Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Nimekaa nikatafakari. Nikaona ni vyema nililete hili suala hapa ili sote tupate kufahamishana.
Miezi michache baada ya Serikali ya Awamu ya 5 kuingia madaraka na Rais John Magufuli kutangaza Baraza la Mawaziri, Februari 2016 Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe naye alitangaza Baraza lake la Mawaziri vivuli bungeni > Mbowe atangaza Baraza kivuli la Mawaziri, Mbatia ndani. Zitto, Kubenea nje - JamiiForums
Umepita muda mrefu sasa na mambo mengi yametokea kwenye siasa za nchi yetu, hasa kwenye siasa za vyama. Na kwa bahati nzuri au mbaya, imeonekana kwamba viongozi na wanachi kwa ujumla, sote tumekuwa tukienda na upepo. Yaani, tunaenda na matukio kwa kadri yanavyotokea kiasi cha kusahau kuangalia mambo mengine. Hili la Baraza Kivuli likiwemo.
Mathalani, baadhi ya Wizara zilivunjwa na kuunganishwa. Nyingine zilitenganishwa na kadhalika. Vilevile, Wabunge wamehama mostly kutoka Upinzani kwenda Chama Tawala. Hivyo, naamini mambo haya yote ni lazima yatakuwa yameathiri lile Baraza Kivuli ambalo kimsingi ni relfection ya Baraza halisi linaloundwa na Rais wa JMT.
Ukipitia Baraza la Mawaziri vivuli, utagundua mapungufu ya wizara kubaki vile vile (mfano Wizara ya Nishati na Madini, ), Bado Wabunge waliohama vyama wanatajwa kuwa ni viongozi wa wizarani (Mfano Mwita Waitara, Abdallah Mtolea) n.k.
Je, kwanini Upinzani bado hawajafanya maboresho kwenye Baraza la Mawaziri vivuli ili kuendana na athari ya mabadiliko ya kimfumo yaliyofanywa na Serikali katika wizara mbalimbali? Ni sheria/Katiba inawabana au wamesahau!?