Yussuf Makamba amwinda Reginald Mengi, yeye awataja mafisadi Papa rasmi!

We may have different opinions kuhusu Mengi na hatujui ana nia gani hasa lakini kwa hili tumpongeze kwa ujasiri wake wa kuweza kuhitisha press conference na kuwataja watu. Hii peke yake ina legal implications. Ukiangalia magazeti mengine ya leo wame elezea Mengi alichosema lakini hawa kuandika majina ya mafisadi kwa kuogopa kushtakiwa. Lets see what move hawa waliotajwa na Mengi watafanya.

Bravo...watu wanafikiria Mengi kutaja watu majina hadharani ni sawa na wao kutaja majina ya wachezaji wa Liverpool wakiwa vijiweni.
 
Hao mafisadi kawaanika vipi? Kamtaja nani? Kipi kipya alichosema? Mbona tunaridhika kirahisi hivi? Hamna substance katika alichoongea bali posturing tu.

Amandla........

Kipya ni mtu wa personality kusimama na kuwataja kwa majina wafisadi papa, na kuwahusisha moja kwa moja na umaskini wa watanzania, lakini kuu kuliko yote ni kuwataadharisha kuwa tusipokuwa makini na hawa watu nchi yetu itayumbishwa vibaya huko mbeleni.
 
Baada ya Mengi kutoa "bomu" nadhani itakuwa si vibaya kuuliza how clean is he?

Kuna watu wanadai kuwa tangu aikose KILIMANJARO HOTEL kwa Al Bawadi Mengi hakanyagi pale...na mbaya zaidi ugomvi wake na Yusuph Manji ni kutokana na kukosa yale Magodown ya NSSF sasa hivi ile statement yake ya jana usiku ni premption ya Objective kubwa zaidi... si vibaya kumjadili na yeye kujua kama ni safi au la

Nadhani itakuwa si vibaya tukamkoma nyani GILADI kwa JF style....bila kuogopa wala nini. Naamini kuwa tuko huru kumjadili bila woga wowote.
 
Anaonyesha wazi kuwa anatetea maslahi binafsi ,anataka kuteka vyanzo vyote vya utajiri na kubaki peke yake ili aendeshe wakubwa wa serikali kama wenzake ambao wanamwendesha puta Kikwete na serikali yake ,naona Mengi hapa nae anaonyesha tamaa ya kufikia stage hiyo ,he is the one from his face reading utaona alipo.

135449.jpg
 
Mimi najua ni MSAFI maana hana kashfa mpaka ninavyoandika. wewe wajua lipi?
 
kitu kingine ambacho inatupasa kuelewa ni kuwa hakuna rafiki mkubwa wa bwana Mengi kama JK (kwa wasiofahamu habari ndo hiyo), hawa jamaa wako close sana, na bwana Mengi back-up yake kubwa ni JK, uchungu alionao bwana Mengi ni kuona kampeni za chinichini ambazo Rostam at el wanazifanya ili kumwondoa Mkwere madarakani 2010, kwa hiyo anawalipua kwa lengo la kuwapoteza kwenye muelekeo wao kwa niaba ya JK, kwa sababu Mkwere awezi kabisa kukohoa mbele ya Rostam na Genge lake
 
kama umenisoma vema ni kwamba namuoan mengi kama msanii tu.....kila mwenye akili ya kawaida anajua kabisa hao aliowataja sio mapapa kama alivyosema papa ni JK mwenyewe na yeye anampa shavu JK kuwa yu msafi...

Imagine kwenye press na angetangaza 'rais wa nchi Kikwete' ndio fisadi namba moja nchini, nini kingefuatia next? Hata speech isingeisha kabla majasusi (polisi) hawajamzoa! Mimi nafikiri in a way amesema hivyo indirectly maana hawa wote aliowataja ndio wanaoifadhili CCM inayoongozwa na Kikwete. Ukitaka kumtukana mtu mwelezee usimwambie directly lile tusi mtaishia kupigana na hasa kama unajua jamaa ana msuli kukushinda!
 
wewe nahisi ni mmoja wa mafisadi ndo maana unatka wakumbatiwe.mengi kama mtanzania ameona hali halisi ya watanzania wengi wanavyoteseka kwa umaskini uliokidhiri ulotokana na wachache kina Rostam anawapasulia ukweli wewe unawatetea?Watanzania wengi wanakushangaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!11
 
Anaweza asiwe msafi yeye binafsi lakini hilo haliondoi ukweli kwamba wale wote aliowataja ni MAFISADI wakubwa!
 
Hatuna hata pa kuanzia kuuchukua mzigo aliotuonyesha mengi, tutaendelea kuwachambua tuuuuuu, na kumchuza mengi weeeee

Au kuna wazo?

Tanzania yenyewe ndio hii hakuna sheria inayoeleweka,
watekelezaji wenyewe wa sheria, mikono iko nyuma kwa fedha wanazopewa kila siku wakitaka kusafiri, nasikia wanapewa hela ya shoping na kina Tanil, sasa watasema nini masikini??
hadi nawaonea huruma,
Vibaraka wamejaa tele njaa zinawasumbua, wanajipendekeza kwa hao mapapa wenyewe,

Kama kikwete mwenyewe, alipokea hela ya kuendesha huu mkutano juzi wa vijana ccm toka kwa mmoja wao, unategemea nini??
Imagine, MKUTANO MKUU WA VIJANA CCM UMEFADHILIWA NA WASHUKIWA!!
CCM itatokea wapi na huyo jk wake?
Kama hawa tunaowategemea huwa wanalia shida kila siku na njaa zetu za kiswahili zisizoisha kwa hao mapapa, hadi nasikia wametenga bajeti kwa ajili ya njaa za wanasiasa, unadhani kuna tunakoenda kweli???
 
kitu kingine ambacho inatupasa kuelewa ni kuwa hakuna rafiki mkubwa wa bwana Mengi kama JK (kwa wasiofahamu habari ndo hiyo), hawa jamaa wako close sana, na bwana Mengi back-up yake kubwa ni JK, uchungu alionao bwana Mengi ni kuona kampeni za chinichini ambazo Rostam at el wanazifanya ili kumwondoa Mkwere madarakani 2010, kwa hiyo anawalipua kwa lengo la kuwapoteza kwenye muelekeo wao kwa niaba ya JK, kwa sababu Mkwere awezi kabisa kukohoa mbele ya Rostam na Genge lake

Naona kama hiyo ni kumpa credit isyomstahili mkwere! JK hana hata chembe ya kupinga ufisadi ndani yake. Haya mashambulizi ya Mengi in a way yanam-attack JK directly maana ndio kazi aliyotakiwa yeye JK kufanya. Lakini sema Mengi anaifanya kiutu uzima, kwa kumtanguliza kwenye speech kwamba JK anaongoza mapambano dhidi ya mafisadi. Na kwa sababu anapenda sifa JK akisikia hivyo hawezi kupinga, unaona imeshapelekea watu kumpa credit kwamba ni mpango wake na Mengi! Sijapata kumsikia popote JK akikiri hilo mbele ya wananchi, hivyo sina sababu ya kuamini kwamba anafanya lolote kwenye hiyo ajenda.
 
Baada ya Mengi kutoa "bomu" nadhani itakuwa si vibaya kuuliza how clean is he?

Kuna watu wanadai kuwa tangu aikose KILIMANJARO HOTEL kwa Al Bawadi Mengi hakanyagi pale...na mbaya zaidi ugomvi wake na Yusuph Manji ni kutokana na kukosa yale Magodown ya NSSF sasa hivi ile statement yake ya jana usiku ni premption ya Objective kubwa zaidi... si vibaya kumjadili na yeye kujua kama ni safi au la

Nadhani itakuwa si vibaya tukamkoma nyani GILADI kwa JF style....bila kuogopa wala nini. Naamini kuwa tuko huru kumjadili bila woga wowote.

Leo ndio maana siku muafaka ya kujadili iwapo Mengi ni fisadi au sio fisadi??!!
 
mengi ningemuona hero kama angeweza kutamka kuwa JK,mkapa na watendaji wakuu wao ndio fisadi namba moja.....maana tujiulize hio mikataba hawa akina jetu walisaini wakiwa na nani? kama sio hawa mengi anawaita wasafi......

....mikataba wameandaa serikali wakaitana na akina jetu wakainishana ila leo hii wengine wawe wasafi wengine ati mafisadi.......

.....alafu huyu mengi mbona hasemi mafisadi wakina chenge,mramba yeye kakomaa na hawa wafanya biashara tu....unafikiri mie mwananchi sitakuwa na machaka labda ana wivu wa kibiashara?

hao ni wadogowadogo jamani unaambiw Rostam na manji bado wanakula hela walizochota babu zao hawajaanza hata za baba zao acha zao wenyewe, EL,JK na wengine wameiga kwa hawa walimu. sasa tu deal na walimu kwanza tukiingia kwa wanafunzi mchezo umeisha, tukianza na wanafunzi wata recruit wanafunzi wengine
 
EL sio papa la ufisadi ni kibaraka tu wa mafisadi, hakuna fisadi papa anayetumwa, huwa wanatuma. EL kwa kutumwa tu na RA hakumfanyi kuwa fisadi papa, ingawa ni fisadi.
Sawa kabisa, alichokifanya Mengi ni kuwataja wale wanao ratibu Ufisadi katika kiwango cha juu kabisa hata kuyumbisha nchi na watu wake.MAPAPA.
Tukiwaweza hawa, waliobaki ni takataka za kufagia tuu.
 
Mimi nafikiri GT umepotoka au unataka kutuhamisha kwenye hoja iliyo jamvini, ishu ya kuzungumzia hapa si usafi wa Mengi bali ni utaratibu ambao serikali (vyombo vya dola) inaweza kuuchukua katika kuwezesha kupatikana kwa ushahidi kutoka kwa Mengi kuthibitisha tuhuma zake ili hao "mafisadi" waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na si kuanza kurushiana mpira ooh nani msafi ooh huyu vipi. Otherwise tutarudi kulekule kwenye "miafrika ndivyo ilivyo"

Tuhuma zimetolewa ni juu ya vyombo husika kufuatilia uhalali wa tuhuma for further action or else wahusika waliotajwa wamfungulie kesi, hapo ndipo tutajua lipi embe na ipi ndimu!!
 
Wallah JK anakua kutumia remote control. Mwenyewe kakaa kimya anatazama jama wanavyosuguana na kila mmoja anazidi kujisogeza kwake
 
Anaonyesha wazi kuwa anatetea maslahi binafsi ,anataka kuteka vyanzo vyote vya utajiri na kubaki peke yake ili aendeshe wakubwa wa serikali kama wenzake ambao wanamwendesha puta Kikwete na serikali yake ,naona Mengi hapa nae anaonyesha tamaa ya kufikia stage hiyo ,he is the one from his face reading utaona alipo.

135449.jpg

Nchi hii hata ufanye zuri gani wasema ovyo watakuwepo tu. Hao wote watano waliotajwa tunawajua wote ni mafisadi wkubwa wameimaliza nchi, ubinafsi gani unauzungumzia eti kuwa unaonekana usoni? Kwani mtu hata akiwa tajiri vipi (hata wewe) kama ni kwa nguvu zako halali kuna anayekukataza? Shida yetu ni wale wanatuibia. Please dont waste my time on this, Mwiba!
 
Wallah JK anakua kutumia remote control. Mwenyewe kakaa kimya anatazama jama wanavyosuguana na kila mmoja anazidi kujisogeza kwake

Sio kazi rais hiyo. Kazi yake ni kuwa on control saa zote na kudhihirishia umma hilo, tena local control.
 
Back
Top Bottom