Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
KWENYE SIASA HAKUNA KUWA KATIKATI"NEUTRAL" MTAWALA LAZIMA AAMUE KUSUKA AU KUNYOA. VINGINEVYO ANGUKO NI HAKIKA.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Siasa inakanuni zake, na moja ya kanuni hizo ni pamoja na hii ya kuchagua upande. Ni aidha uwe moto au uwe baridi Full stop. Maswala ya kusema au kuonyesha matendo ya kuwa Neutral ni kujitoa kwenye mfumo wa utawala bila ya wewe mwenyewe kujua. Na hakika ni kuwa utaanguka kwa kishindo kikuu.
Siasa ndio jambo gumu kuliko yote duniani. Ni rahisi kurusha Rocket, kuunda teknolojia za hali ya juu, kuwa Daktari lakini siasa ni ngumu kuliko mambo yote hayo.
Baada ya siasa jambo gumu linalofuatia ni Mapenzi.
Ugumu wa siasa unatokana na kuongoza kiumbe ambacho kina utashi, hujui kinawaza nini, na mbaya zaidi kiumbe kinachobadilika badilika. Kuongoza wanadamu ndio kazi ngumu zaidi kuliko jambo lolote lile.
Leo atasema hivi kesho atasema vile. Leo atakuwa pamoja na wewe kwa kukuunga mkono kesho atakutana.
Zaidi hujui chochote anachokifanya binadamu ni kweli au anaigiza.
Sifa hizo ndizo zilichangia na zinachangia kwa kiasi kikubwa baadhi ya Watawala kutumia mfumo wa kimabavu (udikteta) ili kuendelea kutawala
Ukishapewa Nchi kaa ukijua utakutana na makundi makubwa mawili. Moja,lililokuwa linanufaika na utawala uliopita ambao umeuchukua wewe,na kundi la pili ni lile ambalo halikuwa linanufaika na sasa linakuona wewe ndio mwanzo wa matumaini yao.
Ni kosa la kiufundi kutaka haya makundi yakae pamoja. Haiwezekaniki Makundi hayo kukaa pamoja.
Ni kosa la kiufundi, kutotaka kujihusisha na kundi lolote yaani wewe kuwa Neutral.
Hapo utapigwa mapema zaidi.
Ni lazima uchague upande.
Ni kosa la kiufundi, kutumia wahusika mashuhuri kutoka kwa moja ya makundi yaliyohasimiana.
Kikawaida unatakiwa kama ipo haja ya kufanya hivyo, chukua wahusika waliopoa ambao hawana impact yoyote Kwa siasa zako.
Ni rahisi makundi mawili yaliyohasimiana kushirikiana kukuangusha ikiwa utakuwa Neutral. Mbinu pekee iliyopo ni kujiunga na kundi mojawapo kisha uendelee na utawala wako.
Mbinu ya kufuta makundi hayo mawili inaweza kukupotezea muda na mara nyingi utawaunganisha na watakushinda.
Ungana na mmoja, kisha mtumie kumpiga mwingine. Kisha ukishamalizana na uliyempiga. Kazi inakuwa rahisi. Mmalize hiyo aliyevalia.
Nawatakia majukumu Mema.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam