Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 213
- 1,726
Kwa ufupi:
- Mzee Malecela amehakikishiwa nafasi na Lusinde katupwa nje vibaya sana na kudaiwa kuwa alidanganya suala la Elimu yake, Lusinde kakasirika sana kwa hali hii na huenda akachukua hatua ambayo haikutarajiwa ndani ya CCM, si tetesi hizi!
- Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba amewapigia simu mkoa wa Manyara akitaka kura za maoni huko Simanjiro ambako alishinda Ole Sendeka zirudiwe (nia ni kumng'oa Sendeka) lakini wao wakamwuliza mbona hakukuwa na malalamiko hata chembe wala kasoro yoyote? Wana CCM kule Simanjiro wanashangaa kule Bumbuli ambako Januari aligombea hawajarudia japo kulikuwa na malalamiko kadha wa kadha lakini wao wanalazimishwa kurudia, wanaonekana kukasirishwa na maamuzi ya kulazimishwa.