Fantastic... Sasa itakuwaje MUUNGANO UKIVUNJIKA ? HIYO MELI ITAKUWA INAFANYA
ZIARA kati ya PEMBA na ZANZIBAR ?
Fantastic... Sasa itakuwaje MUUNGANO UKIVUNJIKA ? HIYO MELI ITAKUWA INAFANYA
ZIARA kati ya PEMBA na ZANZIBAR ?
Hii ni boti sio meli
Kwani meli zinaleta mizigo tanzania ni za kitanzania.?
Fantastic... Sasa itakuwaje MUUNGANO UKIVUNJIKA ? HIYO MELI ITAKUWA INAFANYA
ZIARA kati ya PEMBA na ZANZIBAR ?
hONGERA SANA BAKHRESSA. hii ndiyo faida ya kuwa na mabepari katika nchi. wao mabepari siku zote huangalia quality kabla ya kununua kitu. Hii meli inanikumbusha kivuko kimoja kipo pale new york city kinachopeleka watu starten Ireland. kinachukua watu 1000 kwa mpigo na humo ndani ni mzuri sana kama ilivyo hiyo meli ya bakhressa.Hongera yake bwana bakhressa
Muungano ukivunjika...biashara itayumba sana!!
Ni mpya au imepakwa rangi. Maji ya bahari au ziwani, isije ikawa kama hizi zilizozama.
Mtukumbukage na sisi wa ziwa nyasa, au ndo tushakuwa wamalawi?
Kwani meli zinaleta mizigo tanzania ni za kitanzania.?
Ni mpya au imepakwa rangi. Maji ya bahari au ziwani, isije ikawa kama hizi zilizozama.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200. Meneja Mkuu wa Kamuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratizo za mamlaka mbalimbali. Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari. Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.
MELI ZA MZEE AZAM unajua hazijawahi KUZAMA???
Kwa Ukweli ni MPYA... Tuache SIASA .