Waislam tumedanganywa kwa miaka mingi sana. Tuamke, tufanye siasa misikitini na popote pale

Status
Not open for further replies.

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
Waislam kwa miaka mingi sana tumejazwa ujinga kwa makusudi kabisa kuaminishwa kuwa ni mwiko kuchanganya siasa na dini.

Huo ni uongo na tumekuwa tukijazwa ujinga "brainwashed" kuamini hilo.

Uislam haujatukataza popote kufanya siasa. Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya binadam. Tusidanganywe tena na tukaendelea kudanyika kuwa siasa haziendani na Uislam.

Mtu akikwambia "siasa haina dini" elewa kuwa huyo anakutowa kwenye Uislam wako. Usikubali hata kidogo, ni yeye hana dini anataka akutowe na wewe kwenye Uislam wako.

Kwa makusudi kabisa mefikia hatua mpaka maneno yanabadilishwa "systematically ""udini" nq sisi tunachekeleantu.

Elewa maana ya maneno haya:

Udini = Uislam. Mdini = Muislam.
Wadini = Waislam.
imswahili = Muislam.
Waswahili = Waislam.
Uswahili = Uislam.
Mwarabu = Muislam.
Waarabu = Waislam.

Hayo ni kwa uchache tu, mtaongezea na mengine. Huo ni upotoshwaji wa makusudi na unaoratibiwa siyo wa bahati mbaya.

Waielwmntuamke na tufanye siasa popote. Madheikhnwetu.muwe.msyarinwa.mbele kuhamadishansiasankama wslivyofanya Masheikh wetu wakati wa kudai uhuru.

Uislam ni siasa, siasa ni Uislam.

Someni haya yalindikwa zamani hapa hapa Tanzania:

Mtazamo wa Uislamu kuhusu siasa


WENGI wetu tumekuwa tukisikia viongozi, wasomi na watu mbalimbali wakizungumzia masuala ya dini na siasa. Ujumbe mkuu siku zote umekuwa kuvitenganisha viwili hivyo yaani visichanganywe. Katika sehemu mbalimbali duniani, kama ilivyo kwa masuala mengine yahusuyo maisha ya kila siku, Waislamu wamekuwa ama wakiaswa kutochanganya dini na siasa au wakilaumiwa kwa kuvichanganya viwili hivi. Chanzo cha nasaha na lawama hizo ni mtazamo Kimagharibi au Usekula ambao unadai kutenganisha dini na siasa (separation of the Church from politics). Wasekula wanadai kuwa viwili hivyo vikichanganywa basi vurugu itatawala katika jamii husika. Hata hivyo, jamii nyingi za huko Magharibi zinaendeshwa kwa taratibu za kinaswara (Kikristo) lakini bado zinadai kuwa zenyewe ni za Kisekula. Wasiwasi wao umekuwa kwa Uislamu ambao siku zote wanaona kama dini isiyojali au isiyofuata haki za binadamu. Mwandishi Mama Nasir anaelezea zaidi.

Nini Uislamu na siasa ni nini?


Uislamu ni dini au mfumo wa maisha ambao Allah (s.w.) amewaletea waja wake kupitia kwa Mitume wake. Sisi tuliopo sasa Uislamu umetufika kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w.). Uislamu ni mfumo uliokamili, unaongoza kila kipengele kinachohusu maisha ya mwanadamu. Wanaoamua kuukubali au kuufuata Uislamu basi wanaamrishwa na Allah (s.w.) kufanya hivyo kwa ukamilifu na kama inavyopasa kuwa.

Allah (s.w.) anasema: "Enyi mlioamini! Ingieni kwa ukamilifu katika Uislamu. (Ingieni katika hukumu za Uislamu zote), wala msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri". (2:208).

Allah (s.w.) akasisitiza kwa waumini: "Enyi mlioamini! Mcheni Allah kama ipasavyo kumcha, wala msife isipokuwa mmekwisha kuwa Waislamu kamili". (3:102)

Kutokana na aya hizi ni wazi kuwa Muislamu anawajibika kutekeleza masuala yote ya maisha yake kama ilivyoelekezwa na Uislamu (Qur'an na Sunnah).

Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (TUKI) imetafsiri neno "siasa" katika kamusi ya Kiswahili Sanifu kama ifuatavyo:

"Mfumo wa mawazo yaongozayo utawala wa serikali ya nchi.

"Itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi wake, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii".

Uislamu na siasa

Pamoja na kwamba maadui wa Waislamu na dini yao wanatulazimisha kuvitenganisha viwili hivi, lakini kufuatana na maelezo ya hapo juu ni wazi kuwa Muislamu anayeamini na kuufuata Uislamu hawezi kuitoa siasa kwenye dini. Hii ni kwa sababu Uislamu kama unavyoelezwa kwenye Qur'an na Sunnah unagusa nyanja zote zinazohusu maisha ya mwanadamu ikiwemo siasa, na lengo lake kuu ni kusimamisha utawala wa Allah (s.w.) hapa duniani. Kwa hiyo ili lengo hili litimie ni lazima maagizo yote yafuatwe kwa ukamilifu na siyo kipande kipande kwa kutenganisha mambo mbalimbali yahusuyo maisha ya mwanadamu.

Katika Uislamu, dini na siasa ni viwili viwili vilivyopangana (vilivyoingiliana) na kwa hiyo ni kitu kimoja. Uislamu ni njia kamili ya maisha na siasa ni sehemu ya maisha hayo. Kama Uislamu ulivyofundisha swala, swaumu, zakah, hija na mengineyo, umefundisha pia jinsi ya kuendesha dola (State) na kuunda serikali (government)u, kuchagua viongozi na wawakilishi wetu, kuweka mikataba, kuendesha biashara na shughuli nyingine mbalimbali.

Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu na kuwa lengo la mfumo huo ni kusimamisha ufalme wa Allah (s.w.) hapa duniani.

Mfumo wa siasa wa Kiislamu unasimama katika misingi ifuatayo:

Utukufu/ukuu (sovereignity) wa Allah (s.w.). Uislamu unafundisha kuwa chanzo cha nguvu zote na sheria zote ni Allah (s.w.). Hii imedhihirishwa katika sura na aya mbalimbali za Qur'an kama vile 25:2 na 67:1. Ni Mwenyezi Mungu ndiye anayejua kipi kizuri na kipi kibaya kwa viumbe vyake. Na Yeye ndiye mwamuzi wa mwisho.

Kazi ya dola yoyote hewa ni kusimamia utekelezaji wa sheria, kwa hiyo ni dola iweze kusimamia sheria ya Allah (s.w.) ni lazima nayo itoke huko huko kwa Allah (s.w.). Sheria zilizomo kwenye Qur'an (za kukata wezi mikono, kuchapa viboko/kupiga mawe wazinifu na kadhalika) ni amri za Allah na hivyo haziwezi kubadilishwa na mamlaka yoyote ya kibinadamu hata Umoja wa Mataifa badala yake inatakiwa zitekelezwe na waja wote. Kwa Waislamu kutekeleleza amri/sheria hizo kwa vitendo ndio kukamilisha Uislamu wetu. Kunapotokea mifumo ya siasa ambayo haitekelezi au haisimamishi amri za Allah (s.w.) ni wazi kuwa Uislamu unapata kasoro, na hapo ndipo ulazima wa kuwa na dola ya Kiislamu unapokuja.

Ukhalifa wa binadamu: Mwenyezi Mungu anasema wazi katika Qur'an kuwa mwanadamu ni khalifa (mwakilishi) wake hapa duniani. Kwa mantiki hii mwanadamu analazimika fanye alivyoamrishwa na Allah. Hata hivyo, mwanadamu amepewa uhuru wa kufuata au kuzikana amri za Allah (s.w.) na ndio maana kuna wanaadamu wengi ambao wametokea kuwa wasaliti wa Allah (s.w.). Badala ya kutekeleza alivyoamrishwa ili kuleta amani na utulivu duniani wameamua kumuasi Allah (s.w.) na kusababisha machafuko tunayoyashuhudia sehemu mbalimbali duniani hivi sasa.

Kutunga sheria kwa ushauri (Shura): Uislamu unafundisha kuendesha serikali, kutunga sheria na kufanya maamuzi kwa kuzingatia ushauri na ushirikishaji watu (raia) kama Qur'an inasema katika 3:159 na 42:38. Uislamu hauruhusu udikteta, rejea zake ni Qur'an na Sunnah.

Uwajibikaji wa serikali: Katika mfumo wa siasa unaondeshwa Kiislamu, mtawala na serikali lazima wawajibike kwanza kwa Allah (s.w.) na baadaye kwa raia. Mtawala huwa ni mtumishi wa raia na wote kwa pamoja ni makhalifa wa Allah. Wote watawajibika kwa Allah (s.w.) siku ya mwisho ingawa kwa viwango tofauti. Jukumu la mtawala ni zito zaidi.

Vile vile, katika mfumo wa siasa wa Kiislamu raia yeyote wa kawaida ana uhuru wa kuhoji chochote kuhusiana na mtawala na serikali yake mradi tu abaki katika mipaka ya Qur'an na Sunnah.

Uhuru wa mahakama na usawa mbele ya sheria: Hili linapatikana katika mfumo wa siasa wa Kiislamu ambapo mkuu wa nchi au kiongozi mwingine yeyote hawi juu ya sheria. Mojawapo ya kazi za dola ya Kiislamu ni kuhakikisha haki kwa raia wote. Kigezo cha kuwapambanua waja katika Uislamu ni taqwa (ucha Mungu) tu na si vinginevyo.

--
Juu RUDI
 
Kipindi kile ulinywea mpaka nikakuonea huruma bibii. Ila sasa ni muda wako jiachie mamaa. Fanyeni siasa mpaka katikati ya ibada ni rukhsa. Wala hamjaanza leo ila one day yes
 
Naona unahangaika tu, tatizo lenu la kwanza hamjiamini, la pili, mmewekeza kwenye midomo zaidi ya vitendo. Hizo siasa unazowashauri wenzio, ujue lazima mtumie sheria za nchi, sio sharia zenu.

- Nikuulize; umekuwa ukipiga hizi kelele zako miaka mingi, je, umewahi kubadilisha chochote? Nothing.

Kila nikikusoma, kisaikolojia nakuona unavyoleta haya maandiko yako ya kulalamika hapa kila siku, mara MoU ya kanisa na serikali, mara waislamu mmetengwa, kama ndio unajiona mjanja, wakati kimsingi huna ujanja wowote ule, hizi ni kelele tu unazopiga ambazo hazimsumbui anayejielewa.

Nikwambie na wenzako mjue, hapa duniani siku zote anayeheshimika ni yule anayetenda, sio anayepiga kelele kila siku. Mfano, anayeheshimika ni yule aliyejichanga kwa nguvu zake, akajenga hospitali, kisha serikali ndio ikamuomba imsaidie kuchangia gharama, ili huduma zitolewazo pale, ziwe bora zaidi.

Lakini ajabu, wewe unawekeza kwenye mdomo miaka yote, na unaona sifa, badala uwashauri wenzio huko misikitini nanyi mjichange mjenge hospitali zenu, kisha serikali iwasaidie sehemu ya gharama za kuziendesha, kila siku ni kulia serikali iondoe kuchangia gharama kwa wale waliojenga tayari, huu wako ni mfano wa mindset iliyochakaa.

Hujui wenzako kama walijichanga wakajenga, hawawezi kushindwa kujichanga pia ili kuziendesha, mindset ya bora tukose wote inawadumaza, huwezi kufanana na yule aliyejijenga tayari, huyu tayari yuko mbele yako.

Lastly nikwambie ukweli ujue, hayupo mwenye wasiwasi na Uislamu, hayupo. Utakuwa vipi na wasiwasi kwa yule ambaye hata yeye mwenyewe hajiamini? unayejua miaka yote amewekeza kwenye mdomo na ndio anajiona mjanja? huyu unamuangalia tu, kisha unatabasamu, unaenda zako!.
 
Waislam kwa miaka mingi sana tumejazwa ujinga kwa makusudi kabisa kuaminishwa kuwa ni mwiko kuchanganya siasa na dini.



Adui wa waislamu ni ujinga wa kutokupenda kusoma elimu Dunia,siyo kwamba hawapo wasomi wa kiislamu,wapo ila siyo wengi kwenye mfumo wa maisha,ajira na Serikalini

Japo wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa hapa Bongo,ila shule ni muhimu

Wagalatia wakiongozwa na Kanisa katoliki,linaongoza Kwa kuwa na wasomi wengi,waumini wengi kwenye nafasi nyeti za maamuzi na wenye kipato kizuri na endelevu

Siyo kwamba waislamu hawapo katika siasa,ebu angalia hierarchy ya CCM Kwa sasa,kwenye Chama na jumuiya zake,topmost posts zote zinaongozwa na waislamu

Waislamu wasome kwa wingi,najua kwenye kuzaana mpo vizuri tofauti na wagalatia,someni,msiwe kama wazenji ambao Kila mwaka division 0 zinaongezeka na hii itawapunguzia kulia Lia kuwa NECTA inawafelisha kimakusudi
 
Kipindi kile ulinywea mpaka nikakuonea huruma bibii. Ila sasa ni muda wako jiachie mamaa. Fanyeni siasa mpaka katikati ya ibada ni rukhsa. Wala hamjaanza leo ila one day yes
JPM aliwabana mbupu,wakakaosa pakupumulia
 
Hadi mnadanganywa mlikuwa wapi?

Halafu kwanini waislam huwa mnajiona mna haki kuliko wengine?

Niambie nini madhara kwa wale wasio waislam haswa hii 2023?

Kwa mantiki ya Uzi wako, tuendelee kushirikiana kwenye nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi. Baina ya waislam na wasio waislam?

Nini maoni yako ikiwa serikali itajikuta imeegemea upande mmoja kiutawala ikabase kwe uislam?

Ni dhambi gani itatukuta tusio waislam, hata kama tunatenda mema?

Utapata faida gani faiza fox pale ambapo watu wote watakuwa waislam ingawa matendo yao yatakuwa si ya kumfurahisha mwenyezi MUNGU?

Yaani Kuna jambo linakuja , naliona lileeeeeeeee!!
 
Hadi mnadanganywa mlikuwa wapi?

Halafu kwanini waislam huwa mnajiona mna haki kuliko wengine?

Niambie nini madhara kwa wale wasio waislam haswa hii 2023?

Kwa mantiki ya Uzi wako, tuendelee kushirikiana kwenye nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi. Baina ya waislam na wasio waislam?

Nini maoni yako ikiwa serikali itajikuta imeegemea upande mmoja kiutawala ikabase kwe uislam?

Ni dhambi gani itatukuta tusio waislam, hata kama tunatenda mema?

Utapata faida gani faiza fox pale ambapo watu wote watakuwa waislam ingawa matendo yao yatakuwa si ya kumfurahisha mwenyezi MUNGU?

Yaani Kuna jambo linakuja , naliona lileeeeeeeee!!
Waislamu wanapenda kudeka deka na kudekezwa,yote ni Kwa sababu ya inferiority complex

Na ndo maana hata kuchinja tumewachia Ili waliridike
 
Adui wa waislamu ni ujinga wa kutokupenda kusoma elimu Dunia,siyo kwamba hawapo wasomi wa kiislamu,wapo ila siyo wengi kwenye mfumo wa maisha,ajira na Serikalini

Japo wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa hapa Bongo,ila shule ni muhimu

Wagalatia wakiongozwa na Kanisa katoliki,linaongoza Kwa kuwa na wasomi wengi,waumini wengi kwenye nafasi nyeti za maamuzi na wenye kipato kizuri na endelevu

Siyo kwamba waislamu hawapo katika siasa,ebu angalia hierarchy ya CCM Kwa sasa,kwenye Chama na jumuiya zake,topmost posts zote zinaongozwa na waislamu

Waislamu wasome kwa wingi,najua kwenye kuzaana mpomvizuri tofauti na wagalatia,someni,msiwe kama wazenji ambao Kila mwaka division 0 zinaongezeka na hii itawapunguzia kulia Lia kuwa NECTA inawafelisha kimakusudi
Waislamu hawajasoma kama unayoandika nikweli, lakini wanapochaguliwa kwenye nafasi za uongozi huku wakiwa nasifa zote mnasema ni Udini, lakini Mgalatia akichagua wagalatia wenzake mnasema aliechaguliwa anavigezo.

Mfano mdogo Samia akichagua Muislamu katika nafasi ya uongozi ni Udini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom