BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Makamba amwinda Mengi
- Ahoji safari za mikoani
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
HUKU kukiwa na shinikizo la kutaka kumuondoa katika nafasi yake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, mwanasiasa huyo machachari, ametajwa sasa kumfuatilia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.
Makamba ameelezwa kupendekeza ndani ya vikao vya chama hicho kuchunguzwa kwa uhusiano wa Mengi na wanasiasa waandamizi wa CCM wakiwamo wabunge, wengi wao wakiwa ni wale wanaofahamika kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi.
Habari za ndani ya vikao vya juu vya CCM vilivyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na baadaye mjini Dodoma, zinaeleza kwamba Makamba alitoa hoja hiyo katika vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM na katika Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho tawala.
Wakati Makamba akiwasilisha hoja hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mmoja wa wageni wazito walioshiriki sherehe za miaka 75 ya kuzaliwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Mtera, John Malecela, mahali ambapo anaelezwa kusifia juhudi za wabunge wanaopinga ufisadi.
Miongoni mwa wabunge ambao Makamba anahisi wanaivuruga CCM wakiungwa mkono na Mengi ni pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ambaye pamoja na kupongezwa na Kikwete kupata zawadi ya mwanamke shujaa, alikuwa mmoja wa washiriki wa sherehe ya kuzaliwa mumewe mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Makamba anadaiwa kuhoji sababu ya Mengi kuingilia mambo ya CCM kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa wa ndani ya chama hicho, hali ambayo Katibu Mkuu huyo wa CCM anaielezea ndani ya vikao kama inaashiria hatari kwa chama hicho siku za usoni.
Hatua ya Makamba kumgusa Mengi katika vikao rasmi vya chama, vimeelezwa kuwa sehemu ya mkakati maalumu wa kupunguza kasi kubwa ya mfanyabiashara huyo kuonekana akishirikiana na baadhi ya wabunge katika baadhi ya shughuli mbalimbali za kijamii, huku wakibainisha wazi kumuunga mkono Rais Kikwete.
Ingawa haijawekwa bayana lengo hasa la mapendekezo ya Makamba ni kuhoji pia hatua ya hivi karibuni ya Mengi kutoa misaada ya fedha kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii kujiinua kiuchumi katika baadhi ya majimbo ya wabunge mbalimbali wa CCM bila kuyahusisha makao makuu ya chama hicho.
Mengi pia amekuwa mstari wa mbele katika vita ya ufisadi, vita ambayo inaungwa mkono na baadhi ya wabunge wa CCM akiwamo Anne Kilango - Malecela, ambaye hivi karibuni alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri na Serikali ya Marekani, kupitia ubalozi wake nchini.
Hata hivyo, habari zinaeleza kwamba hatua hiyo ya Makamba ni mkakati wa kujihami ama kulipiza kisasi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakiwamo wabunge wanaopinga ufisadi ambao wamekuwa wakitaka kiongozi huyo kuondolewa katika nafasi yake kutokana na kushindwa kukisaidia chama hicho.
Tayari Makamba alitengwa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini, ambako CCM ilishinda baada ya kuelezwa kwamba kiongozi huyo wa CCM alikuwa chanzo cha chama hicho kushindwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime.
Imefahamika kwamba sasa hata uchaguzi mdogo wa jimbo la Busanda, Makamba hatoshiriki kikamilifu, kukitolewa sababu kwamba ana majukumu mengi ya kitaifa na sababu nyingine za kiafya. CCM wanatarajiwa kumteua Lolesia Bukwimba, kuwania ubunge jimbo la Busanda.
Hayo yakiendelea, huko Mbeya, hali si shwari ndani ya chama hicho baada ya kuwapo mtafaruku miongono mwa viongozi wa CCM katika wilaya hiyo.
Katika moja ya matoleo yake, Raia Mwema ilikuwa na makala yenye kuelezea tahadhari iliyotolewa na wananchi wilayani Kyela kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mwenendo wa kisiasa wilayani humo, sasa imedhihiri kwamba kilio cha wananchi wale kilikuwa ni cha kweli na kilipaswa kufanyiwa kazi na si kupuuzwa kama ilivyojidhihirisha.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilayani Kyela sasa wamefikia hatua inayoipeleka wilaya hiyo kwenye machafuko makubwa zaidi, kwani kitendo cha makatibu kata wanne wa Chama hicho kuwavamia viongozi wao wa Kamati ya Maadili ya Wilaya hiyo na kuwapiga wakitumia mateke na ngumi, kinazidi kuongeza chumvi kwenye kidonda.
Makatibu kata hao wanne wanaodaiwa kuwatwanga viongozi wao ni pamoja na Josephat Mwakajinga kutoka kata ya Kajunjumele, Grayson Mwaikambo wa kata ya Kyela mjini, Alex Mwaisombwa wa kata ya Lusungo na Ipyana Mwangunga ambaye ni Katibu Mwenezi wa kata ya Makwale
Hali ya kimazingira inaonyesha kuwa vurugu hizo zilimlenga zaidi Katibu wa Chama hicho wilayani Kyela, Maria Mwambanga ambaye kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, inaelezwa kuwa wanataka kumuondoa kwa madai kuwa yuko upande wa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Harrison Mwakyembe.
Pamoja na madai hayo kuna taarifa vile vile kuwa Katibu huyo hatakiwi na baadhi ya viongozi wa chama hicho wilayani humo kwa madai kuwa hashindi ofisini na muda mwingi amekuwa akiutumia jijini Mbeya, hivyo kuunda genge la kumuondoa kwa nguvu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kyela, Japheth Mwakasumi anaelezea kushangazwa kwake na hatua ya makatibu kata hao kumvamia na kumpiga Mtendaji Mkuu wa Chama wilayani humo kwa madai yasiyo na kichwa wala miguu.
Dhamira yao wanataka mtu anayepokea mawazo yao, hapo ndipo ninaposhindwa kuwaelewa kwani si unayaleta kwenye vikao, ni wazi kuwa there is someone behind, maana miongoni mwa madai yao ni kwamba Katibu ni mtu wa Mbunge, kwa kweli siwaelewi, anaelezea kwa masikitiko Mwenyekiti huyo katika mahojiano maalumu na Raia Mwema.
Akizungumzia hali ya Katibu wake anasema sio nzuri na kwamba anaendelea na matibabu ikiwemo kupigwa picha.
Wee unafanya mchezo midume mizima inamshambulia mwanamke, hapana tumefika pabaya kama siasa zenyewe ndio hizi za majungu yasiyo na kichwa wala miguu halafu mnamshambulia mwamamke asiye na hatia, anazidi kushangaa Mwenyekiti huyo.
Aidha akizungumzia kinachoendelea ndani ya Chama hicho, Mwakasumi alisema kuwa Kamati ya Siasa ya Wilaya itaketi kesho Alhamis kulijadili suala hilo na kutoa maamuzi.
Hata hivyo, duru za ndani ya chama hicho wilayani humo zinabaisha kwamba vurugu hizo zilizosababisha Katibu huyo wa Wilaya kuumizwa vibaya, zinafadhiliwa na mmoja wa madiwani wilayani humo na kiongozi wa moja ya jumuiya za chama hicho mkoani Mbeya.
Ni wazi kwamba kwa taarifa hizo ni kwamba kuna kila dalili ya kuwepo kwa kambi mbili zenye mielekeo tofauti ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani.
Katika mahojiano na baadhi ya viongozi wa juu wa Chama hicho katika Wilaya ya Kyela pamoja na mkoani, wanazihusisha vurugu hizo moja kwa moja na harakati za kampeni za uchaguzi ujao mwakani na kwamba mbinu inayotumiwa na wafanya vurugu hao katika kukabiliana na Mbunge aliyepo haitofautiani na ile iliyotumika katika uchaguzi uliopita, kumtenganisha na uongozi wa juu wa chama hicho wilayani humo.
Katika mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, viongozi wa juu wa wilaya wa Chama hicho hawakumtaka kabisa Mbunge wa sasa na badala yake waliegemea kwa Mbunge aliyekuwapo madarakani wakati ule, na hata Dk. Mwakyembe aliposhinda kwenye mchujo huo bado viongozi hao hawakumpa ushirikiano hivyo kutegemea zaidi nguvu ya wapiga kura ambako hadi sasa ndiko nguvu yake iliko.
Inaelezwa kuwa vurugu hizo za Jumamosi iliyopita zilitokea kwenye Kikao cha Kamati Maadili kilichoitishwa maalumu na kwa ajili ya kuwahoji baadhi ya makatibu kata, pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya hiyo, Visk Mahenge wanaotuhumiwa kuhusiana na vurugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama ya Wilaya hiyo Machi 31, mwaka huu.
Pamoja na tuhuma hiyo, Mwenyekiti wa Chama hicho Wilayani Kyela, Mwakasumi anaitaja tuhuma nyingine iliyokuwa wahojiwe makatibu hao ni kwa baadhi ya makatibu hao kudaiwa kuendesha kikao chenye mlengo wa kampeni za uchaguzi mwakani huku kikihusishwa na utoaji posho nje ya taratibu za chama hicho.
Wakizungumzia suala hilo la kampeni viongozi wa Chama hicho mkoani hapa walibaisha kuwa wanaelewa kuwepo kwa kampeni zinazoendelea chini kwa chini, lakini wakasisitiza haziwezi zikahalalishwa kuudharau uongozi uliopo madarakani kwani kwa kufanya hivyo ni kuruhusu vurugu na matumizi ya rushwa.
Mmoja wa viongozi wa chama hicho mkoani hapa alifikia hatua ya kusema, Kinachonisikitisha ni hatua ya baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kuchochea vurugu ndani ya chama wilayani Kyela, Katibu anatekeleza wajibu wake kwa kufuata kanuni na taratibu za chama zilizopo, hawezi kutoshirikiana na Mbunge wa jimbo la wilaya yake, hata kama mbunge ni kutoka chama cha upinzani bado angeshirikiana naye, ila tu asingeruhusiwa (mbunge wa upinzani) kuingia kwenye vikao vyetu vya chama, lengo ni maendeleo kwa wananchi na sio watu binafsi.
Moja ya matatizo yanayozikabili siasa za mkoa wa Mbeya ni kwa baadhi ya wanasiasa kuendelea kuishi katika ndoto za mtandao uliomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, wakiamini kwamba bado unazo nguvu zile zile za mwaka 2006 kurudi nyuma.
Pamoja Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Nawab Mulla kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akielezea kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu kwa waliosababisha vurugu hizo iwapo suala hilo litatuliwa nje ya mahakama, baadhi ya wanachama wameelezea kupingana naye katika hilo kwa maelezo kuwa Chama hicho siku hizi hakina uwezo huo wa kuwajibishana.
Wanautaja mgogoro ulioibuka kwenye kikao kimoja cha CCM Mkoa ambapo kiongozi mwanamke alitaka kumvalisha sidiria kiongozi mwenzake mwanaume kwa madai kwamba anaingilia mambo ya wanawake, lakini duru za kisiasa mkoani humo zikidai kuwa sababu hasa ni kutoungwa mkono kwenye kampeni zake kuwania uongozi wa juu wa chama hicho kwenye moja ya jumuiya zake.
Au ndio maana na Mengi leo kaamua kuwalipua mafisadi? Maana nasikia kwenye Press conference yake amewataja akina Rostam, Jeetu, Somaiya na Manji kuwa ndio mafisadi wakuu nchini
Invisible said:Alichokiongea Mengi:
``Our country is currently facing a huge problem of corruption and is troubled by the fact that the people involved in acts of corruption do not what to be touched.
The resolve by our President, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, to fight corruption and all other evils has shaken these people and they are now determined more than ever to combat all the people who are supporting the President in stopping further plunder of our country`s resources.
[ICODE]Tanzanians should know that people who are being accused of being corrupt in our country do not exceed ten, and out of the ten, five are being accused of being notoriously corrupt -
corrupt sharks
[/ICODE].
``These are: Rostam Aziz, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeethu Patel and Subash Patel.
These people are being accused of stealing billions of public money, and to make this worse, the billions have been transferred out of the country.
``These notoriously corrupt people are involved in almost all scandals that have happened in our country, including those concerning Richmond, EPA, Dowans, Army helicopters and vehicles, the Presidential Jet, Radar, NSSF, PSPF, National Lottery etc, etc.
``The great efforts of His Excellency the President to hasten economic development and better living for every Tanzanian are weakened by the horrendous theft of national resources.
A great majority of Tanzanians still face extreme poverty; they are unable to determine where the one meal a day is going to come from.
To make things worse, where a Tanzanian with better means provides assistance to lessen hardship within the society and to eradicate poverty, these people involved in corruption allege that such assistance has political agenda. They want Tanzanians to starve or die as a result of other problems.
``It seems that their aim now is to cause national havoc; it will not be surprising to learn that these people support what is behind DECI while Tanzanians remain chasing Pastors instead of asking themselves the real source of the havoc.
``These notoriously corrupt people are not only stealing our national resources; they are also stealing our precious time.
Instead of using our time for economic development we are using most of it to combat corruption.
``Our efforts have failed to even cause a dent; instead these corrupt people have been hardened in their determination.
They have established newspapers that are abusive and treat Tanzanians with contempt.
``They have created a scenario where the thief chases and attacks the person from whom he has stolen.
Even as Tanzanians continue to cry foul, the notoriously corrupt people continue to use their ill-obtained wealth to influence the granting of big contracts to them often in different names.
``Millions of Tanzanians are combating corruption, but there are a few who have come forward vehemently and are known by their names.
The notoriously corrupt people have been heard to say that they will annihilate these vehement combatants.
``The notoriously corrupt people should know that if the combatants are harmed in any way in this country or any other country, they will be answerable to the people of Tanzania.
``We Tanzanians must now ask ourselves - what gives these notoriously corrupt people the audacity to treat Tanzanians with contempt?
I would like to conclude by saying that all corrupt people and especially those who are being accused of notorious corruption must be dealt with conclusively, otherwise they will rock the stability of our nation. We must realise that we have now reached the stage when we must say enough is enough.
Mengi ataja mafisadi papa 2009-04-24
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataja watu watano wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi mkubwa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka iwezekanavyo ili kuinusuru nchi kuyumbishwa nao. Watu hao, ambao Mengi alisema kwamba wanatuhumiwa kuwa ni mafisadi papa, ni pamoja na:
Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam .
Aliwataja wengine, kuwa ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi. `
Hawa wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na baya zaidi fedha hizo zimehamishiwa nje ya nchi,
alisema Mengi alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za IPP Limited, jijini Dar es Salaam jana na kuongeza:
`…mafisadi wote na hasa wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa ni lazima washughulikiwe, la sivyo wataiyumbisha na kuitingisha nchi yetu.Ni lazima Watanzania tuone kwamba sasa tumefika mahali pa kusema imetosha.`` Alisema watu hao ni kati ya watuhumiwa wasiozidi kumi wanaotuhumiwa kwa ufisadi mkubwa nchini na kuongeza kuwa wanahusishwa na karibu kila kashfa kubwa nchini, ikiwamo inayohusu kampuni hewa ya Richmond, ambayo ilitiliana saini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mkataba tata wa kufua umeme wa dharura.
Kashfa nyingine, ambayo watu hao wanahusishwa nayo, alisema inahusu Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambamo imethibitika kuchotwa Sh. bilioni 133 kwa njia za kifisadi na ile inayohusu kampuni ya Dowans Tanzania Limited, iliyorithi mkataba tata wa Richmond.
Nyingine, inahusu ununuzi wa helikopta na magari ya jeshi, ndege ya Rais, rada, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Bahati Nasibu ya Taifa na Mradi wa Makaa ya Mawe wa Mchuchuma. Alisema jitihada kubwa za Rais Jakaya Kikwete za kuleta maendeleo na maisha bora kwa kila Mtanzania, zimekuwa zikidhoofishwa na wizi mkubwa wa rasilimali za taifa, huku Watanzania wengi wakiandamwa na umaskini mkubwa, ikiwamo kutojua hata mlo mmoja kwa siku utatoka wapi. ``Chakusikitisha ni kwamba, pale Mtanzania mwema mwenye uwezo anaposaidia jamii kuondokana na umaskini, mafisadi wanapiga kelele kuwa misaada ya aina hiyo ina agenda.
Wanapinga, wanataka Watanzania wafe kwa njaa na matatizo mengine,`
alisema Mengi. Alisema inavyoonekana, nia ya watu hao ni kutaka kuvuruga nchi na kwamba, si ajabu wakaunga mkono matatizo yanayotokana na kampuni ya Development Enterpreneurship Community (Deci) iliyokuwa ikichezesha mchezo wa upatu na Watanzania wakabaki wakifukuzana na wachungaji bila kujiuliza ni kina nani hasa wanachochea vurugu hizo. Mengi alisema ‘mafisadi papa, hawawaibii tu Watanzania rasilimali, bali wanawaibia pia muda.
Badala ya kutumia muda katika shughuli za maendeleo tunajikuta tukitumia muda mwingi kupambana nao, na hawatingishiki. Badala yake wanatumia fedha walizotuibia kuanzisha magazeti ya kujenga kiburi cha kutudharau, kututukana na kutunyanyasa. Inakuwa kesi ya mwizi kumkimbiza na kumpiga aliyeibiwa,` alisema Mengi. Alisema hata hivi sasa, mafisadi papa wanaendelea kutumia uwezo wao wa kiuchumi uliotokana na wizi wa rasilimali za nchi kushawishi na kupata miradi mikubwa mikubwa kwa kutumia majina tofauti tofauti, huku wakipuuza kabisa kelele za wananchi kuhusu ufisadi huo. Mengi alisema Watanzania wanaolia na ufisadi, ni mamilioni wakiongozwa na Rais Kikwete, lakini wapo wachache waliojitokeza na wanajulikana kwa majina.
Alisema zipo habari kwamba, wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa, wamedhamiria kuwatokomeza kabisa wanaopiga vita ufisadi wanaojulikana kwa majina. Kutokana na habari hizo, alisema:
Mafisadi papa ni lazima wajue kwamba iwapo wapambanaji hao wa ufisadi watadhuriwa kwa njia yoyote hapa nchini au nje ya nchi, watawajibishwa na wananchi wa Tanzania.
Aliongeza: ``Ni lazima Watanzania sasa tujiulize, hivi hawa mafisadi wanapata wapiujasiri wa majigambo, dharau na nguvu za kututukana na kutunyanyasa?`
` Awali, Mengi alisema nia njema ya Rais Kikwete ya kupambana na mafisadi na aina zote za uovu zimewashtua mafisadi na sasa wamecharuka na wanapambana na watu wote wanaomsaidia kupambana nao kuwazuia wasiendelee kuitafuna nchi. Rostam amekuwa akituhumiwa kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, inayodaiwa kuchota Sh. bilioni 40 kwenye EPA, tuhuma ambazo amekuwa akizikanusha. Shubash Patel anakabiliwa na sakata la kuchukua ardhi ya wanakijiji kwa njia za hila eneo ambalo kuna madini ya chuma, katika eneo la Mchuchuma, Iringa.
Tanil Somaiya anatajwa kuwa ni mshirika kwa mtuhumiwa wa ununuzi wa rada, Shailesh Prapji Vithlani ambaye tayari ana kesi katika mahakama ya Kisutu alikoshitakiwa bila kuwepo nchini. Katika sakata la rada, serikali ililizwa kiasi kikubwa cha fedha huku zaidi ya Dola milioni 12 zikiingia katika mifuko ya waliofanikisha ununuzi huo. Somaiya na Vithlani walikuwa wanamiliki kampuni nchini iliyohusika na kashfa hiyo.
Jeetu Patel kwa sasa ana kesi za EPA katika mahakama ya Kisutu zikihusu kampuni zake tano tofauti ambazo zilihusika kuchota mabilioni ya fedha kati ya Sh bilioni 133 zilizochotwa kifisadi.
SOURCE: Nipashe
Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi
Mbunge wa Igunga na Mweka hazina wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, hatimaye amejibu rasmi madai mazito yaliyotolewa na Reginald Mengi kuhusu "mafisadi papa". Tamko hilo rasmi linapatikana katika ukurasa wa 6 wa gazeti la 'The Citizen' la leo Alhamisi, tarehe 30 Aprili 2009...
www.jamiiforums.com
Tamko la Serikali dhidi ya Reginald Mengi na Rostam Aziz
Wakuu JF. Nimesoma kwenye mtandao kuwa Tariki Azizi wa TZ leo angetoa tamko la Serikali Kuhusu Mengi. Tafadhali mlioko nyumbani tupasheni habari kama kalitoa na amesema nini. ===== Rostam Na Mengi: Serikali Yatoa Tamko MONDAY, MAY 11, 2009 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh...
www.jamiiforums.com
Videos: