N-handsome
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,453
- 556
Imekaa vibaya wala haijatulia, why now near election? katumwa na nani? na bado tutasikia mengi sana prior to 2010
Mpaka sasa naweza kusema mambo matatu
1.Mzee ni Mbaguzi
2.Familia imemshinda
3.Ana wivu,fitina na chuki na watu anaoshindana nao kibiashara
Haiingii akilini leo kusema mafisadi ni watu watano tu,ambao tena wamehusishwa na kesi za hivi karibuni za kifisadi.
Anogopa kuwataja watu ambao wanafahamika
kabisa kuwa wamertufiksha hapa.
Hataki kuigusa CCM na watu wake kwa kuwa anawaogopa watamaliza.
Ameweza kujenga hoja kuwa mafisadi ni wahindi tu,na tuwabague wakati hao hao wahindi wanatumia na mafisadi mama ambao wapo serikalini,wakubwa ambo mengi anawaogopa kuwasema
Labda wewe ndiyo une-clarify wazi hivi hao jamaa waliotajwa hapo ni weupi, kwa standard yako! Mie sioni hata kidogo lipo suala la rangi; hapa ni ufisadi tu; mweusi au mweupi ufisadi ni ule ule; nyie ndiyo ndumila kuwili. Hapo chini umetaja dini; lo; hapo ndipo tunachoshana kabisa. Kwa nusubongo yako umeongelea vitu ambavyo vinakutawala wewe katika hizi discussions na maamuzi, Dini na Rangi ya mtu; hapa hamna vyote viwili; bali ni Utaifa; hata hao wewe uliowataja ni WaTanzania kwa hiyo punguza hiyo jazba. Mengi kafanya hatua moja mbele labda ungeendeleza jingine hapo huwezi kum-demoralise mtu!
Mengi aanika mafisadi papa
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi ameibuka na kudai nchi inahujumiwa kundi dogo la watu aliowaita 'mafisadi papa' na wamejiandaa kutoa roho za wanaowapinga kwa gharama yoyote.
Bw. Mengi alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kuwa mafisadi hao wameifikisha nchi pabaya kwani hawataki kuguswa.
Aliwataja watu hao wakiwemo wafanyabiashara na wanasiasa (majina tunayo) na kueleza kuwa wameivuruga nchi kwa kiasi kikubwa.
"Nia njema ya Rais Jakaya Kikwete ya kupambana na mafisadi na aina zote za uovu zimewashtua mafisadi na sasa wamecharuka wanapambana na watu wote wanaomsaidia Rais kupambana nao kuwazuia wasiendelee kuitafuna nchi,"alisema Bw. Mengi.
Bw. Mengi alisema mafisadi hao wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na baya zaidi, yamehamisha pesa hizo nje ya nchi.
Alisema wanaotuhumiwa wanahusishwa na karibu ya kila kashfa kubwa iliyoibuka hapa nchini.
"Jitihada kubwa za Rais Kikwete kuleta maendeleo na Maisha Bora kwa kila Mtanzania zinadhoofishwa na wizi mkubwa wa rasilimali za Taifa,"alisema Bw. Mengi na kuongeza;
"Bado Watanzania wengi wanaandamwa na umasikini mkubwa, hawajui hata mlo mmoja kwa siku utatoka wapi"
Bw. Mengi ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini, alisema cha kusikitisha ni kwamba pale Mtanzania mwema mwenye uwezo anaposaidia jamii kuondokana na umaskini, mafisadi wamekuwa wakipiga kelele kuwa misaada ya aina hiyo ina agenda na kupinga kwa kutaka Watanzania wafe njaa na matatizo mengine.
"Inavyoonekana nia ya mafisadi hao sasa ni kuvuruga nchi na si ajabu wakaunga mkono matatizo yanayotokana na kampuni ya Kuvuna na Kupanda mbegu, DECI na Watanzania wakabaki wakifukuzana na wachungaji bila kujiuliza ni kina nani hasa wanachochea vurugu hizo,"alisema.
Bw. Mengi alisema DECI imeleta matatizo makubwa katika nchi mbalimbali duniani, ambapo iliiangusha Serikali ya Albania na kwamba hatma yake ikiendelea kuchochewa na watu wapenda vurugu, italeta matatizo makubwa hapa nchini.
Alisema kuwa mafisadi papa hao hawaibi rasilimali tu, bali wanaiba pia muda, badala ya wananchi kutumia muda katika shughuli za maendeleo, wanajikuta wakiutumia kupambana nao.
Bw. Mengi alidai mafisadi hao wanatumia fedha walizoiba kuanzisha magazeti ya kujenga kiburi cha kudharau Watanzania, kuwatukana na kuwanyanyasa.
"Inakuwa ni kesi ya mwizi kumkimbiza na kumpiga aliyeibiwa. Hata sasa hivi mafisadi hao wanaendelea kutumia uwezo wao wa kiuchumi uliotokana na wizi wa rasilimali za nchi kuwashawishi na kupata miradi mikubwa mikubwa kwa kutumia majina tofauti tofauti huku wakipuuza kabisa kelele za wananchi kuhusu ufisadi wao,"alisema.
Alisema Watanzania wanaolia na ufisadi ni mamilioni wakiongozwa na Rais Kikwete, lakini wachache waliojitokeza na wanajulikana kwa majina.
Alieleza kuwa hata hivyo kuna tetesi kwamba mafisadi papa wamedhamiria kuwatokomeza kabisa wapinga ufisadi wanaojulikana kwa majina.
Alisema mafisadi hao ni lazima wajue kwamba iwapo wapambanaji hao wa ufisadi watadhuriwa kwa njia yoyote, ndani au nje ya nchi, watawajibishwa na Watanzania.
Alisema mafisadi hao wanafanya kila wawezalo kuhakikisha Watanzania wanaopiga vita ufisadi, wanaangamia kwa njia mbalimbali zikwemo sumu, ajali au kwa kupigwa risasi ili kuondoa ushahidi.
"Watanzania mtasikia tu kwamba fulani amefia nje ya nchi na mtachukulia kama kitu cha kawaida kumbe mafisadi ndio waliotekeleza azma yao, ni lazima muwe macho kwani wanataka kuisambaratisha nchi,"alisema.
Aliwataka Watanzania kujiuliza mafisadi wanapata wapi ujasiri, majigambo, dharau, nguvu za kuwatukana na kuwanyanyasa ?
Alisema mafisadi wote hususani wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa ni lazima washughulikiwe, la sivyo wataiyumbisha na kuitikisa nchi na kwamba ni lazima Watanzania waone kwamba sasa nchi imefika mahali pa kusema imetosha.
Bw. Mengi alisema amejitoa muhanga kupigana vita dhidi ya mafisadi na kubainisha kuwa yeyote atakayekerwa na hatua ya kuitwa 'fisadi papa 'aende mahakamani ili wakapambane kisheria.
SOURCE; MAJIRA
Je vita yetu ya kupambana na umaskini itafanikiwa kwa kuwataja tuu mafisadi hadharani??
Kuna haja ya kupambana na mafisadi wenyewe au wale wanaowapa nafasi nzuri ya kutuibia???
Hapa jamvini naomba tujadili kwa kina na mnisaidie kuelewa zaidi!!!!!
Bado ninaamini ccm ndo tatizo kubwa la umaskini tunaoendelea nao mpaka sasa....
Mkuu, licha ya kwamba uchambuzi wa 'negativity' sio kitu kigeni, LAKINI hii itaigharimu Tanzania safari ndefu sana sababu ya uchanga na umasikini wa nchi yetu. Tunajaribu kujenga 'mentality' isiyomwafaka kwa janga la ufisadi ambao wote tunajua kwamba bila ya kuutokomeza hakuna hatua tutakayopiga. Inabidi tubasilike na kufumba macho pale tunapopata mtu anayeweza kujitokeza na kukemea jambo ambalo tunajua linaiangamiza nchi. Mengi, Mwakyembe, Kilango, ..., wamethubutu kusema wazi kile ambacho hakuna yeyote anaweza kupinga kwamba sio cha kweli. Ukiangalia nafasi za hawa watu wote, wanaweza kukaa kimya na wakaendelea kula kuku kwa uhai wao uliobaki, lakini wanasema kwa kuwa wanaguswa na wanataka tubadilike.Mkodeleaji and the Like;
Mengi ametaja mafisadi anaowajua, na sisi wote tunawajua. That is fine, he is brave and then he played his part.
Sasa wewe Mkodoleaji (na the like); mnajua wazi kuwa Mengi anawaacha wengine pembeni, kama Muungwana JK, yes, mie naamini kabisa JK is a major culprit; (and I have stated this before); Sasa ni zamu yako kusimama na kusema JK ni fisadi mkuu, you have that freedom, lakini kumkandamiza Mengi kwa kazi nzuri aliyoifanya si vizuri. Kumbuka kuwa unavyoanza kum-discourage mtu kama huyu shujaa, then you demorlarise others also. It is then your next part to take on JK; let us go one step forward instead of backward!
Mengi anasumbuliwa na Maradhi ya UGOZI na ndio maana aliowataja wote ni WEUPE, Hii ni hatari sana kwa TANZANIA yetu hasa kwa wakati huu ambao CCM imeifikisha Nchi pahala pabaya kwa kuwaweka Watanzania katika Umasikini wa Kutupwa.Kauli yake inaweza kuchochea fujo kati ya Sisi Walalahoi na wale Weupe wote Wenye Kiapato kwa Dhana tu ya Kuwa Wote ni MAFISADI.
Ukitizama kwa umakini kauli yake imeficha jambo moja kubwa nalo ni lile alilolisema Makamba kuwa Mengi anaajenda ya SIRI ya Kuimaliza CCM pamoja na KIKWETE sio Kweli kama anampenda Kikwete hampendi hata kidogo na anampiga Vita kwani likitokea lolote baya kwa kauli ya Mengi litammaliza Kikwete Kisiasa.
Hivi Mengi anamficha nani kama nae sie FISADIIIII Hii inajulikana au alishindwa nini Kumtaja MKAPA, YONA , MRAMBA, CHENGE, MARANADA IDDI SIMBA, KARAMAGI nk au kwa kuwa hawa ni WEUSI na Wengi wa Dini yake Mengiii ? au Kwao ni Kumojaaaaaaaa.
CCM Yote imejaaa uchafu uliokithiri akiwemo na yeye Mengi kama mwanachama wa CCM Hivi karibuni Mengi huyu huyu MNAFIKI alimwaga MIlioni Mia moja Kwa Umoja wa WANAWAKE CCM Kule mkowani Mbeya akijuwa kuwa ni Umoja wa Chama Cha Mafisadi sasa aeleweke nini Mzee Huyu kama sio Ndumila Kuwili wa Ufisadiiiiiiiiiiiii.
Makamba mwenyewe siyo msafi, hilo tunalifahamu. Tunaweza kusema anakumbatia mafisadi, kama moto umeanza kuwawakia hao mafisadi naye babu Makamba aweke kichwa maji, moto huo kuuzima ni ngumu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Hao mafisadi kawaanika vipi? Kamtaja nani? Kipi kipya alichosema? Mbona tunaridhika kirahisi hivi? Hamna substance katika alichoongea bali posturing tu.
Amandla........
Mkuu hii ni janja ya nyani tuu,mahindi yanakomaa shambani,Wakati umefika kujitakasa kwa kila njia hata kama ni kuyatosa magabacholi wazawa wasalimike haya.Mengi ni kipaza sauti tuu wala asiudanganye umma waWatanzania,
Mkuu G,
Mbona sasa unatoka kwenye hoja. Yeye katimiza wajibu wake kwa kutaja 5. Na wewe itisha mkutano leo uongezee wengine kwenye hiyo orodha. Kwani umezuiliwa. Anataja watu ambao ana ushahidi wa kutosha ndo maana hana wasi wasi hata wakienda mahakamani. Naona tunaanza porojo za kupotosha mjadala. Yeye ameonesha mfano na mtu mwingine aje basi ataje wengine. Lazima anazo sababu za kufanya hivyo. Ziwe za wazi au zilizo jificha. La muhimu kwetu ni kumpongeza na kujadili nini kinatakiwa kufuata baada ya hapa.
1. Katika statement yake amesema kuwa mafisadi wakubwa wanaoimaliza Tanzania hawazidi kumi.
2. Na yeye akaamua kuwataja watano ambao amewaita 'mafisadi papa' -
1. Rostam Aziz, 2. Tonil Somaiya, 3. Yusuf Manji, 4. Subash Patel na 5. Jeetu Patel.
Amesema hawa wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na mbaya zaidi fesha hizo wamezihamishia nje ya nchi.