'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'!

ngoja tuwasaidie japo kidogo tu

8 Januari 2012
CHADEMA; Urais utaamriwa kwa mahitaji ya Umma na Sifa za Kiongozi, si uchu au utashi wa watu/mtu binafsi
KUMEKUWEPO taarifa zinazosambazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, zikiwa na nia ya kuonesha kuwa kuna mbio za kuwania urais ndani ya chama na kuwa kuna baadhi ya watu wanapewa nafasi kubwa kugombea nafasi hiyo, kiasi kwamba sasa ndani ya CHADEMA “hapatoshi” kwa ajili ya kuwania urais.Chama kinapenda kutoa taarifa sahihi kwa wanachama, wapenzi, washabiki wake na Watanzania wote kwa ujumla, juu ya suala hili ambalo linaonekana kuwa na nia ya kutaka kukifananisha CHADEMA na vyama vingine au kuwafananisha viongozi wa chama hiki na viongozi wa vyama vingine ambao wamekuwa wakilifanya suala la kugombea nafasi ya urais kuwa linaongozwa na kuamriwa kwa utashi binafsi wa mtu, ukiongozwa na uchu na tamaa ya nafasi ya vyeo.Kwa sasa ndani ya CHADEMA kitu hicho cha ‘kupamba moto’ kwa ajili ya kuwania urais hakipo na wala hakiwezi kuwepo. Hasa kwa sasa ambapo chama kimejikita kuzidi kujijenga kwa kutimiza wajibu wake, kama serikali mbadala inayosubiri kupata ridhaa ya wananchi kuongoza nchi.Kwa muda huu, kwa CHADEMA suala muhimu ni namna ya kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii pana ya Watanzania na kisha kutafuta majawabu au masuluhisho ya kudumu, kwa kushirikiana na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao, kwa ajili ya maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda muhimu, chama kinasimamia na hakiwezi kutolewa kwenye mstari kwa watu kukimbilia urais.Kwa CHADEMA, siku zote suala la urais linategemea na kufuata mahitaji mapana ya Watanzania, kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa, utashi au uchu wa watu/mtu binafsi. Na katika kufikia hatma ya mahitaji/ maslahi mapana ya wananchi, chama hiki siku zote huamua kwa kufuata na kuzingatia katiba, kanuni na taratibu zake, si vinginevyo.Ni uwezo na umakini wa kuzingatia mahitaji ya chama na maslahi mapana ya umma katika kuamua masuala mazito kwa mstakabali wa taifa, huku kikifuata katiba yake, kanuni na taratibu, ndiyo umekipambanua CHADEMA kuendelea kuwa chama makini, kinachoaminiwa kwa dhati na Watanzania, na kiupekee kuwa kinastahili kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii.Mahitaji ya chama na ya Watanzania ndiyo yaliyotumika kupata wagombea urais wa CHADEMA katika chaguzi kuu mbili, mwaka 2005 na 2010. kwa kuzingatia mtazamo huo, mara zote hizo mbili, wagombea waliombwa, wala hawakuongozwa na uchu au tamaa ya madaraka.Hali itakuwa hivyo hivyo wakati ukiwadia wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015, kamwe utashi, uchu au maslahi binafsi ya mtu hayawezi kupata/kupewa nafasi ndani ya CHADEMA.Kwa CHADEMA, urais si cheo, ni dhamana ya utumishi kwa umma, suala ambalo linazingatia masuala muhimu, ambayo ni mahitaji ya wananchi (nchi) na kisha sifa za mtu husika kuwa kiongozi wa nafasi hiyo. Basi.Kwa sasa CHADEMA na viongozi wake makini hawawezi kuanza mbio za kusaka urais, badala yake, muda wa sasa unatumika kujikita katika kushughulikia na kutafuta ufumbuzi wa vyanzo vya matatizo ya jamii yanayozidi kuongezeka, huku serikali ikiishia kushughulika na dalili/matokeo, hivyo kukosa majawabu ya kudumu na kuishia kutoa lawama kwa wakosoaji wake.Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi.Daima, CHADEMA na viongozi wake makini, kitaendelea kuweka mbele kwanza kabla ya kitu kingine chochote, mapambano dhidi ya vyanzo vya matatizo kama vile umaskini (ugumu wa maisha), rushwa na ufisadi mwingine lukuki unaozidi kutafuna na kuangamiza taifa na watu wake, hali inayowafanya Watanzania kuwa katika mtanziko na mkwamo mkubwa kimaendeleo, miaka 50 baada ya uhuru, huku wakiwa ndani ya taifa lenye baraka tele za utajiri wa rasilimali na kila aina ya nyenzo muhimu inayohitajika kwa maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda ya muhimu kwa sasa.Imetolewa leo, Januari 8, 2012, Dar es Salaam
Kurugenzi ya Habari na UeneziMakao Makuu ya CHADEMA Taifa
 
Zitto Kabwe

Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA

https://www.facebook.com/zittokabwe

Asante ndugu yangu zito kwa kujibu haraka hoja hii. Kila hoja inayotaka kudhoofisha chama inabidi ijibiwe haraka na kwa uhakika.
 
[h=6]Zitto Kabwe
[/h][h=6]Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA[/h]

https://www.facebook.com/zittokabwe
Na nyie kina Zitto mnakuwa wanafki mno, mnakuwa tu sasa kama ccm yaani mnasubiri mpaka mahoja haya yanatapakaa vinyesi ndipo mnaibuka hovyo na kukanusha kishkajishkaji tu. Ulipaswa kulitolea maelezo hili toka awali lakini uliamua kuliacha kupima upepo eti? Mtaua chama na mauroho yenu....

Pangu Pakavu.
 
[h=6]Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA[/h]
Source Facebook.
 
zitto sikiliza kwa makini ule wimbo wa wanasiasa vigeugeu. Hata ulipotangaza hukutushirikisha vipi hili unatushirikisha? au ni mbinu ya kutaka kutushitukiza na kupima upepo.
 
ulitaka kugombea uenyekiti wa chadema hukufanikiwa pengine ungetuomba ushauri tungekwambia gombea au usigombee. wewe Zitto ni mtata unatangaza nagombea mara keshosigombei kesho kutwa utasema wazee wameniomba nimekubali kugombea.
 
Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA

Source Facebook.

Hii imekata mizizi yote ya fitina na nimeisevu hii kwa ajili ya mwaka 2015, Hongera zitto kwa kukubali kubadilika.
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.
 
Roho mbaya inawasumbua hili gazeti na kwa mara ya kwanza nimpongeze Zitto kwa kuthibitisha kua hatogombea Urais 2015 bali atamuunga mkono mgombea wa CDM

pamoja na Msiba mambo mengine yanaendelea, Msiba haujafuta mnyukano huo ila unauweka likizo fupi Zito kusema hivyo ni dalili ya kuona kuwa hawezi kupata nafasi kwenye mnyukano huo ama wamekubaliana kitu..........
 
ulitaka kugombea uenyekiti wa chadema hukufanikiwa pengine ungetuomba ushauri tungekwambia gombea au usigombee. wewe Zitto ni mtata unatangaza nagombea mara keshosigombei kesho kutwa utasema wazee wameniomba nimekubali kugombea.

MAMA POROJO HAYO YA KWELI HUYO KIJANA MJANJA SANA NA ANAWAPUMBAZA WENZAKE, ZITO ANATUMIA MATOKEO YA TAFITI MBALIMBALI NA HIVYO ANAJUA WAZI KUWA YEYE NI MAARUFU KULIKO MWENYEKITI WAKE.NA NDIYO MAANA ALITAKA KUGOMBEA UENYEKITI AKIWA NA UHAKIKA, NA PIA KWA LENGO LA PILI LA KUMDHIBITI PADRI KATIKA KUWANIA KUTEULIWA NA CDM KUGOMBEA URAIS.....................MBOWE HILO ANALIJUA WAZI PIA KUWA YUKO NYUMA YA PAFRI NA KIJANA HUYO KWA UMAARUFU KTK CDM HIVYO NAYE ANAONA NI BORA AKABAKIA KWENYE UBUNGE WAKE NA HATA UMAKAMU M,KITI MAANA YEYE NDOTO YA URAISI HANA NA HAJATHUBUTU NA HATATHUBUTU KUONGEA (sababu.........elimu). ZITOOOOOOOOOO NI KAFULILA/HAMAD RASHIDI WA CDM IKO SIKU ATAWACHACHAFYA TU NYIE TULIENI MUONE MIMI NI RAFIKI YANGU SAANA NAMJUA ANAO MSIMAMO WA NDANI UNAOSOMEKA USONI
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.

As a great thinker, you must have fast thinking! Sintagombea urais inamaana hatajitokeza kuchukua form. Atakayejitokeza na kupitishwa na chama basi atamuunga mkono. Hata kama chama kikiona ndiyeatakayekuwa anafaa kulingana na mazingira na mahitaji ya wakati huo basi yeye ndiye atakayebeba ilani na bendera ya chama. Ndio maana ya kumuunga mkono mgombea wa chadema. Au ulitaka maelezo gani ya ziada!?
 
Magazeti kama ya majira, uhuru, habari leo, mi napendekeza fedha za kuyaendesha haya magazeti wangepewa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kupunguza tatizo la mikopo, kwani magazeti haya yanaandika upupu 2 wa kimamluki.
 
utamuungaje mgombea wa chadema wakati hujui atakuwa ni nani? pengine chama kitakupendekeza wewe? basi ungesema nikipendekezwa na chama sitakubali. kauli yako haisemi nafsi yako kama itatokea wewe ndiye mteule wa chama.

Zitto ni mwana chama wa Chadema,tena kiongozi muandamizi ulitaka amuunge mkono mgombea wa CCM?
 
Zitto Kabwe

Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA

https://www.facebook.com/zittokabwe

Zito hapa umenena, jaribu kukanusha haya mambo kama kiongozi wa Chama
 
Magazeti kama ya majira, uhuru, habari leo, mi napendekeza fedha za kuyaendesha haya magazeti wangepewa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kupunguza tatizo la mikopo, kwani magazeti haya yanaandika upupu 2 wa kimamluki.

Jamba Leo Je?
 
Sasa Zitto ndiye anayepatia kuendeleza malumbano wakati wa msiba? Tena Facebook?

Sasa yeye na hao anaowasema wanakuwa na tofauti gani?

Kama kweli unaheshimu msiba, hulumbani wakati wa msiba period. Utasubiri msiba uishe utalumbana mpaka liamba. Ukilumbana wakati una msiba unaonekana wewe Zitto na hao Majira wote sawa.

Mkuu kiranga,
Zitto Kuandika kwenye face book yake sentensi ' sitagombea urais 2015, nitamuunga mkono mgombea wa chadema' ni malumbano au ni kuweka ukweli hadharani?

Hongera zitto kwa kuwakatia wabaya wetu mzizi wa fitina, sasa wakatafute hoja nyingine. You are very correct. Big up, mimi najua wewe unachosema ni kweli. Mengine ni speculation.
 
Back
Top Bottom