Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?

Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,mtu yoyote aliyewahi kufanya kazi na Zitto hata kwa saa 1 atakubali kwamba Zitto ni kijana makini sana.Ni vigumu sana kupata vijana makini wa aina ya Zitto katika kizazi chetu ambacho kimejaa watu wanaopenda starehe tu.

Mwacheni achague kile anachoona kinafaa kwake kama ameona siasa ni mchezo mchafu.Mpaka Zitto kufikia kusema siasa ni second choice kwake hadharani japokuwa ni ukweli kutokana na kauli zake za nyuma ujue ni baada ya kuona rafu nyingi zikifanyika dhidi yake bila justifiable reasons.

Hata kama ukiacha siasa leo Zitto kile ulichokifanya na kukihubiri katika muda mchache uliokuwepo katika siasa za kitaifa kitafanya jina lako lisipotee katika historia ya nchi hii.

Naamini pia kama utaamua kujikita kwenye taaluma bado utatoa mchango mkubwa kwa maendeleo na ustawi wa nchi yako.Kwani kutoa mchango kwenye maendeleo ya nchi si lazima uwe mwanasiasa.

Kila mtu katika nafasi yake ana mchango katika maendeleo ya taifa hili na sidhani kama Zitto ndiyo lazima awe mwanasiasa. Hata mtoa mada hii "Remmy" waweza kuwa mwanasiasa pia.
 
changamoto tulizokuwa nazo kwenye siasa za TZ

1. tume huru ya uchaguzi
2. elimu ya uchaguzi kwa wapiga kura
3. wanasiasa waaminifu na wanaotaka mabadiliko ya kweli na sio kuadvance matumbo yao na kuwaacha wananchi katikati
4. funding kwa vyama vya siasa
5.
6. n.k
haya maneno ya zito ni mojawapo ya changamoto tulizokuwa nazo tanzania katika political system yetu

mnamkumbuka dr masumbuko lamwai
 
Nimemuona zito akihojiwa TBC 1 leo asubuhi na kwa kweli sasa naamini yaliyotangulia kuelezwa,si mkweli!!
Anadai siasa sio chaguo lake la kwanza lakini anataka uenyekiti wa chama,for what?
Anapinga maamuzi ya vikao halali vya vyama hadharani wakati yeye ni kiongozi,anapotumia maneno "sikubaliani na maamuzi".
Zito ameshakuwa big headed and I believe he is going heading for a fall.
Wananchi hasa wapenda mabadiliko wanasononeka sana na kauli za Zito na masononeko yao ndio itakuwa laana kwa Zito

Kuna uwezekano mkubwa akaondoka CHADEMA na kubaki kwenye siasa. Na kama akiamua kubaki kwenye siasa uwezekano mkubwa ataingia CCM maana kuna baadhi ndani ya CHADEMA wanadai ni mamluki wa CCM.

Hivyo itakuwa vizuri kama CHADEMA wakimfukuza kabla ya kuamua yeye kujiuzulu ili hata akiamua kujiunga CCM basi kujiunga kwake kusiwe na uzito mkubwa maana ataonekana anatapatapa ili kuganga njaa.
 
haya kadri siku zinavyokwenda ndio rangi halisi za Zito Kabwe zinazidi kujionyesha, haya Zito acha aibu fika Kinondoni leta barua ujiuzulu maana umeisha pata mkate wako huna sababu ya kubakia kwenye siasa.

Kweli pesa mwanaharamu, sikutarajia kama Zitto ninayemfahamu angefikia huko!!!!!!!!!!!!!!! Who is serious politician then!!?????? help me please!
 
Kuna uwezekano mkubwa akaondoka CHADEMA na kubaki kwenye siasa. Na kama akiamua kubaki kwenye siasa uwezekano mkubwa ataingia CCM maana kuna baadhi ndani ya CHADEMA wanadai ni mamluki wa CCM.

Hivyo itakuwa vizuri kama CHADEMA wakimfukuza kabla ya kuamua yeye kujiuzulu ili hata akiamua kujiunga CCM basi kujiunga kwake kusiwe na uzito mkubwa maana ataonekana anatapatapa ili kuganga njaa.
Uzito wa nini? Hawafukuzwi watu eti kukwepa uzito,adhabu hiyo itolewe kwa uhalali na kwa makosa yanayostahili.
Mbona Kaburu aliondoka na hakuna Uzito wowote?
 
Kuna uwezekano mkubwa akaondoka CHADEMA na kubaki kwenye siasa. Na kama akiamua kubaki kwenye siasa uwezekano mkubwa ataingia CCM maana kuna baadhi ndani ya CHADEMA wanadai ni mamluki wa CCM.

Hivyo itakuwa vizuri kama CHADEMA wakimfukuza kabla ya kuamua yeye kujiuzulu ili hata akiamua kujiunga CCM basi kujiunga kwake kusiwe na uzito mkubwa maana ataonekana anatapatapa ili kuganga njaa.

mawazo mgando haya. mmezoea wanasiasa wa upinzani wakikosana na wenzao kuhama vyama vyao. Zitto keshasema hahami. Ninyi mnaomsukuma ahame mtaula wa chuya.

Zitto hana njaa na wala hatapata njaa akiacha siasa maana siasa kwake sio ajira. Amekuwa akifanya kazi za taaluma yake hata ndani ya ubunge. Acheni kuhukumu
 
Kweli pesa mwanaharamu, sikutarajia kama Zitto ninayemfahamu angefikia huko!!!!!!!!!!!!!!! Who is serious politician then!!?????? help me please!

kalipwa shilingi ngapi maana unasema kana kwamba wewe ndio unamshikia hizo pesa. Chuki zimewajaa
 
Yeye kashapoteza trust kwa watanzania na kwa chama chake, kwa hiyo hafai hata kuwa mwakilishi wa jimbo.

trust ya jimbo lake wanajua wanajimbo na sio wewe unaeshinda kwenye pc na hata kura hupigi. ukitaka kujua anakubalika vipi jimboni kwake angalia matokeo ya serikali za vijiji huko halafu pima na matokeo ya vijiji vya majimbo ya wenzake ndani ya hichoc hicho chama chao.
 
Lakini hamumpi kijana a breathing space; its none stop Zitto Zitto Zitto kibaya zaidi mazuri na mabaya inabidi aji defend mwenyewe.

Chama chake akimsaidii na watanzania wanataka majibu; tofauti na viongozi wengine wenye watu chungu mtele wa kuwasaidia kujibu saa zingine.

Hii ni more than too much to swallow for a young MP give the dude a chance na Chama chake inabidi kijifunze kumtetea au kimpe altimutum ya political career either aondoke au kubali desturi yao. Uchaguzi auko mbali na huu si muda wa kulambana kwenye public ni damage kwa chama.

Kama anabaki kama anavyosema awe na timu kama wengine so far anaonekana yupo kwenye lost path career wise ana ajui aelekee wapi.

yeye huyo kijana amekuwa mbele sana kutetea wenzake na kulinda chama. unakumbuka wkaati wa chacha wangwe alipokufa, wote waliingia mitini akabaki yeye kulinda chama kuanzia mazishi mpaka kwa waandishi. wenyewe kazi yao kumchimba tu. wanasema hafayi kazi kama timu kwa uongo wao na chuki zao. huyu kijana ni team builder siku zote. kwa wao timu ni kuwatetea na sio wao kumlinda mwenzao. Zitto ni wa kusambuliwa tu ndani ya chadema. wenzake wana kisebusebu
 
Zitto anapenda siasa ila kajichanganya mwenyewe!

Kilicho mponza ni Kupenda Siasa za kuzungumza na kufikiri baadaye!

Waulize wanaomjua tangu DARUSO!

Ugonjwa uliompata Zitto unaitwa "POLITICAL WITHERING" for unstrategic Politician !
 
1. Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,mtu yoyote aliyewahi kufanya kazi na Zitto hata kwa saa 1 atakubali kwamba Zitto ni kijana makini sana.

2. Ni vigumu sana kupata vijana makini wa aina ya Zitto katika kizazi chetu ambacho kimejaa watu wanaopenda starehe tu.

Mwacheni achague kile anachoona kinafaa kwake kama ameona siasa ni mchezo mchafu.Mpaka Zitto kufikia kusema siasa ni second choice kwake hadharani japokuwa ni ukweli kutokana na kauli zake za nyuma ujue ni
3. baada ya kuona rafu nyingi zikifanyika dhidi yake bila justifiable reasons.

Hata kama ukiacha siasa leo Zitto kile ulichokifanya na kukihubiri katika muda mchache uliokuwepo katika siasa za kitaifa kitafanya jina lako lisipotee katika historia ya nchi hii.

Naamini pia kama utaamua kujikita kwenye taaluma bado utatoa mchango mkubwa kwa maendeleo na ustawi wa nchi yako.Kwani kutoa mchango kwenye maendeleo ya nchi si lazima uwe mwanasiasa.

Kila mtu katika nafasi yake ana mchango katika maendeleo ya taifa hili na sidhani kama Zitto ndiyo lazima awe mwanasiasa. Hata mtoa mada hii "Remmy" waweza kuwa mwanasiasa pia.

- Incredible hivi kuna Zitto wangapi katika siasa ya Tanzania? Huyu ni Zitto mbunge wa Kigoma au mwingine, I am lost eti!

Respect.

FMEs!
 
yeye huyo kijana amekuwa mbele sana kutetea wenzake na kulinda chama. unakumbuka wkaati wa chacha wangwe alipokufa, wote waliingia mitini akabaki yeye kulinda chama kuanzia mazishi mpaka kwa waandishi. wenyewe kazi yao kumchimba tu. wanasema hafayi kazi kama timu kwa uongo wao na chuki zao. huyu kijana ni team builder siku zote. kwa wao timu ni kuwatetea na sio wao kumlinda mwenzao. Zitto ni wa kusambuliwa tu ndani ya chadema. wenzake wana kisebusebu

Sasa kuna faida gani ya kukaa mpweke ndani ya chama nani rafiki zake huko chamani kama hata anao.

Je chama chake kinaridhika na conducts zake in and out of the party buildings. Hana fuata makubaliano ya wengi ya ndani ya chama au anapingana na mengi.

Mwisho wa siku he has to make firm decisions; what makes him happy na kama ni politics through chama chake amalize hiyo migogoro for good; a party works as a team and not as individual success. Hivyo is either with Chadema or without it lakini mifarakano aisaidii at 2010.

Particualry lugha zake anazotumia kuashiria kuna mgogoro within. Kwa upande wangu those are internal discipline matters rather than public entertainment.
 
Zitto anapenda siasa ila kajichanganya mwenyewe! Kilicho mponza ni Kupenda Siasa za kuzungumza na kufikiri baadaye!

Kama walivyosema wahenga - majuto mjukuu, anayejuta siku zote ametenda. Kujuta ni dalili ya kukubali kuchemsha, laiti angejua asingetenda. Mwanasiasa makini, hujirudi haraka anapoboronga na ama hukaa kimya au huomba msamaha - mwanasiasa limbukeni ama huzira anapobanwa au hujaribu kukomaa na upinzani lakini maji yanapofika shingoni hutafuta upenyo wa kuondokea.
 
This is not a breaking news,it has been said by himself in public since year 2007 that his first choice is to become a lecturer.

Tatizo ni kwamba wote mmekuwa polarised kwenye siasa kana kwamba kuna nchi duniani iliendelea kwa siasa tu matokeo yake mnaenda kuufukia utaalamu kwenye shughuli ya siasa ambayo hata mnenguaji wa TOT anaiweza.

Msifikiri wanasiasa watajifunga kengele kama paka atakayefungwa na panya. Kuweni watalamu kwenye fani zenu mtawashinda.

Watalamu wa mitandao wamejaribu na tunaona mtikisiko. JF, emails ni matokeo ya fani hizo mmeona zilivyoibua ufisadi. Hivi tunavyojadili hizi thread zote wanasiasa wanazipitia.

Mitandao imeweza tumieni proffession zingine mtawaondoa. Lakini mkijirundika kwenye siasa eti kwa sababu huko ndiko kuna vijisenti vya kujenga nyumba Mbezi basi hapo ndipo itakuwa doomsday yenu.

Mnaenda kwenye siasa kutafuta mitaji, si mkakope bank kama kweli mmeshakuwa wafanyabiashara wabobevu. Mbona mnaogopa na hata biashara zenu hazidumu miaka mitano mkiporomoka kwenye siasa.
 
Huyu Zitto kwisha habari yake. Toka alipoleta ule wazimu wa dowans humu ndani na kujifamnya ana msimamo binafsi ambao hayumbishwi, wengine tuliondoa kabisa mategemeo kwake.

Zitto alikuwa atusaidie sana watanzania, lakini sijui ni kwamba he became big headed au ni immaturity ya siasa, lakini mweleka aliopiga ni mkubwa sana.

Yaani wewe mwanasiasa unataka kujifanya at the same time una misimamo binafsi ambayo inapingana kwa asilimia kubwa na electorate, wapi huu wazimu umeshafanywa dunia hii??

All the best Zitto
 
roho mbaya zitawauwa. Zitto Kabwe hawezi kuhukumiwa kwa tukio moja tu la dowans kama mnavyotaka na ndio maana poll szilizofanyika september zilionyesha akiwa mbunge anayekubalika zaidi akiwa amewazunguka wenzake mara tatu zaidi.
Zitto alionyesha alivyo tayari kuchuku maamuzi magumu hata kama yanaathiri umaarufu wake na Watanzania tulimwelewa maana alijieleza vya kutosha. Mliobaki mmejaa chuki tu na vijiba vya roho. Utapiga mweleka wewe, Zitto yupo imara. Ni bora kumjua kiongozi kwa makosa yake anayofanya kuliko kiongozi anayejificha kwenye ya ufisadi alihali yeye fisadi mkubwa sana.
 
Mimi namheshimu sana Zitto kuwa ni mbunge aliyechaguliwa na wananchi, sijamuona kwa macho na sielewi alichowaahidi wapiga kura wake hadi wakamchagua.

Nimeanza kumsikia Zitto hasa wakati aliposimamishwa bungeni kwenye mjadala wa Richmond na halafu Dowans na baadaye pale alipoonywa bungeni aliposema waziri analeta majibu ya hovyo hovyo na juzi alipotaka kugombea uenyekiti na Mbowe basi. Kwa hiyo mawazo yangu yanajikita kwenye hako ka-research kangu kadogo.

Zitto bado ni mchanga sana kisiasa akilinganishwa na viongozi wengine ndani ya Chadema. Unapokuwa mwanasiasa unaangaliwa na wengi wenye uwezo,akili, busara, maarifa na uzoefu mbalimbali wengine hata kukuzidi. Unatakiwa kujishusha mbele yao ili wao wakukweze, unapojikweza mwenyewe unaboa hata waliokutumaini wanakuchoka. Zitto anatabia ya kujikuza kuji-proud, nataka niwe Rais niwe lecturer nk hii haitakiwi siasani.

Kwa walio naye karibu sijui kama anashaurika hana collective responsibility, hata kama wewe unaona mawazo yako ni bora jaribu kuhesabu ni wangapi wanaya-support ukibaki peke yako kubali yaishe ungana nao.

Zitto anaposema anasimamia anachokijua sawa, angekuwa mwanasayansi akisimamia utafiti wake na akafanya experiment tukahakikisha tutamwelewa lakini siyo siasa. Kwenye siasa ukisimamia utafiti wako utajikuta umetupwa nje ya ulingo. Siasa haina majaribio naona alikuwa anajaribu siasa karibu itamtoa KO.

Nasema Zitto bado mchanga kisiasa kwasababu, anaposema yeye atampigia kampeni Kafulila wakati yeye yumo Chadema kivipi yaani, akipangiwa kampeni tarehe moja na chama chake atafanyaje. Kifupi mimi naona lengo lake ni kuwavuluga wenzake, ni bora aondoke mapema kabla hajapoteza ladha maana kwenye siasa kuna ladha bwana ukiipoteza kuirudisha kazi kweli kweli amuulize Sumaye, Mrema, Mtikila nk.

Mimi niliona lengo la Zitto kusema atampigia kampeni mpinzani yeyote hata si wa chama chake ni kupima upepo aone kama atapendwa na wengi kwa kutoa wazo hilo wapinzani wote wamuone yeyendiye mwenye uchungu zaidi ya wengine hasa ndani ya Chadema baadaye wamwambie anafaa kuwa m/kiti wa chama.Hapa alikuwa anafanya majaribio na matokeo yake sasa anasema siasa si chaguo lake la kwanza, watu wameanza kumpuuza badala ya kumpongeza, kaona heshima inapungua.

Kwanza anaposema yeye atampigia kampeni mtu yeyote amejilinganisha na nani Nyerere? amejiona yeye si wa jimbo hata asipopiga kampeni jimboni kwake atashinda tu asifanye mchezo na kampeni, Nyerere ndiyo anayaweza hayo alimpigia kampeni Mkapa aliyekuwa hajulikani lakini si Zitto huyu wa juzi anahitaji muda kama miaka 10 mbele ndipo ajipime uzito.

Afterall mimi naona hata kama akiondoka Chadema ipo imara katika utendaji na uongozi hawana lelemama ikilinganishwa na vyama vingine. Matunda hupimwa na watu wa nje, mimi siko karibu na Chadema kuwa najua yaliyo ndani lakini naona matendo yake kwa kuwa malengo ya chama chochote cha upinzani kiujumla yanajulikana.

Kwa swala la Zitto kutumiwa mimi sioni kama anatumiwa haya yote yanatokana na yeye kutokuwa makini na kutojua anatakiwa afanye nini katika siasa, uchanga wa siasa.
 
uNATAKA UMCHAMBUE MARA NGAPI?

Ameongea sahihi na hayuko pekee

Tunachokosa Tanzania au kushangaa ni mtu kusema yaliyo moyoni mwake! ijsmauona mwanasiasa yoyote ambaye first choice ni siasa, ndio maana akina Mwandosya chuo kikuu UDSM wanajulikana wako likizo! bado yuko kwenye prospectus!

mtu ambaye Siasa lilikuwa chaguo la kwanza ni JK! alipomaliza tu chuo kikuu alienda kugawa kadi za TANU!

Yeye kashapoteza trust kwa watanzania na kwa chama chake, kwa hiyo hafai hata kuwa mwakilishi wa jimbo.

Watanzania wangapi, wana JF, jimboni mwake au wote in general? popularity ya Zito bado kubwa sana ndugu, labda unajipa moyo na ku-curse kutokana na chuki zako

changamoto tulizokuwa nazo kwenye siasa za TZ

1. tume huru ya uchaguzi
2. elimu ya uchaguzi kwa wapiga kura
3. wanasiasa waaminifu na wanaotaka mabadiliko ya kweli na sio kuadvance matumbo yao na kuwaacha wananchi katikati
4. funding kwa vyama vya siasa
5.
6. n.k
haya maneno ya zito ni mojawapo ya changamoto tulizokuwa nazo tanzania katika political system yetu

mnamkumbuka dr masumbuko lamwai

well said my friend, and if we will not think about these challenge then issues of changes and revolution is another day dream

Kweli pesa mwanaharamu, sikutarajia kama Zitto ninayemfahamu angefikia huko!!!!!!!!!!!!!!! Who is serious politician then!!?????? help me please!

No one, you need to go there my friend, if you can't then learn to trust leaders!

Huyu Zitto kwisha habari yake. Toka alipoleta ule wazimu wa dowans humu ndani na kujifamnya ana msimamo binafsi ambao hayumbishwi, wengine tuliondoa kabisa mategemeo kwake.

Zitto alikuwa atusaidie sana watanzania, lakini sijui ni kwamba he became big headed au ni immaturity ya siasa, lakini mweleka aliopiga ni mkubwa sana.

Yaani wewe mwanasiasa unataka kujifanya at the same time una misimamo binafsi ambayo inapingana kwa asilimia kubwa na electorate, wapi huu wazimu umeshafanywa dunia hii??

All the best Zitto

Hujatoa sababu za hisia zako, ila naweza kutoa hisia zangu kuwa watu kama wa aina yako ndiyo wanaowakimbiza hawa wanasiasa!

Semilong kasema, hapo juu Lwamwai, tulikuwa na akina Mrema, leo Zitto...

do you think these people have problems?? hatujajifunza kutoa gharama za mapinduzi.Nani alishuhudia Lwamwai anatembea nusu uchi alivyoporwa vyeti vyake na CCM? nani alimkumbuka?, very same people they pointed fingers na kusema 'AMELOST'

miaka 15 baada ya mrema, hakuna mwanasiasa yeyote aliyepata kura nyingi za upinzani baada ya Mrema, leo hii Mrema ni zezeta, anadharauliwa na kila mtu! 'amelost'

Kwa siasa za Tanzania namuunga Mkono Zito akae pembeni, I once asked Kitila is it viable having political parties? Leo akikaa na njaa waliombeba jangwani watamkumbuka?? watasema 'amelost'

Watanzania hatujawa tayari bado, na kwa namna hii acha CCM watusulubu mpaka akili zitakapokuja kichwani, zikija kichwani, tutataka kiongozi , na atakayekuja HATAKUWA MALAIKA!! tukitaka awe malaika tutaishia kusema 'AMELOST'

au unafikiri atakayekuja atakuwaje?? taavaa magunia, hatazungumza mawazo yake, atakuwa wa ndiyo mzee ya wananchi! akishakuwa hivyo basi atakuwa amelost kabla ya kulostishwa na anaowaongoza!

Kama ubongo wetu bado haujatanuka kukubali kuwa aliye kinyume chetu si adui yetu tutaamka karne tatu zijazo! ndio kizazi kinachokosa fikra mbadala na challenge halisi kwa sababu ya kushinda madrasa na kubatizwa utotoni! tumedumazwa jamani tukubali tukatae!

Root ya tatizo la Zitto linajulikana, na hakuna mtanzania aliyekaa kuwaza hilo, kila siku anapiga kelele pengine kuna watakaomsikia, Roho yake haitatulia mpaka justice itendeke au aondoke, hili lilijulikana tangu awali! hili linajulikana wazi

Leo hii siwezi nikawapa chadema nchi wakichukua kesho vyama vingine havitapiga kura! hilo tusipoliona na kupiga kelele , tumedumaa

Operation Sangara inaendelea lakini pamoja na kuendelea we need justice! they abused democracy, very same party you all want to be a ruling party what joke is this! Kenya haijatufundisha bado??
 
Yeye mwenyewe Zitto alituambia aliingia Chadema akiwa na miaka 16 hawezi kutoka Chadema kwa sababu familia yote ni Chadema hii ni sababu ya kitoto kabisa ina maana yeye angetoka ila anaona aibu tu? kweli huyu si mwanasiasa nimeanza kuamini ni Celebrity wa saisa anapoona watu wana mfuatafuata ndiyo furaha yake is not a real fighter.

Kama siasa si chaguo la kwanza ina maana chaguo la kwanza alichagua akiwa na umri gani, we should be very careful with this guy. Sasa alikuwa anagombea uenyekiti wa nini kama si kuvuruga wenzake. Mimi nilikuwa muumini mkubwa tu wa Zitto basi aondoke salama. Kama msemaji mmoja alivyosema hapo juu Chadema wakauke kama hawamuoni wasije wakalogwa kumfukuza ajiondoe mwenyewe ila waanze pole pole kutomshirikisha kwenye mambo nyeti ya chama.

Najua Chadema bado wanamhitaji lakini huwezi kumlazimisha ng'ombe kunywa maji.

hee jamani tuwe makini na maneno yetu.. ulikuwa muumini mkubwa wa Zitto? muumini?Mbona unajishusha sana?
 
Afterall mimi naona hata kama akiondoka Chadema ipo imara katika utendaji na uongozi hawana lelemama ikilinganishwa na vyama vingine. Matunda hupimwa na watu wa nje, mimi siko karibu na Chadema kuwa najua yaliyo ndani lakini naona matendo yake kwa kuwa malengo ya chama chochote cha upinzani kiujumla yanajulikana.

Kwa swala la Zitto kutumiwa mimi sioni kama anatumiwa haya yote yanatokana na yeye kutokuwa makini na kutojua anatakiwa afanye nini katika siasa, uchanga wa siasa.

well said,

Ila tunachokosa kuangalia ni, je chanzo cha matatizo ya Zito ni nini?

Pili je kiondoka athari zake ni zipi?

Mkuu, labda haujajua trend ya wapiga kura wa nchi hii, tangu mwaka 95 kila uchaguzi uliofuata wapinzani wamekuwa wanapata kura pungufu, mpaka uliopita JK kakomba asilimia 80%!!

Tatizo ni kuwa watu hawapigi kura! na kutopiga kura kwa watu ni kutokana na matatizo haya ya ndani ya hivi vyama, watu wanaona is wastage of time

Sasa ili hiyo chadema yako imara unayoisifia iwe imara, lazima watu wapige kura ili kuonyesha hivyo.Haiwezekani chama kinapata silimia 2% ya kura ukasema kina matarajio ya kushika nchi! only crazy can think that!

Zito ana matatizo yake, lakini tukiangalia mzizi wa hili tatizo ni chadema kama chama! na kwa namna hii tutapata akina zito wengi miaka yote inayokuja, hatutapata wapiga kura,kwani watu anavidharau hivi vyama.

Yet kama mtu unayetaka change unasema akiondoka Chadema ni imara??,

hatuangalii chadema hapa, wengine, tunataka mabadiliko na revolution ya kitaifa, ifike muda wananchi waseme wachague vyama mbadala vya kuiondoa ccm madarakani?? sasa kama wanagombana namna hii, tatizo ni nini.?

By the way, Chadema kinavyo handdle issue ya zito kinaonyesha ni dhaifu.Kingekuwa na nguvu kimfukuze basi, wanaogopa nini? au wanasubiri nini??AIDHA

Muonekano na tuhuma zako ni wa uongo!

au Tuhuma za Zito juu ya chama chake ni kweli!

IS IT TRUE KUWA CHADEMA KWELI ILIMPA NAIBU MKUU wa chama mtu ambaye ni immature?? if so nani wa kulaumiwa??....................then all chadema is Immature!!!

Mbowe hana nguvu kutoa maamuzi, kwani mpaka sasa hivi hajui nani yuko upende wake au upande wa Zito, NDIYO-usibishe, si hakupigiwa kura?? usipopigiwa kura una hakika gani watu wanakupenda??Slaa ameshindwa kuongea na naibu wake waongee wayamalize!!! same Slaa mnataka awe waziri mkuu wa kuwapatanisha watusi na wahutu, what a joke is this??

Very same Mbowe ndiyo mnataka achukue viatu vya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, acheni utani!

Zito anatoa picha ya upinzani na wapinzani na hii ni nzuri kwa analysis, wakati unamungalia Zito,wengine wanaangalia reaction ya hao wakubwa wake, halafu tunapiga picha je wanaweza? tukiwapa nchi??

Vitu vingine kwa nini tusimshukuru Mungu tu? tujue hatuna vyama tuanze upya, au tubuni mbinu ya kuindoa CCM madarakani nje ya ballot box!

Zito, zito, zito, zito siyo compass yetu watanzania! we need to think higher than this,leave him alone....after all I adore him to tell us all what is happening inside of this so called political party, the very same chama wameshaondoka watu watatu wakubwa, hatujui wale wenzangu na mie wasiojua magazeti na waandishi wa habari, the very same party Marehemu wangwe kalalamika hayohayo!

Tuwe wakweli jamani nchi ya wote hii, kila mtu apewe haki yake! kuwa mkweli ndani ya chama sio usaliti, na kama hawakusikii piga kelele usikike kilio chako zito kimesikika! mkisema hivyo-mkimnyamazisha basi kesho chadema nayo itakuwa na akina Sheikh Yahaya kumi, watakaosema ukiuliza swali unakatika ulimi!
 
Back
Top Bottom