Zanzibar: Meli mpya yawasili!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

attachment.php


Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200. Meneja Mkuu wa Kamuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratizo za mamlaka mbalimbali. Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari. Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.
 
Monday, October 1, 2012


IMG-20121001-WA003.jpg


Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.
IMG-20121001-WA001.jpg

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
IMG-20121001-WA005.jpg

Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
IMG-20121001-WA008.jpg

Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
IMG-20121001-WA009.jpg

Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
IMG-20121001-WA0041.jpg

Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
IMG-20121001-WA006.jpg

 

Fantastic... Sasa itakuwaje MUUNGANO UKIVUNJIKA ? HIYO MELI ITAKUWA INAFANYA

ZIARA kati ya PEMBA na
ZANZIBAR ?
 
Surely he does good for zanzibar

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sasa wachome tena na kanisa jingine alafu ndipo wataona nini atawafinyia huyu Mungu mkuu wa Israel kama ktk zile meli 2 zilizopita.

Enewei, God is good all the time and all the time God is good.
 
Ni nzuri lakin HII SIO HABARI YA KISIASA kumbuka hapa ni jukwaa la siasa

Kumbuka Issue ilikuwa ya KISIASA haukumbuki MBUNGE WAZIRI WA CUF alijiuzulu na WAZANZIBARI walitaka

Waziri WA NDANI wa TANGANYIKA pia ajiuzulu ? Haukumbuki WABUNGE, Bungeni wote waliondoka wa CHADEMA na

CUF na WA CCM WAISLAMU isipokuwa BIG BOSS ZITTO KABWE ???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom