na mali zake. Akasema mawaziri wamepitiwa na malobyst ambao wanataka chc libaki kwa muda mfupi ili mafisadi waweze kuua kuila nchi! Ni hotuba kali ambayo imewafanya mawaziri wawili pamoja na Lukuvi waombe mwongozo ili athibitishe kuwa mawaziri wamekula mlungula. Ni hali tete sana bungeni
 
CHC inaangalia mali zipi zilizobaki? Majengo karibu yote ya ilyokuwa NBC ya ukweli yaliuzwa.
 
nilikuwa nasubiri hii thread kwa hamu..bado naendelea kufuatilia hii scene!
 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma na mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe (Chadema) amewasha moto bungeni asubuhi hii.

Zitto ameliponda baraza la mawaziri kuwa wamechakachua ripoti ya kamati yake na hivyo amewataka kuleta ripoti halali ya kamati hiyo. Kwa kweli hali ni tete bungeni. Lukuvi alijaribu kusimama akaambiwa akae chini kwani yeye sio spika. Zitto amedai yeye hafinyangi maneno.

Ngoja tuone. Yaani ni balaa ndani ya ukumbi wa bunge.
 
Sasa kapanda mbunge wa mwibara (ccm) ambaye alikuwa kwenye kamati ya Zitto, naye anaua. Hali ni tete mjengoni sa hizi. Mwaka huu kweli tunashuhudia bunge.
 
Mbubge wa Mwibara

Mh Lugala ameichana chana serikali ya chama chake kwa kutaka kuiibia nchi kwa kuiingiza CHC kwenda TR na kuifanya isiwajibike wakati TR hawajui hata mashirika mangapi yako chini yake na wala hawana cerificte zake. Moto umewaka sana na sasa Hamad Rashid wa CUF anaendelea kurusha madongo kwa serikali.

Baraza la mawaziri limeumbuka na Mkullo anaabgalia chini na koti linampwaya kwa aibu!
 
Mbubge wa MwibaraN Mh Lugala ameichana chana serikali ya chama chake kwa kutaka kuiibia nchi kwa kuiingiza CHC kwenda TR na kuifanya isiwajibike wakati TR hawajui hata mashirika mangapi yako chini yake na wala hawana cerificte zake. Moto umewaka sana na sasa Hamad Rashid wa CUF anaendelea kurusha madongo kwa serikali. Baraza la mawaziri limeumbuka na Mkullo anaabgalia chini na koti linampwaya kwa aibu!
Taarifa yako nzuri, lakini elewa kuwa vifupisho hivyo havieleweki na kila mtu na wala si standard!...right?
 
Mwenye busara Hamad Rashid (CUF) anazungumza kusihi muda wa CHC uwe zaidi. Mbunge wa CCM kamtangulia na kinamna kumuunga mkono Zitto. Inaeelekea kweli suala hili linaguza maslahi ya nchi. Bravo wabunge. huyu Lukuvi elimu ndogo. Yeye anafikiri lobbying ni tusi. Watu wanasomea kuwa Lobbyists hadi PhD level.
 
Mbunge wa mwibara (ccm) kanyea ugali , hana chenga wala nini. Kaongea ukweli mtupu. Shame to magamba kimyaaa. Mkulo koti linambana sasa. Maslahi za taifa kwanza.
 
iasee magamba ni kama nzi, wao kufia kwenye kidonda ni wajibu.
.
 
Kwa kweli mimi sipendi waziri asiye na uzalendo. Nchi hii sasa iko katika nano colonialisation. Yaani wabunge na mawaziri wa CCM hawabehave kama watanzania. Ngoja 2015.
 
Zitto umetumia taaluma yako ya Uchumi vizuri,

Nimeshangaa sana Msajili wa hazina hana Records Muhimu za mashirika anayoyasimamia?

Finance minister nae ame-behave very unprofessionally leo,hii ilikua aibu!
 
Back
Top Bottom