Yehova witness kutimuliwa kwa kukataza wanafunzi kuimba wimbo wa taifa!

......Hili dhehebu nalo lina lake jambo,wimbo wa taifa hauna ubaya wowote maana ni maombi tosha kwa muumba wetu kuibariki nchi yetu. Hao wazungu wanataka wanafunzi waimbe wimbo gani? Hawa wazungu nao wanataka kutawala kila kitu sasa.
 
Kwanza wimbo wa taifa wenyewe uko discriminatory.

Unaanza kwa kusema "Mungu ibariki Tanzania"

Sasa na sisi tusioamini mungu si tutaona huu wimbo ni kichaa kitupu, tukisema hatutaki kuimba on this ground utatulazimisha?

Ndivyo tunavyoishi tunalazimishana tu as far as dini concern. Chukulia mfano Waislamu wanavyolazimishwa kupunzika siku ya Jumapili ili wengine wakaabudu Mungu wao, huku wakilazimishwa kufanyakazi siku ya Ijumaa na kushindwa kwenda kumuabudu Mungu wao. Pengine nanyi kina Kingunge ndio hivyo mnalazimishwa kumtaja Mungu hata kule Bungeni.
 
Samahani sana lakini naomba nijuulishwe. KUSUJUDI ni kitendo gani?
Ama katika dini yangu ya kiislamu kusujudi ni kupiga magoti na kuerka kipaji cha uso aridhini, jee wenzetu katika dini yenu kusujudi ni huko au la?

Basically kuabudu, kutukuza.

Interpretations nyingine zinaweka haya mambo ya nyimbo za taifa na pledges za allegiance katika kapu moja na kusujudu.

Kwa mfano, wewe kama muislam kweli unaambiwa uimbe wimbo mmoja na wakristo, wimbo unaanza kwa kusema "Mungu Ibariki Afrika" lakini hausemi mungu gani (waislam wengine wakimtaja mungu ni lazima waseme S.A.W, Sasa huyu mungu asiyeeleweka huyu aliye katika wimbo wa taifa mungu gani?

Wa Wakristo? Wa Waislam? Wa watu wa dini za asili?

Na kama wengine dini zao haziruhusu kumtajataja mungu itakuwaje? Kama wengine wanaona hizi ni jitihada za wanasiasa kumtumia mungu kufanikisha uporaji wao utasemaje?

Kitu muhimu ni kuwapa watu uhuru, waamue wanavyotaka, kama wanataka kuimba wimbo wanaimba, kama hawataki poa.

Kulazimisha ni ubeberu , ni ukoloni, tunabadilisha rangi tu ya wakoloni, tumewatoa weupe tunawaleta weusi.
 
Si tunajidai hatuna religious persecution?

As long as hakuna evil intention, kila mtu afanye kwa mujibu wa dini yake.

Anayeabudu mti poa, anayekataa kuimba wimbo poa.

Kwani wasipoimba atakufa mtu?

Ukoloni tu!

Kiranga basi isiwe wewe wa kuwaambia Watanzania wenzako na badala yake wawe wao? Mbona watu wanappinga ushoga na si hawahawa walioubariki?
 
You are not making yourself clear.

Nisiwe mimi wa kuwaambia Watanzania nini, na kwa nini?
 
Mbona mnawaonea hao jehovah...? Tanga wanafunzi wa kiislam hukatazwa kuimba wimbo wa taifa hata kutoa mchango wa mwenge kisa eti wimbo wa taifa ni wakikristo na mwenge eti dhumuni lake ni kueneza ukristo....hao ni wanafunzi wa advance sio primary....najua baadhi yao watakkuwepo humu...tunawasubiri mjibu hizi tuhuma....

Well Mahiza ameshasema kuwa huo ni uhaini basi sasa umeshaelewa kama hapo mwanzo ulikuwa hujaelerwa. Peleka mbele ili wachukuliwe hatuwa kama una ushahidi wa kutosha.
Ama hili la Mwenge hili si la Katiba na ni hiari hivyo achana nalo, hata hivyo hata huo ukiristo hausemi kuwa tuabudie moto.
 
Uhaini ni code word ya kumfunga mtu pale mnapokosa kitu cha msingi cha kumfunga, ndiyo mambo ya Patriot Act hayo.
 
Tuheshimiane,

Patakuwa hapakaliki hapa, ohooo.Mwanaume kuambiwa ana bwana tusi.

Taifa? Taifa liko wapi? Hao illuminati wanaowachezeeni katika mchezo wa redio mjione mna kitu kinaitwa taifa ndio washawateka akili?

Siku hizi hamna taifa, na hii si Tanzania tu, mpaka Marekani, mambo ni mwendo wa ma Corporatocracy tu, ma Halliburton yashachukua kila kitu, wewe unabaki na concept za Westphalia za 1600 huko!

Punguza Munkari sote tuna BWANA au ulisema kuwa wewe ni mpagani vile? Lakini kuabudu ni kufuata maelekezo ya Bwana na iwapo maelekezo ya Mzungu yanasimama badala yake kwa asie Mungu basi bila shaka huyu Bwana wake atakuwa hao Wazungu.
Ama kwa Utaifa hili halina mjadala na ndio maana unapoteza wakati wako sasa kujadili mustakabali wa hilo unalolikanusha kuwa si Taifa.
 
Si tunajidai hatuna religious persecution?

As long as hakuna evil intention, kila mtu afanye kwa mujibu wa dini yake.

Anayeabudu mti poa, anayekataa kuimba wimbo poa.

Kwani wasipoimba atakufa mtu?

Ukoloni tu!

Ndugu serikali inahaki ya kusimamia sheria zake inavyotakikana. Hakuna uhuru usio na mipaka kama ndivyo basi kusingekua na rule of order wala governance. To every right there is a responsibility.

Sasa basi sheria ya nchi inasemaje kuhusu ibaada/imani. without direct quotation; kila mtu ana uhuru wa kuabudu nakuamini chochote ili mradi kwa kufanya hivyo havunji sheria za nchi. Je kuheshimu na kuimba wimbo wa Taifa si responsibility ya kila mwananchi? Tukumbuke kuwa ukiruhusu kila mtu afanye analotaka kwenye taifa ambalo lina watu wenye imani tofauti huku serikali yenyewe haiamini katika chochote isipokua katiba je hakutakua na migongano? Then kwa sisi iko clear tunaongozwa na katiba na katiba ndo iko juu ya wote kwaajili ya wote. Kama hivi ndivyo basi ni kosa kosa kwa mtu au kikundi cha watu kuenda kinyume na kitu kinachotuongoza. Kama Jehova witness wakiruhusiwa je wale wanaoamini katika kutoa kafara wenzao wakatazwe kwa misingi ipi? So kila uhuru unampaka wake na hii mipaka ndo makubaliano ya pamoja-Katiba. Kama haikidhi haja basi tuna hoja na tudai kuirekebisha short of that ni kuifuata penda tusipende na kazi ya serikali ndo kama ilivyo fanya-kusimamia katiba.
 
Punguza Munkari sote tuna BWANA au ulisema kuwa wewe ni mpagani vile? Lakini kuabudu ni kufuata maelekezo ya Bwana na iwapo maelekezo ya Mzungu yanasimama badala yake kwa asie Mungu basi bila shaka huyu Bwana wake atakuwa hao Wazungu.
Ama kwa Utaifa hili halina mjadala na ndio maana unapoteza wakati wako sasa kujadili mustakabali wa hilo unalolikanusha kuwa si Taifa.

Sote tuna bwana kakwambia nani? Tulikaa siku moja tukakubaliana hivyo?

Collectivism tu kama Borgs!
 
......Hili dhehebu nalo lina lake jambo,wimbo wa taifa hauna ubaya wowote maana ni maombi tosha kwa muumba wetu kuibariki nchi yetu. Hao wazungu wanataka wanafunzi waimbe wimbo gani? Hawa wazungu nao wanataka kutawala kila kitu sasa.

Sasa wao wanakwambia hauendani na dini yao. Kama wimbo wa taifa hauna ubaya wowote, kuacha kuimba nako hakuna ubaya wowote, mkwaacha kuna mtu atakufa?
 
Basically kuabudu, kutukuza.

Interpretations nyingine zinaweka haya mambo ya nyimbo za taifa na pledges za allegiance katika kapu moja na kusujudu.

Kwa mfano, wewe kama muislam kweli unaambiwa uimbe wimbo mmoja na wakristo, wimbo unaanza kwa kusema "Mungu Ibariki Afrika" lakini hausemi mungu gani (waislam wengine wakimtaja mungu ni lazima waseme S.A.W, Sasa huyu mungu asiyeeleweka huyu aliye katika wimbo wa taifa mungu gani?

Wa Wakristo? Wa Waislam? Wa watu wa dini za asili?

Na kama wengine dini zao haziruhusu kumtajataja mungu itakuwaje? Kama wengine wanaona hizi ni jitihada za wanasiasa kumtumia mungu kufanikisha uporaji wao utasemaje?

Kitu muhimu ni kuwapa watu uhuru, waamue wanavyotaka, kama wanataka kuimba wimbo wanaimba, kama hawataki poa.

Kulazimisha ni ubeberu , ni ukoloni, tunabadilisha rangi tu ya wakoloni, tumewatoa weupe tunawaleta weusi.

Naanza kukubali kuwa humjuwi Mungu na hivyo unahitaji kupewa majibu.
Kabla ya yote UISLAMU (naibold makusudi ili kutafautisha uislamu kama dini na Waislamu kama binaadamu) unaamini kuwa yuko Mungu mmoja nae huyo haonekani ( nafikiri utawatafautisha wale waungu wanaoonekana) na hivyo Mungu Baba si mwengine bali ni huyohuyo.
La pili Uislamu haukatazi kuishi kijirani na Mkristo bali unakataza kushirikiana katika yale ambayo uislamu unakataza. Kwa bahati mbaya mambo mengi ambayo wakristo wanafanya ni kinyume na maamrisho ya uislamu hivyo waislamu wanapokataa kushirikiana na Wenzao wakiristo katika baadhi ya mambo inakuwa sababu ndiyo hiyo na wala sio kwa kuwa personality ni ukiristo.
Ama kuhusu msimamo wako na Utaifa well huo ndio msimamo wako na una haki lakini iwapo wengi tunatambuwa Utaifa basi moral ya Kilimwengu ya wengi wana haki lazima iwepo.
 
Wewe hujui kusoma au vipi?

Umeona signature hiyo? Mimi siamini kama mungu yupo, mungu ni hoax na mythology, sasa nitajuaje kitu ambacho hakipo other than in the conext of mythology.

"La pili Uislamu haukatazi kuishi kijirani na Mkristo bali unakataza kushirikiana katika yale ambayo uislamu unakataza."

Uislamu haujasema there is no god but Allah and Muhammad is his prophet, sasa kwa nini mtu akishangaa huyu mungu anayeombwa na wote kwa pamoja ni mungu gani? ni Allah, Yehovah au Jua?

Wengi wana haki, wengi wakikubali kuchinja ni haki, au kumlala mama ni haki itageuka kuwa haki?

Pleeease!
 
Uhaini ni code word ya kumfunga mtu pale mnapokosa kitu cha msingi cha kumfunga, ndiyo mambo ya Patriot Act hayo.

Bahati mbaya Kimaumbile binaadamu tunaishi katika matakwa ya waliotuzidi iwe Muumba, Watawala au hata mazingira.
 
Muumba hayupo, watawala watakutawala ukiwaachia tu na mazingira inategemea unaongelea mazingira gani, mengine yanatawalika.

Kwa hiyo point yako ume i stretch, mwanadamu anaweza kuya control mazingira yake na kuyatawala kwa kiasi kikubwa, ni uvivu, woga na uzembe unaofanya watu wasiweze kufanya hivi na kumsingizia mungu ambaye hata hayupo.
 
Sasa wao wanakwambia hauendani na dini yao. Kama wimbo wa taifa hauna ubaya wowote, kuacha kuimba nako hakuna ubaya wowote, mkwaacha kuna mtu atakufa?

Dini hazina uamuzi katika kuendesha nchi labda uende Saudi Arabia ambako nako tafsiri na maamuzi yanafanywa na binaadamu.
 
Muumba hayupo, watawala watakutawala ukiwaachia tu na mazingira inategemea unaongelea mazingira gani, mengine yanatawalika.

Kwa hiyo point yako ume i stretch, mwanadamu anaweza kuya control mazingira yake na kuyatawala kwa kiasi kikubwa, ni uvivu, woga na uzembe unaofanya watu wasiweze kufanya hivi na kumsingizia mungu ambaye hata hayupo.

Nafikiri lipo tatizo hapa. Mungu hayupo sawa sasa tunabishania nini hapa ? Hawa unaowatetea wanafanya nini hapa Tanzania?
Unajuwa kama hujaamuwa akilini mwako hii thread inazungumzia nini basi bora utulie.
 
Back
Top Bottom