Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Mwanzoni mwa juma hili Bunge la JMT liliingia kwenye mjadala ambao uliishia kuokoa usalama wa ajira za Walimu waliodhaniwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka za ajira zao kufuatia kuimbisha na kuchezesha wanafunzi wimbo maarufu wa haniii... (honey) unaotawala hisia za makundi yote ya rika wakiwemo watoto.
Klipu hiyo ya Walimu hao na wanafunzi ilisambaa (viral) kwenye mitandao-jamii kiasi cha kuzua hisia na maswali yaliyopelekea watumishi hao kuchukuliwa hatua na mamlaka zao za nidhamu na ajira; hatua ambazo Bunge liliona zipitiwe upya kwa namna ya kuzisahihisha. Nalipongeza Bunge kwa umakini huo.
Hoja zangu:-
1. Kuzuia wimbo wa haniii... mashuleni na kuuacha uendelee sokoni kumeokoa nini?
2. Kuzuia wimbo wa haniii... mashuleni ni kuzuia pia dada wa kazi asimchezeshe mtoto arudipo nyumbani toka shule?
3. Kuzuia wimbo wa haniii... mashuleni na labda nyumbani na kuuacha uendelee kupigwa kwenye majumba ya starehe yaliyojazana kwenye makazi ya watu wanakoishi watoto hao ndiyo tumeokoa nini?
4. Kuzuia wimbo wa haniii... mashuleni na kuuacha uendelee kupigwa kwenye majumba ya starehe yaliyojazana jirani na mashule wanakosoma watoto hao ndiyo tumeokoa nini?
5. Kuzuia wimbo wa haniii... mashuleni na kuuacha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya usafiri wa umma wanavyotumia wanafunzi kwenda mashuleni, kurudi majumbani na kwenda maeneo mengine ya miji wanayoishi ndiyo tumeokoa nini?
6. Nadhani wimbo huo ambao sina hakika kama ulipata ithibati ya BASATA ungeondolewa sokoni kabisa kama ambavyo Bunge la JMT liliwahi kuondoa wimbo ule maarufu wa "Nibebeshe ukimwi nihangaike nao" kwamba ulikuwa unahujumu jitihada za taifa za kupambana na maambukizi ya zimwi hilo.
Nchi inapenda muziki na ni tasnia iliyoajiri wengi sana lakini somo la muziki kwenye mtaala ni kama halipo asilani na BASATA wako kimya tu wasitafute kuchagiza muziki kufufuliwa kwenye mitaala ya kufundishia mashuleni ili tuzalishe wanamuziki wenye weledi.
Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, BASATA ifumuliwe na kusukwa upya kama siyo kuwajibishwa. Walimu wameonewa bure tu.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app