Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Wakikagua Miradi ya Umwagiliaji Arusha, Tabora na Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti mkoani Arusha kufuatilia utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji kwenye mashamba ya utafiti- TARI na Mashamba ya Uzalishaji wa Mbegu- ASA.

Pia, Ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti ilifika kwenye shamba la Mbegu Kilimi Nzega, Tabora kufuatilia utekelezaji za mradi ambao hadi sasa umegharibu zaidi ya Tsh Bil 6.

Shamba linatumia teknolojia ya kisasa kabisa ya umwagiliaji ya Center Pivot mbapo mategemeo ni shamba litaongeza uzalishaji wa mbegu kutoka Tani 200 za sasa hadi Tani 3000 kwa mwaka.

Aidha, Kamati imetembelea mradi mkubwa wa Umwagiliaji wa Mkombozi uliopo Tarafa ya Pawaga, Isimani Iringa. Mradi utakaogarimu Tsh Bil 55 na utanufaisha zaidi ya wananchi elfu 16 kwa kuanzia.

Wananchi wa Isimani na Iringa kwa ujumla wataweza kulima mpunga na mazao mengine kwa misimu zaidi ya mitatu kwa mwaka sasa.

WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.35.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.42.42.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.35.55.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.35.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.42.43(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-20 at 17.42.43(2).jpeg
 
Back
Top Bottom