Masha amkimbia Wenje, amvaa Ngeleja, Arfi aibukia CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
TUESDAY, JULY 21, 2015

agombea.jpg


Makada wa Chadema walioomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Ukonga wakiwa katika mkutano wa uchaguzi kwenye Ukumbi wa Santiago Msongola, Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory

In Summary


  • Aidha, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Arfi ambaye hivi karibuni alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho, amejiunga na CCM na amechukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Nsimbo, Katavi.

By Waandishi Wetu, MwananchiDar/mikoani. Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya nchi, Lawrence Masha amemkwepa hasimu wake kisiasa, Ezekia Wenje katika Jimbo la Nyamagana, Mwanza na kwenda kugombea ubunge Sengerema ambako atavaana na mbunge anayemaliza muda wake, William Ngeleja.

Aidha, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Arfi ambaye hivi karibuni alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho, amejiunga na CCM na amechukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Nsimbo, Katavi.

Masha amkwepa Wenje

Katika uchaguzi uliopita mwaka 2010, Masha aligombea kipindi cha pili katika Jimbo la Nyamagana (CCM), katika mpambano uliokuwa na ushindani mkali na kuangushwa na Wenje wa Chadema.

Awali, kabla ya uchaguzi huo, Masha akiwa waziri mwenye dhamana na mambo ya ndani, alimwekea pingamizi Wenje akidai hakuwa raia, lakini hoja hiyo haikumzuia mshindani wake, badala yake ilimwongezea kura za huruma hadi akaibuka mshindi.

Safari hii Masha amepima maji na kuamua kumvaa waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Ngeleja ambaye hivi karibuni alikuwa miongoni mwa wanaCCM 38 walioomba kuwania urais, lakini akaondolewa katika hatua za awali.

Alipoulizwa jana, Masha alisema amechukua fomu Sengerema kwa sababu ni nyumbani kwao, ndipo alikozaliwa na kukulia, hivyo ameamua kushirikiana nao kusukuma gurudumu la maendeleo.

"Nyamagana pia ni nyumbani, hivyo tutaendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo kwa kila jimbo. Sijafanya maridhiano yoyote ya kuachiana jimbo, lakini natumia haki yangu ya kugombea popote," alisema.

Hata hivyo, hata katika jimbo la Sengerema alikoomba kugombea hayuko salama kutokana na nguvu ya upinzani iliyopo kupitia Chadema ambacho nguvu yake ilidhihirika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba mwaka jana pale ilipochukua viti vyote katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Sengerema na maeneo mengine ya vijijini.

Mbali na Masha na Ngeleja, wengine waliojitokeza katika jimbo hilo kupitia CCM ni Anna Shija, George Rweyemamu, Philemon Tano, Dk Omari Sukari, Dk Angelina Samike, Jumanne Mabawa, Mussa Malima, Baraka Malebele, Joshua Shimiyu na Zablon Bugingo.

Arfi atimkia CCM

Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Averin Mushi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Arfi ambaye alikuwa Mbunge wa Mpanda Mjini, ameomba ubunge katika jimbo jipya la Nsimbo lililoko katika Wilaya ya Mlele.

Alisema hadi siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu hizo juzi, makada 23 wa CCM walijitokeza kuomba kuteuliwa kuwania ubunge katika majimbo manne ya uchaguzi yaliyoko Mkoa wa Katavi.

Aliwataja walioomba kuteuliwa kugombea ubunge katika Jimbo la Nsimbo kuwa ni Arfi, Shabir Hasanari "Dallah', Richard Mbogo, Manamba David na Mapesa Frank.

Walioomba kugombea ubunge katika Jimbo la Katavi ni Isaack Kamwelwe, Shafi Mpenda, Maganga Kampala na Oscar Albano.

Katika jimbo jipya la Kavuu ni Zumba Emmanuel, Mselem Said na Prudenciana Kikwembe.

Jimbo la Mpanda Mjini waliochukua na kurejesha fomu ni Sebastian Kapufi, Galus Mgawe na Gabriel Mnyele na katika Jimbo la Mpanda Vijijini ni Moshi Kakoso, Abdallah Sumry, Willy Makufe, Elizabeth Sultan, Godfrey Nkuba, Rock Mgeju na Chifu Charles Malaki.

Bulaya ajipa siku mbili

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya amesema ndani ya saa 48 (kuanzia jana), atatangaza chama ambacho atahamia na kugombea ubunge.

"Ni kweli sigombei kupitia CCM, ila ndani ya siku mbili nitawaambieni chama ambacho nitatumia kugombea ubunge. Haya mambo ya vyama yapo tu na ni njia tu ya kupita, lakini lengo letu ni kuhakikisha tunaleta maendeleo kwa wananchi bungeni.

"Nilipokuwa CCM nilijitahidi kuleta maendeleo, lakini imefika wakati ambao nadhani nitaleta maendeleo zaidi kupitia chama kingine ambacho ndani ya siku mbili mtakijua," alisema.

Guninita ajitoa

Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita aliyekuwa ameomba kugombea ubunge katika Jimbo la Kilombero ametangaza kujitoa kabla ya kura ya maoni akidai ana shaka na mchakato unavyokwenda.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kilombero, Bakari Mfaume alisema: "Sijapata taarifa ya kujitoa, ndiyo kwanza nasikia kwako, sijapata malalamiko yoyote katika wagombea 20 nilionao kwenye wilaya yangu.

"Guninita alichukua fomu Julai 18 akajaza na kurudisha siku hiyohiyo kisha akaaga kwamba hatohudhuria kikao cha wagombea wote na kamati ya siasa ya wilaya kwa kuwa amepata dharura Dar, nilimkubalia kuwa angejiunga na wenzake kujinadi kwa wanachama katika kampeni za ndani, sasa sijui kimetokea nini," alisema Mfaume.

Guninita alisema amejitoa kwenye mchakato huo na kuamua kubaki kuwa mwanachama wa kawaida, licha ya kutumia Sh600,000 kwa ajili ya fomu na michango mingine ili kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuhofia mchakato huo hakusudii kujitoa kwenye chama hicho, badala yake atakuwa bega kwa bega na mgombea atakayepitishwa.

Wengine wanaogombea majimbo mbalimbali ni:

Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa, Abdul Zahoro, Muharami Mkenge, Salim Abed, Mbonde Mbonde, Mathew Yungwe, Maulid Mtulya, Fabian Said, Lekesani Mvule na Chacha Wambura.

Chalinze: Ridhiwan Kikwete, Iman Madega, Mbaraka Tamimu, Changwa Mkwezu, Omar Kabanga na Hamis Devile.

Kibaha Mjini: Silvestry Koka, Rugemalira Rutatina, Idd Majuto, Rashid Bagdela na Abdulaziz Jadi.

Kibaha Vijijini: Dk Ibrahim Msabaha, Hamoud Jumaa, Bureta Allen, Hussein Chuma, Janeth Munguatosha na Shomary Sangali.

Kahama Mjini: Jumanne Kishimba, Wilbert Nkuba, Deogratius Sazia, Deogratius Mpagama, Adam Ngalawa, Michael Bundala, John Nyenye, Andrew Masanje, Masubo Julius, Luhende Shija na Godwin Kitonka.

Ushetu: Elias Kwandikwa, Isaya Bukakie na Erhard Mlyasi.

Msalala: Ezekiel Maige, John Sukili, Emmanuel Kipole, Nicholaus Magangila, John Lufunga na Wakilala Mashara.

Geita Mjini: Ngara Kanyasu, Daffa Daffa, Dk Samweli Opulukwa, Jacob Mtalitinya, Paschal Malugu, Mathayo Melikiory, Dk Leonard Mugema, Regina Mikenzi, Evarist Nyororo, Juma Malunga na Chacha Mwita.

Geita Vijijini: Jivitius Sabatho, Ernest Mabina, Thoma Ntogwakulya, John Marco, Emmanuel Sherembi na Joseph Msukuma.

Busanda: Tumaini Magesa, Lolesia Bukwimba, Luchenche Mbatilo, Francis Kiganga, John Mhonzu, Sostenes Kulwa na Marko Malembeka.

Buchosa: Dk Charles Tizeba na Eston Malima.

Mbeya Mjini: Christopher Nyenyembe, Joseph Mbilinyi ‘Sugu' na Lazaro Mwankemwa.

Kyela: Bernard John, Babylon Mwakyambila, Lusekelo Mwasasumbe, Godfrey Mwakalukwa, Dickson Mwaipopo, Denis Maria, Claud Fungo, Bruno Lupondo, Michael Mwasanga, Clemency Kyando, Alinanuswe Mwalwange na Abraham Mwanyamaki.

Busokelo: Dk Stephen Kimondo, Ambakisye Mwakifwange, Asifiwe Mwakalobo, Isack Mwambona, Boniface Mwabukusi, Elias Mwakapimba, Simon Mwamaso na Elisha Mwambapa.

Rungwe: Deogratius Mwailenge, Ayubu Mwakasole, Nicodemas Ngwala, Ahobokile Mwaitenda, Sophia Mwakagenda, John Mwambigija, Barnaba Pomboma, Brown Mwaipasi, Yassin Mwakisole, Festo Mwaipaja, Christopher Kitweka, Richard Mbalase, Wilfredy Mwaipyana, Bertha Mwakasege, Daud Mwasanga na Yusuph Asukile.

Mbarali: Jidawaya Kazamoyo, Dickson Baragasi, Grace Mboka, Tazan Ndingo, Rajab Msingo, Liberatus Mwang'ombe na Ronilick Chami.

Lupa: Victor Kinyonga, Ernest Mwamengo, Philipo Mwakibingo, Enock Mageta, Emil Mwangwa, Sande Sanga, Moses Mwaifunga, Mohamed Hussein, Jamson Mwiligumo, Njelu Kasaka, George Mwaipungu na Peter Noah.

Mbozi: Eliud Msongole, Abraham Msyete, Solomon Kibona, Eliud Kibona, Zablon Nzunda, Abdul Nindi, Anastazia Nzowa, Happiness Kwilabya, Fannuel Mkisi, Furaha Mwazembe, Gift Kalinga, Pascal Haonga, Andrew Bukuku, Ambakisye Kabango, Stephen Mwakingili, Jerald Silwimba, Fadhil Shombe, Jonathan Mwashilindi, Fredy Haonga, Bob Mwampashe, Ostern Meru, Sophia Mwabenga, Mochael Mtafya, Mchungaji Wilhelm Mwakavanga, Seule Nzowa na Dickson Kibona.

Mbeya Vijijini: Moses Mwaigaga, Chance Mwaikambo, Franco Mwalutende, William Msokwa, Stephano Mwandiga, Frank Mwaisumbe, Elias Kwimba, Antony Mwaselela, Wila Jacob, John Mwamengo, Jeremiah Mwaweza, Adson Sheyo, Emmanuel Shonyela, Alimu Mwasile, Adam Zella, Nhungo Jisandu, Daud Mponzi na Cyprian Magulu.

Ileje: Nicolaus Mtindya, Emmanuel Mbuba, Emmanuel Msyani, Gwamaka Mbughi, Cosmas Sikinga, Leornad Fumbo, Joel Kajinga na Riziki Mbembela.

Songwe: Mpoki Mwankusye, Michael Nyilawila, John Mwaniwasa, Ofugan Wanga na Frank Mwakitalima.

Babati Vijijini: Omary Kwaang', Damas Nakey, Vrajlal Jituson, Hassan Kaniki, Vencent Naano, Faustine George, Mary Geai, Charles Ingi, Jamal Mukta, Valerian Margwe, Atanas Kijuu, Stephano Manda, Daniel Sulle, Laurent Tara, Ester Sarwat, Leonard Mao, Daniel Marko, Herman Sanka, Salum Shawishi. Christina Kembe, Ester Sarwat na Respikia Muna (viti maalumu).

Babati Mjini: Kisyeri Chambiri, Haines Darebe, Ally Msuya, Ally Sumary, Sulei Doita, Samo Samo, Cosmas Masauda, Ramadhan Slaa, Paulina Gekul na Gabriel Kimolo.

Hanang': Dk Mary Nagu, Dk Eliamani Sedoyeka, Peter Nyalandu, Deusdedit Mayomba, Derick Magoma, Nada Shauri, Cyiril Ako, Leonard Guti, Whilhelem Gidabudai, Dk Haite Samo na Rose Kamili anayegombea viti maalumu.

Mbulu Mjini: Zacharia Isaay, Peter Pareso, Andrew Aqweso na Juma Marmo.

Mbulu Vijijini: Fratley Gregory, Martha Umbulla, Malkiani Nari, Dk Isack Maleyeki na Simon Daffi.

Simanjiro: Christopher Ole Sendeka, Peter Toima, Simon Ndwala na James Ole Millya.

Kiteto: Benedict Ole Nangoro, Emmanuel Papien, Amina Mrisho, Joseph Mwaseba na Ally Lugendo.

Ukerewe: Sumbuko Chipanda, Osward Mwizalubi, Christopher Nyandiga, Deogratias Lyato, Dk Elias Misana, John Mkungu, Magesa Boniphace, Hezron Tungaraza, Dk Deusdedit Makalius, Marick Marupu, Laurent Munyu, Bigambo Mahendeka, Bandoma Kabulile, Gerald Robert na Emerciana Mkumbulo.

Bariadi: Andrew Chenge, Masanja Kadogosa, Cosmas Chenya na Joram Masanja.

Meatu: Donald Masanga, Oscar Paul, Romana Kitija na Salum Mbuzi.

Itilima: Daud Njalu, Masanja Ngangani, Dani Makanga, Kulwa Njanja na Hilu Kibilu.

Kisesa: Ruhaga Mpina

Maswa Mashariki: Michael Jilala, Mashimba Ndaki, Benjamin Tungu, Aron Mboje na Henry Nditi.

Maswa Magharibi: Jonathan Ngela, Stanslaus Nyongo, Ally Mtegwa, George Lugomelo, Edward Bunyongoli na George Nangale.

Busega: Dk Titus Kamani, Dk Rafael Chegeni, Bernard Kibese, Igo Shing'ombe, Dismas Shwea, Robert Nyanda, Nyangi Msemakweli na Josephat Mkwabi.

Njombe Kusini: Edward Mwalongo, Alfred Luvanda, Arnold Mtewele, Vitalis Konga, Mariano Mwanyigu, Romanus Mayemba, Deiniol Msemwa na Hassan Mkwawa.

Njombe Kaskazini: Laula Malekela, Emmanuel Nyagawa, Joram Hongoli, Lemah Hongoli, Osmund Malekela, Mussa Mgata, Gaston Kaduma, Avike Kyenga na Oscar Msigwa.

Ludewa: Deo Filikunjombe, Zephania Chaula na Kapteni Mstaafu Jacob Mpangala.

Makete: Dk Binilith Mahenge, Dk Noman Sigala, Lufunyo Kinda, Bonic Mhami na Fabian Mkingwa.

Wanging'ombe: Gerson Lwenge, Thomas Nyimbo, Yono Kevela, Kenned Mpumilwa, Malumbo Mangula, Abraham Chaula, Richard Magenge, Petro Dudange, Hoseana Lunogelo, Nobchard Msigwa, Eston Ngilangwa na Abel Badi.

Makambako: Deo Sanga na Alimwimike Sahwi.

Viti Maalumu Njombe: Pindi Chana, Neema Mgaya, Nebo Mwina, Rosemary Staki, Suzan Kolimba, Margaret Kyando na Erica Sanga.

Kilombero: Kanali mstaafu Harun Kondo, Vitus Lipagila na Abdullah Lyana, Oscar Mazengo, Japhet Mswaki, Paul Mfungahema, Abubakari Asenga na Abdul Mteketa.
 
Habari hii kwa sehemu naona ina mapungufu.

Hao wagombewa walitajwa hapo wote wanagombea kuteuliwa kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM au??
 
ni kweli nimegundua kitu .

Mkuu, habari imejaa taarifa za waliochukua au kutangaza nia kuwania ya kuteuliwa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya CCM.

Ila unaposoma unakutana na wafuasi pia wa CHADEMA humo: akina Sugu na wengineo. Msomaji asipokuwa makini kwa

aina hii ya uandishi, anaweza kupotoshwa....
 
Hivi watu wote waliojitokeza kugombea ubunge wakikusanywa awajazi uwanja wa taifa kweli kama wale madogo waliokuwa wakitafuta kazi ya uhamiaji.
 
Habari hii kwa sehemu naona ina mapungufu.

Hao wagombewa walitajwa hapo wote wanagombea kuteuliwa kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM au??

Hapana mkuu. Wengine ni kwa tiketi ya CHADEMA. Ila kiukweli wameiweka vibaya walipaswa kuainisha na vyama vyao ili kuepusha usumbusu kwa wasomaji.
 
Back
Top Bottom