Zitto ajutia kuingia kwenye siasa?

Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,701
1,799
Haya jamani wana Jf, jana na leo katika shirika la habari TBC1 kipindi cha jambo Tanzania Zito amekiri kuwa siasa halikuwa chaguo lake la kwanza, kwa maana hii mi natasfiri kwamba ni mamluki wa siasa, na anasema kuwa siasa hailipi anatamani kutoka lakini anashindwa.

Na amekiri kuwa ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu ila tatizo ni kuwasilisha barua. Mambo mengi ameongea, ambayo amenishangaza lakini tutamchambua siku nyingine.

Kwa maana hii basi, wanasiasa wengi ni mamluki na ndo maana tunashindwa kufanya siasa.
 
Haya jamani wana Jf, jana na leo katika shirika la habari TBC1 kipindi cha jambo Tanzania Zito akiri kuwa siasa halikuwa chaguo lake la kwanza, kwa maana hii mi na tasfiri kwamba ni maamluki wa siasa, na anasema kuwa siasa hailipi anatamani kutoka lakini anashindwa. na amekiri kuwa ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu ila tattizo ni kuwasilisha barua. mambo mengi ameongea, ambayo amenishangaza lakini tutamchambua siku nyingine.
kwa maana hii basi wanasiasa wengi ni mamluki na ndo maana tunashindwa kufanya siasa.

Dah,kazi kwelikweli,yaani unamuwekea Zitto maneno mdomoni mkuu..lol

Kimsingi Siasa ni chaguo la pili la wanasiasa walio wengi,ndio maana wengi ama huanzia kwenye taaluma fulani na baadae huishia kwenye siasa,kwa mfano;

-Dk W.P. Slaa kabla ya kujiunga CHADEMA alikuwa ni padri wa kanisa Katoliki na Katibu mkuu wa T.E.C

-Prof.Ibrahim H. Lipumba kabla ya kujiunga C.U.F alikuwa ni mhadhiri na(kama sikosei) mshauri wa Rais wa masuala ya uchumi

-Freeman A. Mbowe yeye alikuwa mfanya biashara(na bado ni mfanya biashara mahiri tu)

Mifano ni mingi tu(hata viongozi wengi wa serikali iliyopo madarakani wengi wao ama walikuwa ni watumishi watendaji serikalini ama wafanya biashara)

So si vizuri na si sahihi kumuita Zitto ni mamluki wa kisiasa kwa vile tu amesema Siasa lilikuwa ni chaguo lake la pili
 
ni mtizamo tu!
i mean ni HOJA YAKO BINAFSI

very IMMATERIAL anyways!
so sorry
 
Nimemuona zito akihojiwa TBC 1 leo asubuhi na kwa kweli sasa naamini yaliyotangulia kuelezwa,si mkweli!!

Anadai siasa sio chaguo lake la kwanza lakini anataka uenyekiti wa chama, for what?

Anapinga maamuzi ya vikao halali vya vyama hadharani wakati yeye ni kiongozi,anapotumia maneno "sikubaliani na maamuzi".

Zito ameshakuwa big headed and I believe he is going heading for a fall.

Wananchi hasa wapenda mabadiliko wanasononeka sana na kauli za Zito na masononeko yao ndio itakuwa laana kwa Zito
 
Duh!! Binafsi, nimechoshwa na mijadala inayomhusu zitto humu jamvini
 
shapu huelewi nini? namaanisha kuwa anatamani kuacha siasa au tuseme imemshinda.
 
Ilishasemwa humu kuwa kaahidiwa something CCM. Sasa anatafuta tu namna ya kutoka sema kutoka upinnzani siyo rahisi. Chadema kama wajanja wamkaukie uone atakavyotapatapa kwa vile anajuwa Chadema wakimfukuza haitamharibia chart yake ila akijitoa mwenyewe umaarufu wake (kama bado upo) utakwisha.
 
ndio Geoff huu ni mtazamo wangu, lakini kwa mtu kama zito siasa ya miaka 4 leo kusema anatamani kutoka, dont you see the issue here? alikuja kujaribu? au he fears to loose election?
 
This is not a breaking news,it has been said by himself in public since year 2007 that his first choice is to become a lecturer.
 
This is not a breaking news,it has been said by himself in public since year 2007 that his first choice is to become a lecturer.

Not a lecturer,but to become a teacher....probably a primary school teacher...
 
ndio Geoff huu ni mtazamo wangu, lakini kwa mtu kama zito siasa ya miaka 4 leo kusema anatamani kutoka, dont you see the issue here? alikuja kujaribu? au he fears to loose election?

Remmy,
wewe umeanzia katikati habari za zitto ndio maana unamwita mamluki lakini zitto sio mamluki. Halafu inaonekana wewe ni mtu wa kuhukumu haraka, tafadhali take time before you make a judgement
 
Yeye mwenyewe Zitto alituambia aliingia Chadema akiwa na miaka 16 hawezi kutoka Chadema kwa sababu familia yote ni Chadema hii ni sababu ya kitoto kabisa ina maana yeye angetoka ila anaona aibu tu? kweli huyu si mwanasiasa nimeanza kuamini ni Celebrity wa saisa anapoona watu wana mfuatafuata ndiyo furaha yake is not a real fighter.

Kama siasa si chaguo la kwanza ina maana chaguo la kwanza alichagua akiwa na umri gani, we should be very careful with this guy. Sasa alikuwa anagombea uenyekiti wa nini kama si kuvuruga wenzake. Mimi nilikuwa muumini mkubwa tu wa Zitto basi aondoke salama. Kama msemaji mmoja alivyosema hapo juu Chadema wakauke kama hawamuoni wasije wakalogwa kumfukuza ajiondoe mwenyewe ila waanze pole pole kutomshirikisha kwenye mambo nyeti ya chama.

Najua Chadema bado wanamhitaji lakini huwezi kumlazimisha ng'ombe kunywa maji.
 
haya kadri siku zinavyokwenda ndio rangi halisi za Zito Kabwe zinazidi kujionyesha, haya Zito acha aibu fika Kinondoni leta barua ujiuzulu maana umeisha pata mkate wako huna sababu ya kubakia kwenye siasa.
 
Zitto kasisitiza tena kuwa uchaguzi mkuu ujao yeye ataiunga mkono NCCR huko Kigoma kusini ambako mgombea atakuwa rafiki yake Kafulila. Najaribu kufikiria uwanja wa kampeni utakavyokuwa pale kamanda wa anga atakapotua kumfanyia kampeni mgombea wa CHADEMA (Most likely, Hassanali ambaye ni mmoja wa wadhamini wa chama) huku Zitto na Mbatia wakiwaponda kwa kumnadi Kafulila. Patakuwa patamu!
 
Sielewi fikra na mtizamo wake juu ya Ustawi wa CHADEMA HASA UKIZINGATIA yeye ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Natilia shaka hatima yake kisiasa, kweli CHADEMA Imemkaribisha kuleta barua ya kujiuzulu ili ajiunge na chama anachodhani kinaweza kutimiza malengo yake ya kuiona Tanzania yenye neema tele kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho.
 
Dah,kazi kwelikweli,yaani unamuwekea Zitto maneno mdomoni mkuu..lol

Kimsingi Siasa ni chaguo la pili la wanasiasa walio wengi,ndio maana wengi ama huanzia kwenye taaluma fulani na baadae huishia kwenye siasa,kwa mfano;

-Dk W.P. Slaa kabla ya kujiunga CHADEMA alikuwa ni padri wa kanisa Katoliki na Katibu mkuu wa T.E.C

-Prof.Ibrahim H. Lipumba kabla ya kujiunga C.U.F alikuwa ni mhadhiri na(kama sikosei) mshauri wa Rais wa masuala ya uchumi

-Freeman A. Mbowe yeye alikuwa mfanya biashara(na bado ni mfanya biashara mahiri tu)

Mifano ni mingi tu(hata viongozi wengi wa serikali iliyopo madarakani wengi wao ama walikuwa ni watumishi watendaji serikalini ama wafanya biashara)

So si vizuri na si sahihi kumuita Zitto ni mamluki wa kisiasa kwa vile tu amesema Siasa lilikuwa ni chaguo lake la pili

HAYA NI MOJA YA KAJIBU MAZURI kwa mwaka huu, alafu huyu mleta hoja anaongea then ETI ANASEMA TUTAMJADIRI SIKU NYINGINE. Mungu wangu, kama hukujiandaa si ungeiweka kapuni hiyo POSTING YAKO???
 
Yaani kwa kweli Zitto ameni-diappoint sana! Kwa kijana kuwa QUITTER! naomba msaada wa kiswahili chake hapo! Kama kijana, you are never defeated untill you give up! Halahala asije tu akaingia CCM, hapo ndo heshima yooote itaisha!
 
Si pia alisema ana ndoto za kuja kuwa mkuu wa nchi. Sasa kama ubunge wa miaka mitano unamtoa jasho itakuwaje urais wa miika kumi??? Anatafuta njia ya kukimbilia CCM huyu!!!
 
shapu huelewi nini? namaanisha kuwa anatamani kuacha siasa au tuseme imemshinda.

anatamani kuacha?? sasa nini kinamshikilia si aache kama anaona its time for him to quit!!
 
Back
Top Bottom