Yamenikuta, maji yapo shingoni, naomba ushauri wapendwa plse!

No way,kwa mlio lelewa kwenye familia za kizungu sawa!
Ila mimi niliye lelewa familia za mlo mmoja tena na mama peke yake,kazi yenyewe amefanya u-house gal,ukondakta full kudhalilishwa afu leo mke wangu awe na maana kuliko mama?

Nihukumiwe kwa hilo,ila mke ntapata mwingine na sio mzazi alo nipigania toka navaa nguo moja mwaka mzima hadi leo nilipo!

Uzungu huu ndo unafanya mnaoa wake zenu wana waambia wazazi kitu cha mwisho,tuangalie maisha yetu mnakubali na kuwatosa wazazi wakiwa na shida,but for me......never,my mama is every thing to me!

sure speaker... FAMILY ALWAYS COMES 1ST!!... kama wanamatatizo ajaraibu njia wa ku settle but. usithubutu kumtukana au kumnunia mama kisa mke...
 
Wanawake wengi wa Kichaga wana tabia hii, huwa hawapendi kabisa ndugu wa mume kuja nyumbani kutembea, hapa nina maana asilimia kubwa ya wanawake wa kichaga si wife material. Naomba mniwie radhi kwani hili nimeliona kwa watu wengi saana

Kweli. Mimi ni mchagga mwanaume na huu ndio utamaduni wetu. Watu wakishaoana wanaanza maisha yao na sio suala la ndugu kuanza kuwazongazonga. Ndio maana uchagani wale wazee (wazazi) wanakaa kule hadi kufa hawaendi mjini kwa watoto wao (labda aje kutibiwa na kurudi). Mama yangu mzazi hata kwa greda hawezi kukubali kufunga nyumba yake kule uchagani eti aje kukaa nami hapa Dar. NO. Na hao ndugu pia wakija eg. kusoma wanatakiwa wawe na adabu debe. Ndio maana kila mara tunaenda home kuhiji kwa kuwa ndio wakati wa kukaa na wazazi ambao wako stationed moshi. Hata kule kijijini kwenyewe mtu ukishaoa LAZIMA uhame kwenye mji wa baba uhamie kwako na mkeo hata kama ni mita 5 toka hapo. (wanaita kuwa na jiko lako). Ndio maana ya dhana ya land fragmentation (vihamba), na pia ndio maana kila mchagga mwanaume (poor or rich) ana mji wake na nyumba inafungwa kama hayupo. Lengo ni kufundisha responsibility na self-dependence. Period. Ukitaka kumsaidia ndugu au mwanae unamsaidia akiwa huko huko kwake. sio unamleta kwako kumlea.
Tatizo linakuja pale mchagga anapoaa au kuolewa na mtu wa kabila jingine ambaye kwao dhana ya extended familiy imegeuzwa kuwa dependent family. yaani ukishakuwa na kaafadhali basi wewe ndiye mbebaji wa kila kitu. Nadhani hapa ndipo ilipo changamoto-how to balance the interests za hayo makabila 2. Kama mkeo ni mchagga hilo linampa sana shida-ndugu kuingilia ndoa yenu. Hakuzoea hivyo na atapata sana shida. Kama wewe sio mchagga pia utapata shida-namna ya kubalance culture ya mkeo na yako. Anyaway, mkitumia elimu zenu mtaweza kusolve hili tatizo.
 
Kweli kabisa mdau. Mali kitu gani bwana. Piga chini huyo haraka sana hakufai. Na kwa taharifa hata ukimuoa hiyo ndoa haitadumu kama mwanzo tu ameshaonyesha makucha yake. Na kama unaogopa kugawana mali sasa, jua utagawana nae mali na watoto hapo baadae. Achane nae kabisa, mwanamke gani asopenda ndugu hata kabla hajaolewa. Hao ndio wenye roho ya kutu. Aende akaolewe na Wajerumani maana ndio nasikia wana roho kama yake. Kibongo bongo ndugu ni part na parcel ya familia.

Acha kumind mali, angalia maisha yako yanakwendaje?
Mali utaziacha duniani,
Angalia wewe unataka kuishi maisha ya aina gani kwa furaha.
 
ndugu yangu pole sn sn kwa haya, yanayokupata yamenipata sn nitkuambia historia yng nilipomuoa mke wangu, mwk mmoja tulipopata mtt moja mke wangu akawa mbogo sn, ndugu wakija anagombana nao bila sbb yamsingi lkn mm nilikuwa namvumilia sana, mama yngu akaja toka village, alipokuwepo akawa mtu wa vituko, mdogo wng alipokuja na kaka zangu akawaonyesha kuwa yy ndiye mwenye nyumba khy hawana mamlaka yakuuliza lolote, lkn nikawa najaribu sn kumuelimisha jinsi ya kukaa na watu, nakumbuka aliweza kunifokea mbele ya baba yangu, nikamwambia baba, namuacha akasema labda utoto, khy, mvumilie kidogo, kwani panapotokea machafuko kwenye family nifuraha ya wabaya, lkn naamin kabisa bila ubishi tayari anamtu wakushika bega ndiyo sbb akasema km huwezi ishi nae basi, nakama unaona ningumu, basi amua kuanzisha safari yambali nauache uchunguzi kujua nani ananimzuzua, nakufanyaasione umuhimu wako.
 
Ndugu lets not beat about the bush. Unajua kupenda au kutopendwa kunatokana na jinsi unavyobehave mbele zao hao. Kwanza nina wasi wasi mkeo kaanza jeuri baada ya wewe kwenda nje ya nchi. Wanawake wengie Primitive ndiyo wanavyokuwa anajua kwenda kwako nje uatarudi uko full nondo na akikuruhusu kuendelea kusaidia hao ndugu zako chochote utakachorudi nacho watagawana, kitu ambacho naona ni upuuzi wa hali ya juu.

Huyo mkeo ni guberi, hata umloweke kwenye tangawizi, kitunguu saum, ndimu na ajinamoto hataleta ladha, wewe anza maisha yako upya ukimuomba Mungu akuongeze kwenye safari ndefu iliyo mbele yako. Happiness is within you, usitegemee mtu baki kama huyo mkeo atakufanya uwe na furaha wakati hata kwenye makuzi yake hakuwahi kufurahishwa.

Wewe angalia mbele, mali utachuma nyingine mwachie na umaskini wake.
 
Mali fedha na kadhalika havitaweza kufikia utu wako na ndugu na mwanao, huyo hakuwa mke wako tangia mnakaa kama wapenzi kwakuwa hukuwa karibu usingeweza kujua kama ana commitment somewhere else!

Ni kweli usiwe na hamu ya kuoa lakini haitakiwi kuvumilia matatizo maisha yenyewe mafupi halafu ujikaraishe eti kisa ndo?! raha jipe mwenyewe, mpige chini na usioe tena kwani ukishaharibu mwanzo ujue kila uendako yatakuwa yaleyale. "Nina mifano hai"
 
Labda uliwaringishia ndugu zako kuwa mke wangu nimemsomesha mwenyewe, ni mwema sana, atawasaidia. Ukawapa expectations za uu kuliko mkeo alivyoweza kuwatimilizia, wakaanza kumchukia na kumfanyia visa. Na yeye anajiona ni mke na anastahili heshima kutoka kwao pia. Lugha au vitendo vikagongana.

Waambie nduguzo kuwa huyo ni mkeo, ni familia yako na anastahili heshima kama wanayokupa wewe, wakimdharau wamekudharau wewe.
Mwambie mkeo hao ni nduguzo na wanastahili heshima kama anayokupa, akiwadharau kakudharau. Hivyo hivyo na kuhusu chuki.
Mwanaume lazima uwe na msimamo sio kulegalega na kukimbilia kuvunja ndoa.

USITOE SIRI ZA MKEO AU UBAYA AU UZURI WA MKEO KWA NDUGUZO, LAZIMA WATAMCHUKIA.

Huyu anakuchosha bure ndugu yangu anakaanga mbuyu akuachie wewe mwenye meno utafune huu si ushauri hata kidogo, mwenzako kakulalamikia jambo zito kama hilo wewe unaleta porojo? ukitaka kujua uhondo wa ngoma ni uingie ucheze!
 
Vipi huyo mchumba wako ni Yatima au amekulia kwenye mazingira magumu?? Wanawake wenye tabia hizo au mama wakwe huwa wamezaliwa kwenye mazingira magumu sana. Imagine unachukiaje ndugu wa mumeo? Yaani unajua hata huyu shetani nafikiri tunamsingizia mambo mengi sana.

Nakushauri umwache aendelee na majinamizi yake ya kishetani, kuchukia watu bila sababu, kama yuko tayari kubadilika sawa ila kabla ya kumuoa mpe tena miaka 3 uangalie kama amerudisha mapenzi kwa ndugu zako. othewise I advice you to leave her alone, wake wema wako wengi watakaokuja na upendo kwa familia yako na wanaokkuzunguka pia.

Amini Amini nakwambia ndugu yangu angekuwa yatima au amekulia kwenye mazingira magumu angekuwa mnyenyekevu na mtiifu kweli, hapa umekwenda kushoto kidooogo!
 
Mkuu, pole sana na hizo changamoto.
Najua wengi wameshauri kwa kadiri ya uwezo wao, lakini kwa upande wangu ningeshauri wazo la 'KUVUNJA NDOA' ondoa kabisa.
Hebu fuata ushauri uliotelewa na wadau hawa




Siku zote lazima tujifunze kutatua na sio kukimbia matatizo. Kama ndoa yako ni ya KIKRISTO, basi imekatazwa kabisa kwa wanandoa kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinzi.
Kwa vile tatizo lako linaweza lisihusiane na uzinzi hivyo basi, yakupasa kutatua tatizo, labda ukirudi kutoka kubeba box.
Kaa na watu wenye busara, watu wa kanisa kama wachungaji jaribu kupata ushauri wao. Pia jaribu kutafuta nafasi nzuri ya faragha kuzungumza na mwenzio. Hayo matatizo yote yanasuluhisho... Hebu weka moyo wako na uamini kuwa utayapatia ufumbuzi matatizo yako na sio kuyakimbia, kwa sababu huna hakika utakutana na mtu wa namna gani.
Kama mliweza kupanga na kufunga ndoa pamoja na changamoto zote zile huoni kuwa unaweza kupata suluhisho??
Ndoa yako ni changa sana, haina hata mwaka,hivyo nafasi ya kupata solution ni kubwa sana. Mkae chini mzungumze
Labda angalizo kwa wasomaji wengine, mojawapo ya vitu vilavyoleta matatizo katika ndoa ni WATOTO wa nje kuletwa ndani ya ndoa. ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia kwa moyo mmoja, lakini kama ikiwezekana watoto wa nje uwahudumie kivyao vyao..

Asante

Hakuna mtoto wa nje wote ni watoto wa ndani bwana Ila wewe nakushangaa sana unayeendekeza vitu vya kijamii ukaacha vya damu ndoa ni man made hatuna uhakika sana kama vianamuhusisha Mungu lakini kiumbe mwanadamu hapatikani bila consent ya Mungu ndio maana it is discussable kutoa talaka lakini sio kutoa mimba!
 
Ningelkua karibu yako ninge kunasa vibao . Inakuaja pesa zako za Box humweki mwanao vizuri naunamwacha aishi kijijini, hana mamake , au mamakeni wakijijini pia?

Kuhusu huyo mkeo, nadhani hakufai, kikubwa kuliko vyote ni pale asipo mkubali mwanao, hilo ndio jambo kubwa, kama hawezi mkubali basi na yeye usimkubali, achana naye hakufai, unapo zaa watoto ni kujitoa mhanga kwa maisha ya hao watoto na kama yeye hamkubali basi hakufai katika maisha yako.

Suala la kuto salimia ndugu, hilo halina umuhimu kwnai ndoa ni yako wewe n amkeo, kam hawapendi nduguz ako labda nao wana tatizo, ila hilo sio muhimu , muhimu ni furaha yako wewe, mkeo na mwanawenu , suala la ndugu ni sio muhimu kwa maisha ya sasa.
 
Inaelekea wewe uko njia panda na hujui nafasi ya mkeo, mzazi wako vilevile ndugu zako katika maisha yako...halafu bro, acha kuwaza mali mana zote tunamalizana nazo duniani nadhani hili linakuumiza sana kichwa! uko so materialist!!

Mwisho wa siku wewe ni mwanaume, mwanaume lazima ajue cha kufanya hivyo uamuzi uko mikononi mwako ukifikiria suala zima la ndoa yako. Mpe support pia mkeo ambae hana mtoto, hii inamuathiri pia kimawazo ilhali una mtoto kabla ya ndoa.
 
hapa naamini ule msemo usemao si kila mwanamke aweza kuwa mke wengine waweza kuwa ma house girl. huyo si wa kumbembeleza kamwe kama leo anawachukia mdg zako na hata mtoto wa damu yako hakika jiandae nawe kukanwa kama Yesu alivyokanwa. kama mpe muda mwambie mali za nini wakati huna amani?unalilia mali huku unakosa baraka za wazazi.tumia akili sana kuishi na mwanamke huyo.
 
Ni hivi Dada Lizzy,

Hayo hayakuwepo hapo mwanzo, imagine hata mtoto wangu aliishi nami pamoja na yeye na kuanza shule hapa mjini hadi darasa la 3 lkn mwaka huu mie narudi field ananiambia mtoto nimempeleka kijijini coz jeuri nataka akajifunze tabia huko rural. Nina mdogo wangu wa mwisho namsomesha na yupo day school, hawaongei hata akimwamkia hajibu hapo mimi nipo je nikiondoka inakuwaje mpendwa? Yaani baada ya ndoa tu tabia imebadilika sana, na sasa ndo ameajiriwa akitoka asubuhi kurudi jioni akifika tu kulala kisa amechoka, mie ndo niingie jikoni au huyo mdogo wangu. Da lizzy nipe ushauri plse
Sas hapa na wewe utakuwa mwanaume *****. Unataka ushauriwe nini ikiwa wewe mwenyewe unapenda hali hiyo? Kama hupendezwi na hali hiyo kwa nini usubiri kupewa ushauri wakati wewe mwenyewe unakerwa? Achana naye kama anakuudhi.
 
Mi nimepita tuuuuuu!! Ila kwa ufupi! Huyo hafaiiiiiii! Mcheuwee kabisaaaaaaaaaa! Maisha ni wa2 Brother.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom