kukukakara
JF-Expert Member
- Jul 31, 2012
- 496
- 164
Hiyo nukuu ya Nyerere mnaitafsiri kinyume-nyume, soma na hii.....
"Rais wa JMT anaweza kutoka chama chochote lakini rais bora atatoka ccm". By J.K.Nyerere.
kwani Lowasa katoka UDP au
Hiyo nukuu ya Nyerere mnaitafsiri kinyume-nyume, soma na hii.....
"Rais wa JMT anaweza kutoka chama chochote lakini rais bora atatoka ccm". By J.K.Nyerere.
Mzee Mwanakijiji siasa ya mwaka huu ni mpya kabisa, hakuna mtu angeweza kutabiri tu walau miezi miwili iliyopita kwamba Dr.slaa atakuwa sio kitu ndani ya chadema! na sasa hakuna anayeweza kutabiri mwezi ujao nini kitafuatia kwenye siasa za Tanzania.
Mkuu hadi muda huu wanairudia.
Hiyo nukuu ya Nyerere mnaitafsiri kinyume-nyume, soma na hii.....
"Rais wa JMT anaweza kutoka chama chochote lakini rais bora atatoka ccm". By J.K.Nyerere.
Tuweni wa kweli, kama sio wanachama wa CCM kuja UKAWA tunataka tupate wapi wananchama? Tuwazae? Hapana, ni lazima wawe ni wanachama toka vyama vingine! Au at least basi ni Washabiki wa chama fulani ndio wanaojenga chama!!!
Kwanini mwana CCM akitoka CCM kuja upinzani ndio inakua nongwa? Naamini Chadema kuna Katiba ambayo wataiheshimu.... ni kweli wengi wametoka CCM lakini tulitaka watoke wapi kama sio CCM? S ndi lengo letu? waujue ukweli ili kweli iwaweke huru? Kuna kosa? Nadhani tusiwe wabinafsi kupita kiasi
Kauli yake tu ya kula mihogo eti kisa kiongozi inamuondolea credibility muongo na nzushi. Toka lini sifa ya kiongozi ikawa kula vibaya na umaskini eti ndo sifa. Huyu ni mtu mwenye roho ya kinyongo,hana moyo wa kusamehe na kujiona msafi.
Mkewe kamshinda ndo Watanzania,eti kuita wengine makapi kwani yeye alitokea wapi. Na picha za mitandaoni zimemuumbua
Wametuweza kwa lipi? Kiukweli sioni lolote ambalo CCM wanaweza kujivunia.
Watu wanaelewa sasa hivi tofauti na zamani.
Kipimo ni tukio la jana, nilidhani litaleta mtikisiko mkubwa ila hakuna chochote cha kutisha.
Mbinu zote za CCM zimekosa matokeo mazuri mwaka huu.
Lete na nukuu za Nyerere kumhusu lowassa tuone kama hujajikimbia.
Mzee Mwanakijiji siasa ya mwaka huu ni mpya kabisa, hakuna mtu angeweza kutabiri tu walau miezi miwili iliyopita kwamba Dr.slaa atakuwa sio kitu ndani ya chadema! na sasa hakuna anayeweza kutabiri mwezi ujao nini kitafuatia kwenye siasa za Tanzania.
Chakula kwa Fikra Zako: CCM wamefanikiwa jambo moja ambalo sikulidhania linaweza kufanikiwa miezi michache tu nyuma; wamewachagulia wapinzani mgombea wao wa Urais, timu yake na mashabiki wake na kulazimisha upinzani (hasa CHADEMA) kubadilisha wagombea wake na kuwapokea kwa furaha waliotolewa kama zawadi na CCM kwao.
Kama kweli - alivyodai Lissu - kuwa CHADEMA walishampitisha Dr. Slaa kuwa mgombea wao wa Urais kwenye kikao cha Kamati Kuu basi kumuondoa yeye (aliyekuwa anahofiwa sana na CCM labda kuliko mtu mwingine yeyote miaka hii mitano) ni mkakati ambao umefanikiwa kupitiliza. Leo wana CDM (sijui kama ni wengi au la) wamejipanga kushangilia mapinduzi ya kimkakati waliyofanyiwa na CCM wakiamini kuwa wamepewa zawadi.
Leo mtu aliyekijenga chama na kupigwa pamoja nao anaonekana hana mpango ati ni kikwazo cha "mabadiliko" wakati mtu ambaye hajawahi kuwa na rekodi ya mabadiliko au hata kuutetea upinzani anahusishwa na mabadiliko! Jeraha hili la upinzani haliwezi kuponeshwa na wale wale waliosibabishwa; tuliambiwa "akili ndogo zisitawale akili kubwa"... sasa siyo tu akili ndogo zinatawala akili kubwa; akili kubwa zenyewe hazijijui kuwa ziliwahi hata kuwa akili kubwa!
Vyovyote vile itakavyokuwa CCM itaendelea kutawala ama kupitia Magufuli au kupitia Lowassa. Hili wapo ambao hawataki kuamini ndilo limetokea huku wenyewe wakiamini kuwa wanapigania "mabadiliko". Kuigeuza upande mmoja wa shilingi ukasema "umebadilisha" ni kweli; lakini hujabadilisha shilingi!
Hapa CCM wametutia kidole...
Cha macho!.. hata hatuoni tena.
MMM