Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,379
Erickb52 katika pozi
Sublakheri wapenzi wasomaji wa JF, kwa wale ndugu zangu wakristo nasema Bwana Yesu asifiwe sana na wale ndugu zangu wengine Wapagani nawasalimia kwa kikwetu "Mizimu ya tate ikagone"
Haya tena leo mjengoni nipo na ndugu yetu, jamaa yetu, rafiki yetu na kibuzi chetu Erickb52. Mahojiano yangu na Erickb52 yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.
Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza Erickb52 swali lolote na yeye bila shaka atayajibu maswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.
Kwa kuanza ninayo maswali kumi na mbili ambayo ningependa kumuuliza Erickb52:
1. Je umezaliwa awamu ipi ya utawala katika nchi yetu?
2. Je Ulishawahi kucheza mchezo wa baba na mama na ule wa kujificha utotoni?
3. Je umeoa? Kama umeoa, Je una watoto wangapi, na kama hujaoa, ina maana huna hata kabinti ka kuchombeza?
4. Je umewahi kupitisha usiku na kahaba?
5. Je ulipojivinjari na kahaba uliona tofauti yoyote na unachokipata kutoka kwa Mke/Mpenzi wako?
6. Je umetahiriwa, kama umetahiriwa, ulitahiriwa ukiwa na umri gani, na je ulitahiriwa kwa ganzi au kavu kavu kama wamasai?
7. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
8. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana
9. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
10. Ukipata fursa ya kupata staftahi na Preta, utamshauri kitu gani?
11. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
12. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….
Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Bwana Erickb52 atakuja kuyajibu maswali yenu.
Karibuni sana
Last edited by a moderator: