Lumecha orijino
Member
- Apr 3, 2011
- 27
- 13
Wapendwa wana JF, mie ni mgeni na hii ni post yangu ya kwanza. Naomba msaada wenu wa mawazo ili ni-epuke hii adha ninayoipata.
Ni hivi wapendwa: Nilikuwa na girl friend wangu toka 2007 but tuliishi wote kwa makubaliano bila kufunga ndoa hadi mwaka jana mwezi wa 8, ndipo nikaona ni vema sasa tufunge ndoa. Lakin kilichochelewesha ni kuwa alikuwa anasoma chuo na sasa ni mwalimu wa sekondari.
Kifupi sijakaa naye saana coz 2008 nilenda nje ya nchi na nitarudi kusetle home mwakani, tatizo ni kuwa mke wangu hawapendi ndugu zangu hata mmoja,sisi tupo sita na mimi ni wa pili lkn hawapendi ndugu zangu: sio wifi zake wala shemeji zake. Kuhusu wazazi hapo ndo usiseme, nikienda nje ya nchi haendi kusalimia hadi mie nirudi na hata kuwapigia simu. Wazazi wangu kwangu hawafiki hadi mie niwepo bila hivyo hawafiki.
Nilijaribu kuongea naye mara kadhaa amekuwa mkali sana na hata amediriki kunijibu kuwa hanilazimishi kuishi na yeye. Lakini nahis anajibu kwa jeuri coz anajua tukiachana lazima tugawane mali: kama vile nyumba +usafiri n.k lakini hivyo vyote ni jasho langu la kupiga boxi ugaibuni.
Yeye sijazaa naye hata mtoto 1, lkn mie ninae alimkuta but hampendi na hataki nikae naye, mtoto wangu yupo kwa wazazi wangu kijijini. kwa kweli inaniuma saana. Kuhusu kuzaa yeye yaonyesha hadi afanyiwe operation, & it needs some millions of money hapo labda ndo atashika mimba (kulingana na vipimo vya hosp. moja kubwa ya hapa ya wahindi hapa DSM).
NB: 1. Nifanye nini ili mke wangu ajirekebishe tabia yake?
2. Japokuwa nampenda lkn wazazi wangu nao naona ni muhimu ktk maisha yangu,sasa nifanyeje ili naye awapende kama ninavyowapenda wazazi wake na ndugu zake?
3. Nikisema nimuache atataka tugawane MALI, wakati lile ni jasho langu la kupiga boxi, je nifanye nini?
Wapendwa samahani kwa maelezo marefu lakini naomba ushauri wenu na naomba msinitukane wapendwa, maji yamenifika shingoni. Sina nyumba ndogo na wala sina hamu tena ya kuoa, kweli najuta saaana tena saana kuoa!