Naomba ushauri kuhusu haya mahusiano ndugu zangu, nimekwama

demand

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
272
572
Heshima zenu Wakuu,

Kimsingi kuna mwanamke ninadate nae miaka 3 sasa tumeish maisha mengi na hapa katikati tumeachana mara kadhaa na kurudiana.

Kiukwel yeye anaonesha kunipenda na mimi pia nampenda sana tu ila kuna red flags hivi ambazo nimeziona sasa naona kabisa nikimuweka ndani zitanishinda kuvumilia.

Moja wapo ni uvivu, matumizi mabaya ya fedha, kiburi na mtu wa kutengeneza hoja akikosea kifup sio mwepesi wa excuse.

Nimejarbu mara kadhaa kumuacha bila mafankio akirudi kuniomba msamaha ananizdi nguvu najikuta nimerudi na muda unazidi kwenda na nafikiri kwa age yangu sasa nahitaji kuwa na serious relationship ili after miaka 2 niweze kuoa (SIO KUFUNGA NDOA, napenda nieleweke hapa).

Mara zote nimejaribu kumuacha lkn nmeshindwa kumove akija tunarudiana na pia namuonea huruma kumuacha, nikichek muda tuliodate, fedha nilizowekeza, marafki zake, baadhi ya ndugu zake napata huruma lakini ni mwanamke ambae naona siwezi fanya naye future.

Kwa maneno hayo Machache wakuu naomba msaada wa mbinu ya kujitenga na huyu binti mapema bila maumivu meng au nifanye nn ili aniache yeye?

(labda sitopata ile guilty/hatia moyon) mana naona muda unazd kwenda labda namchelewesha kuolewa ana 25 mm nna 27.

Kwa upande mwengne mimi pia najichelewesha kupata mtu wa kusettle nae kwa muda tutengeneze bond kabla ya kuish pamoja

Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuwasilisha

Ninyi n watu wema.
 
Mbona kama unamuonea huruma na unajua fika atakuharibia.

Piga chini.

Ajifunze na sababu ulizotoa hapa kuwa ana kiburi mara matumizi mabaya ya fedha ndo umchane live

Ukiendelea kumlea lea atakupanda kuchwani.

Na ujue warembo wapo wengi wanaotamani nafasi kama hiyo wa settle sasa wee endelea kuteseka..
Be humble

"Umekua umejua right 0r pumba......."
 
Mahusiano Yako hayana changamoto kubwa. Kwasasa mwambie kuwa unataka 1,2,3 yaani ambayo hupendi ayafanye asifanye.

Akifata maelezo Yako muweke ndani na mtadumu. Mimi na shemeji Yako tulidumu Kwa miaka mitatu mahusiano na nilipoweka misingi yangu akafata nikaweka ndani saizi tuna miaka 8 ya kuishi pamoja na tunatarajia mtoto wa tatu next year.

Ukijifanya kumuonea huruma atakutesa na kujiona kafika. Kuwa mwanaume na usiwe mvulana. Pia mwambie name awe mwanamke asiwe msichana abdilike umri umeenda bwana mdogo. Mwenzako nilioa nikiwa na miaka 24, acha kuchelewa akizingua tafuta mbadala haraka Sana achana na huruma za mshumaa.
 
Mueleze wazi kuwa huoni future ya kueleweka kati yako na yeye kwasababu kadhaa kama ulivyoainisha hapo juu.

Huenda yeye hajui kama ana mapungufu hayo ( kama hujawahi kumueleza) ,hivyo uumpe nafasi ya kujirekebisha kama anaweza.

Lakini kama umeshawahi kumueleza na ameshindwa kujirekebisha basi achana nae.

NOTE: unaweza kuja kupata mwingine mwenye mapungufu ambayo utaona bora huyu wa sasa ana " afueni".
 
Namuachaje?nmejarbu mara kadhaa bila mafankio
Mwambie kitachofanya nikuache ni 1,2,3
Kama ni anakupenda, atakuheshimu atabadilika.

Sema kuna vingine ni ngumu.. mf mie mtoto wa mtu ananambia niache vimnyweso🍺Nikamwambia tu ni ngumu.. nipe muda nianze kupunguza.

So wako pia mchane, na umpe muda km kweli wampenda. Ila kama ndio ushakazania huoni fyucha nae, basi mchane atembee. Usimpotezee wakati
 
Jifunze kujipenda mwenyewe kwanza,usipende kumfurahisha mtu au kumuonea huruma huku wewe unateseka!

We bado chalii una mengi yakufanya na malengo shazi!

Unatakiwa uchukue maamuzi sahihi Ili uishi kwa amani maisha marefu pengine hata Kuna watu wanakutegemea wazazi,ndugu nk
 
Back
Top Bottom