Yussuf Makamba amwinda Reginald Mengi, yeye awataja mafisadi Papa rasmi!

Kwa kweli i support Reginald Mengi but he failed to mention KIWIRA na mapapa wengine kama EL, NK na MKAPA. Ila Mkapa kama mkapa i feel sorry for him. Anajuta kuufahamu uraisi.
 
Nasubiri kuona mwanzo wa drama hii maana kweli Mengi alikuwa akizungumza kwa uhuru kabisa! Namuunga mkono.

Binafsi nimekuwa nikishindwa kuwa na imani na wafanyabiashara wa Kihindi. Imani niliyoijenga naamini niko sahihi kwamba Biashara za Wahindi nchini zimejaa ufisadi. Wana makundi ya kifisadi na kwa kiasi kikubwa wanasiasa wema wanashindwa kulisema ili wasiitwe wabaguzi.

Ninachokiona ni kwamba Wahindi wanastawi sana ki-biashara wanapokuwa ktk nchi ambazo zina viongozi laini na wenye njaa kama hii yetu na nchi zenye mifumo ya rushwa za wazi wazi. Nchi ambayo Waziri anapigiwa simu na kijana wa ki-hindi na kufunga safari kwenda kuchukuwa chochote. Aibu Tupu!!

Issue hiyo ya waziri kufuata chocolate imenichekesha na kuniumiza sana, mimi binafsi naijua moja ya mke na watoto wa waziri kwenda kwa kijana mhindi kuomba hela ya matumizi ya shule na nyumbani...ni waziri ambaye hadi sasa anatumikia serikali ya awamu ya nne.. alafu leo hii tupo busy kumdiscuss nia ya mengi..mengi kasema hali halisi na yale ambayo wengi wetu tunadiscuss kwenye mabar,jf au majumbani...hamna udini wala racism hapa..mengi kasema yaliyo na ukweli mwingi kama na agenda nyingine hilo lifunguliwe thread yake lakini hapa im with him 1000%
 
Kwa kweli i support Reginald Mengi but he failed to mention KIWIRA na mapapa wengine kama EL, NK na MKAPA. Ila Mkapa kama mkapa i feel sorry for him. Anajuta kuufahamu uraisi.

Watanzania kweli tunatia huruma...hivi mnamlipa Mengi kiasi gani cha kukusanya ushahidi na kuja kuwataja hawa mafisadi hadharani..!!
 
- Hapa hakuna kawaida, majina yametajwa rasmi sasa ni wajibu wetu kuchunguza wameiba nini, wapi? Wameshirikiana na nani?

- Tusiwe wazembe wa kusubiri Mengi atufanyie kila kitu, ndio maana tunakwama, maana tufanyiwe kila kitu mpaka kufikiriwa, that is pathetic!

FMES!

Mkuu tatizo hapo Mengi hakusema mepya yote yameshaandikwa zaidi ya aliyoyasema na wengine wana kesi ,sasa hana jipya ni kutumia mgongo wa wengine kuelemeza hasira zake,na zaidi kujikosha kwa serikali ,he is the one.
Kwa nini kama anausongo na ufisadi asiikemee serikali kwa kushindwa kuwachukulia hatua za haraka ,Mengi anapigana na kivuli chake na utajiri alionao ndio unaomfanya awe anajikanyaga kwa kuogopa kushughulikiwa ,si umeona amejibamiza kwa Kikwete ,kwa ufupi amechagua upande ,nasema Mengi ametangaza rasmi upande aliopo wa timu kati ya timu za mafisadi.
 
mengi ningemuona hero kama angeweza kutamka kuwa JK,mkapa na watendaji wakuu wao ndio fisadi namba moja....
Si amesema mafisadi papa hawazidi kumi???? na amewataja watano???? Labda hao waliosalia, ambao hajawataja (Maana inaonekana anawafahamu) ndio hawa
 
Si amesema mafisadi papa hawazidi kumi???? na amewataja watano???? Labda hao waliosalia, ambao hajawataja (Maana inaonekana anawafahamu) ndio hawa

Hapo ni muongo mafisadi ni wengi sana Chama kizima cha CCM ni mafisadi kuanzia Mwenyekiti mpaka balozi ,waondoke madarakani kuiongoza Serikali ya Tanzania na WaTanzania kwa ujumla.
 
Hapo ni muongo mafisadi ni wengi sana Chama kizima cha CCM ni mafisadi kuanzia Mwenyekiti mpaka balozi ,waondoke madarakani kuiongoza Serikali ya Tanzania na WaTanzania kwa ujumla.

nadhani yeye hajasema mafisadi, amesema 'mafisadi papa' akimaanisha mafisadi wakubwa kuliko. Kama ni mafisadi tu kila mtu anajua kuwa wapo wengi
 
Kwa mwelekeo wa hii thread inaonekana hakuna anayepinga list ya mengi..wengi wana question agenda, wengine wanalalamika hajataja weusi, wengine wanalalamika for the sake of it..mengi asingesema aliyosema bila ushaidi...

nadhani sasa narudi kuwa mwangaliaji..coz kuna watu humu ambao hata kukutana na manji, rostam or the patels first hand ni bado zaidi ya kupishana nao mahakamani au njiani..kutana na hawa watu dubai au london ndo utawajua vizuri na jinsi wanavyojigamba kwamba wana nchi mikononi mwao..hao mafisadi weusi wote wanapewa allowance tuu kama watoto kwa baba yao.
back to being a watcher!
2010 tufanye mabadiliko
 
Msiende mbali kama Mengi alikuwa na ubavu wa kutaja mapapa ya ufisadi mbona EL amemwacha kaogopa nini kumtaja? Msiumize kichwa Mengi ni mfanya biashara na hawa wafanya biashara kuna mgongano wa kimaslahi bila shaka.
 
Mkuu tatizo hapo Mengi hakusema mepya yote yameshaandikwa zaidi ya aliyoyasema na wengine wana kesi ,sasa hana jipya ni kutumia mgongo wa wengine kuelemeza hasira zake,na zaidi kujikosha kwa serikali ,he is the one.

Kwa nini kama anausongo na ufisadi asiikemee serikali kwa kushindwa kuwachukulia hatua za haraka ,Mengi anapigana na kivuli chake na utajiri alionao ndio unaomfanya awe anajikanyaga kwa kuogopa kushughulikiwa ,si umeona amejibamiza kwa Kikwete ,kwa ufupi amechagua upande ,nasema Mengi ametangaza rasmi upande aliopo wa timu kati ya timu za mafisadi.

Unajuaje iwapo Mengi yeye anaona hatua ambazo serikali imechukua so far zinamepewa haraka inayostahili kwa mujibu wa taratibu zetu na ushaidi ulipo??? Au sasa unataka kutuambia yeye kwa sababu ni Mengi basi hana haki ya kuwa na mawazo huru..!!??

Mwiba, ulitaka Mengi aitishe press conf kuongelea mawazo yako au mawazo yake yeye mengi?
 
Msiende mbali kama Mengi alikuwa na ubavu wa kutaja mapapa ya ufisadi mbona EL amemwacha kaogopa nini kumtaja? Msiumize kichwa Mengi ni mfanya biashara na hawa wafanya biashara kuna mgongano wa kimaslahi bila shaka.

Ndio hapo niliposema anapiga mchakamchaka pale walipo Mwakiembe na Rostam ,maslahi tu hakuna lingine.
 
Siyo siri kwamba hawa jamaa ni mafisadi wakubwa.

Lakini tunajua vilevile kwamba BIFU la Mzee Mengi na wahindi ni la siku nyingi kutokana na maslahi ya kibishara. Amekuwa akipambana nao kila mahala na kuna wakati aliwafuata kwenye ufadhili wa mpira akajaribu kuwatoa kilabu ya Yanga na baada ya kuwaondoa huko hakuendelea na ufadhili wake.

Mafisadi wako wengi, Mengi kaanza nasi tumalizie. Sasa swali ni moja; serikali haielekei kuchukua hatua yoyote, wananchi tufanyeje? watu wa Madagascar wameonyesha njia, je, sisi tunaweza?

Moyo tuliouona kwenye 'kupanada na kuvuna' huko DECI ukitumika katika vita hii tutawashinda, lakini ...
 
kwikwikwi mengi hana jipya......ati anampa shavu jk......hao aliowataja jk ndio anawatumia kuchota mijihela.....

.....nani mshika mihuri? mwenye dhamana hao ni wafanya biashara tu wamepata baraka zoote toka kwa jk.......

mhh anachokifanya anajua sana atawagombanisha wao kwa wao, kikwete sasa anawajibu wa kuwashulikia as wameshatajwahadharani na kupewa misifa kebekebe na anataka kuendelea kubaki kwenye kiti chake mwaka kesho, kama alitumia ile sentensi ya kwama wakikupa hela pokea kula ila usitimize matakwa yao atapona ila kama alikula ili atimize matakwa yao watamalizana wenyewe kwa wenyewe, Mengi kataja anaowajua mafisadi Papa labda mwingine atueleze kama kikwete ni kadagaa au kaperege hahahaha!
 
mimi kwa mtazamo wangu sidhani kwamba mengi amefanya hilo la kuwataja hao mafisadi kwa maslahi ya taifa, nadhani amefanya hivyo kwa 1)maslahi binafsi (kuelekea ikulu), 2) ugomvi binafsi na wahusika
hoja yangu ni hii. 1)hawa waliotajwa na mengi kuwa ni mafisadi kila m2 analijua hilo, kulishakuwa na thread hapa jamii forum ya kuwamsion hao mafisadi na wanajamii tuliwalist haohao, pili bwana Slaa pia alishawamension hao pia pale mwembe yanga kwa hiyo alichokifanya mengi sio kigeni kabisa na sioni kama ni kwa maslahi ya taifa bali ni binafsi tu
2) kwa nini asubiri apelekwe mahakamani ili akawalipue huko, kama kweli ni mzalendo wa kweli na ana huruma na wanachi wa tanzania na uwezo anao, basi ingekuwa busara kwake kwenda mahakamani na kufungua keshi ya kuwashtaki hao jamaa (kama sheria hipo?) kwa sababu amesema ushahidi anao, lakini hilo la kusema hao mafisadi ndio waende mahakamani hilo linaonyesha kama nilivyosema hapo juu ni labda chuki binafsi au anatafuta political popularity
 
Rostam mwaka jana kasimama na kuwasema akina Mengi pamoja na Mtikila je hiyo nayo inahitaji moral authority? Mengi naye leo kaongea kamsema Rostam je hiyo nayo inahitaji moral authority gani? Mwakyembe naye si alikuja kwa waandishi na yeye akamsema Rostam wakati yeye mwenyewe anahisa kwenye kampuni ya umeme je alikuwa na moyo authority, Je Mtikila alivyokuja kumsema Rostam wakati amevuta milioni tatu toka kwake je alikuwa na moral authority gani? Ndiyo maana nakwambia issue ni nini kimeongelewa na mtu siyo nani kaongea. Sasa Mengi anamsifia JK ambaye mimi binafsi namwona ni zao la ufisadi sasa kwa nini nisimtilie shaka?

Hivi Mkodoleaje, unamtetea nani???
 
We may have different opinions kuhusu Mengi na hatujui ana nia gani hasa lakini kwa hili tumpongeze kwa ujasiri wake wa kuweza kuhitisha press conference na kuwataja watu. Hii peke yake ina legal implications. Ukiangalia magazeti mengine ya leo wame elezea Mengi alichosema lakini hawa kuandika majina ya mafisadi kwa kuogopa kushtakiwa. Lets see what move hawa waliotajwa na Mengi watafanya.
 
Msiende mbali kama Mengi alikuwa na ubavu wa kutaja mapapa ya ufisadi mbona EL amemwacha kaogopa nini kumtaja? Msiumize kichwa Mengi ni mfanya biashara na hawa wafanya biashara kuna mgongano wa kimaslahi bila shaka.

EL sio papa la ufisadi ni kibaraka tu wa mafisadi, hakuna fisadi papa anayetumwa, huwa wanatuma. EL kwa kutumwa tu na RA hakumfanyi kuwa fisadi papa, ingawa ni fisadi.
 
Kwa kweli i support Reginald Mengi but he failed to mention KIWIRA na mapapa wengine kama EL, NK na MKAPA. Ila Mkapa kama mkapa i feel sorry for him. Anajuta kuufahamu uraisi.

nop nop ametaja top 5, EL yupo kwenye Top 10, Mkapa kwenye top 10, kwanini kama umemsikiliza vizuri amesema wengine wamehusika kwenye kashfa ya Richmond,Dowans, ndege za jeshi, na radar...mpaka akutafunie jamani looh
 
Back
Top Bottom