Elections 2010 Yanayoendelea chinichini ndani ya CCM...

Kama Lusinde alidanganya suala la Elimu yake...hapo hakuna mjadala, atakua amejiaribia mwenyewe kwa kutokua mwadilifu.

Kama hilo ni tatizo basi sheria na taratibu za CCM zina macho. Mnakumbuka kesi ya Mh. Chitalilo yule Mbunge wa Buchosa? Alidai amemaliza F4 na amesoma mpaka Uganda. Polisi walipochunguza wakakuta kwamba huko Uganda wala hakusoma na hana hata cheti cha F4.

Bunge lilipoanza kwenye profile yake ilikuwa inaonyesha amemaliza na ana vyeti vya huko Katikamu Uganda. Baada ya INTERPOL kutoa taarifa kwamba Chitalilo hakusoma Uganda, ndipo profile yake ikabadilishwa na kuonyesha kwamba hakumaliza elimu ya sekondari hapa Tanzania wala Uganda.

DPP alipopelekewa ripoti ya INTERPOL akasema Chitalilo hana kesi ya kujibu na kwamba kwenye siasa kuna udanganyifu mwingi ambao hufanyika ikiwemo hata kutoa ahadi hewa.

Wakatokea wapiga kura wa Buchosa wakashitaki kama Independent Prosecutors, kesi ile ilitupwa nje. Baada ya kelele hizo kuzidi sana ndipo Dr. Tizeba alikuja kupewa post ya Ukuu wa Wilaya ya Sikonge ili angalau kupooza mambo.

Kwa hiyo nikiona hoja hiyo kwamba Lusinde alidanganya elimu yake, kwani wao hawakujua? Mbona anafanya kazi CCM, ina maana huwa wanatoa post bila kupitia vyeti na CV ya mtu anayepewa post? Haya ndio mambo ya Masauni kughushi umri halafu wanakuja kumtema baadaye.

Hii CCM ina vitu vya ajabu sana wakati mwingine. Watakutumia na wakishatimiza malengo yao then wanakutema au kama hawakutaki toka mwanzo watakutafutia vijisababu ili wakuteme.
 
Mengine hayajatimia tu? Twasubiri kwa hamu mkuu
Mkuu Mengine niliyaweka hapa:

CCM Mafia warudia uchaguzi...

Naona hii thread inaweza kuwa imewafanya CCM wabadili lengo, huenda wakaamua kumwachia Lusinde na wakamtafutia nafasi nyingine mzee Malecela kama ilivyokuwa kwa mzee Kingunge. Nimepata taarifa kuwa imewakera kuona habari hii imevuja kabla ya kufikia maamuzi rasmi.

Huko Mafia uchaguzi uliitishwa ghafla saa 8 mchana wa leo (kwa mida ya Tanzania) na mbunge aliyemaliza muda wake Shah analalamikia kitendo hicho ambacho kimekuja kufuatia maamuzi ya Katibu Mkuu mzee Makamba.
 
Shibuda hajaondoka CCM bado? Anangoja nini?

Mkuu huyu hafai hata kwa wapinzani? Si kila anayekataliwa chama kimoja anafaa kwa vyama vingine. Wengine ni mzigo tuu mkuu. Na chadema nawashauri pokeeni wanachama wanaohamia toka vyama vingine ila muwe makini kuwaweka sehemu nyeti, hasa kugombea. Wengine watimkia tu hasa wakati wa uchaguzi kumbe wanataka ujiko tu.

 
Shibuda hajaondoka CCM bado? Anangoja nini?
Shibuda alishatangaza RASMI kuwa kahamia CHADEMA, nadhani hata hapa JF iliandikwa... Labda kama mimi ndo nasahau ila kishahamia CHADEMA rasmi na akasema atakuja kuyasema yote ambayo yamemtokea ndani ya CCM
 
March on soldier.....huyu Makamba huyu...am glad he is not in the government now...abaki hukohuko CCM

Usiseme unafurahia hayupo serikalini - unakosea, kwani serikali hii inaendeshwa na CCM hiyohiyo ambako hukohuko Ma-rope yupo kama kiongozi, tena ngazi kubwa tu!
 
Mkuu hapa kuna swali la kujiuliza ni kwanini Malecela anaahidiwa nafasi, kama ameshindwa kwanini asibaki pembeni, kwani hawezi kutoa mchango akiwa pembeni? Kama ameonekana hakubaliki jimboni kwake (bila kujali sababu) ambako wanamjua vizuri zaidi kuliko sehemu nyingine za Tanzania, atakubalika vipi kwenye sehemu nyingine? Au ndio dhana ya kufa na uongozi. Mbona watu wa calibre yake kana kima Cleopa David Msuya, Joseph Sinde Warioba na Salima Ahmed Salim, wamekaa pembeni kimya? Ina maana wao hawana umuhimu au hawana uwezo?

This is so sick. Tunamheshimu mzee wetu, lakini uongozi hautakiwa kuwa a tool for apeasement. Watu kama kina Mzee Malecela, Msekwa,Kingunges wanfaa kufuata nyao za kina Warioba na Msuya. Too much.

Labda hajajitayarisha kisawasawa kuhusu 'retirement'! Yaani, atafanya nini aki'pumzishwa'?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom