Yaliyojiri Jijini Arusha: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli – Oktoba 6, 2015

Huyo aliyefungua hizo email feki anastahili kufutwa kazi mara moja hapo kitengo cha IT -Masaki kwani kitendo cha kukosea Jina la Ally Bananga na kumuita Ally Bamanga ni cha kuaibisha idara yetu ya propaganda ccm

Kama ulikuwa naye wakati anaforge hizo emails. SAWA
 

Tehetehetehe!!!!!!!!!! CCM mna kampeni za kishamba kweli mwaka huu


6dtycn.jpg

Kama unaona kampeni za kishamba subiri October 25 uone, mtu anavyoingia IKULU
 
ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na watanzania hasa wakazi wa jiji la arusha imewaadia ambapo mgombea wa urais wa tanzania kwa tiketi ya ccm, dk. Magufuli atafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja wa sheikh amir abeid kuanzia saa 8:00 mchana.

star tv na tbc1 watakuwa hewani live kukuletea mkutano katika viwanja vya sheikh amir abeid.

kabla ya kufanya mkutano kwenye viwanja wa sheikh amir abeid, dk. Magufuli ataelekea kwanza wilayani monduli leo asubuhi ambapo atafanya mkutano wa hadhara katika eneo la mto wa mbu na mara baada ya mkutano huo atafanya mkutano mwingine mkubwa wa hadhara, kwenye ''ngome'' ya lowassa mjini monduli, kisha kuelekea wilayani longido kwenye mkutano mwingine wa hadhara wa kampeni.

Updates za mikutano yote zitapatikana hapa.

Be the first to know...!

Umoja ni ushindi.

#hapakazitu
dk. Magufuli na timu yake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu edward moringe sokoine

updates:
watu ni wengi kweli kweli ndani na nje ya uwanja. Maelfu wanazidi kuingia ndani ya uwanja.

Wana arusha wanaweka historia katika mahudhurio haya ambayo yanazidi kuvuta maelfu ya wananchi.

Baadhi ya picha za maandalizi ya mkutano katika uwanja wa sheikh amri abeid...
agzuiabasjcqkra1uul0uyokimcngwcnnyy8mvjqicnu.jpg

12112168_1100653236611663_826268539601147546_n.jpg

updates:
dk. Magufuli anaingia uwanjani.

Hii ni hatari! Uwanja umetapika..

Mkutano unaanza kwa kukaribishwa makada kuwasalimia wana arusha na kuongea mawili matatu.

sendeka:
kama kuna baadhi ya watu bado walidhani ccm haipo arusha, inabidi kwa sasa wakapime fikra zao. Umati huu umejibu maswali na mitazamo hiyo.

Tunataka rais atakayepiga vita rushwa na ufisadi kwa nguvu zote. Ukiulizwa, magufuli atapambana na rushwa na ufisadi, jibu linatoka rohoni, ndiyo.

Huhitaji kwenda maktaba kusoma utendaji wa magufuli, ukipanda gari utauona.

Wana arusha ninaomba niwaulize, kwa nini hakuna maandamano kwenye jimbo la mbunge ndasamburo au mbowe? Kwa nini ni arusha mjini pekee? Jibu nitawapa nikirudi hapa kumnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm.

bulembo
mpaka sasa magufuli amesafiri kwa njia ya barabara umbali wa zaidi ya kilometa 21,000 wilaya 123, majimbo 228.

Mabadiliko ndani ya ccm yalianzia kwenye uchaguzi wa ndani. Agizo la mkutano mkuu ilikuwa ni kuhakikisha wenye magamba wanayavua au chama kinawavua. Kupitia mkutano mkuu, chama kiliamua kumteua magufuli ambaye hana makandokando ili akisafishe chama na serikali. Chama kinaamini magufuli atasafisha chama na serikali.

kinana.
arusha leo mmetia fora. Jipigieni makofi. Haijawahi kutokea katika uwanja huu.

Wapiga kura muache ushabiki katika kupiga kura. Kura ni hukumu ya maisha yako. Pigeni kura kwa malengo.

Watanzania wanataka ajira na siyo matumaini. Watanzania wanataka kero mbali mbali ziondolewe. Urasimu serikalini ukomeshwe mara moja.

Ninaamini kupitia serikali ya magufuli, serikali yake itakuwa na viongozi waadilifu na wachapa kazi kama alivyo yeye.


dk. Magufuli.
ninawapongeza sana sana kwa kuja hapa kunisikiliza mtumishi wenu.

Sijawahi kuona umati mkubwa kama huu katika uwanja huu. Watu mpaka wameamua kupanda kwenye magolofa ili kunisikiliza. Ninawashukuru sana na kuwaahidi sitawaangusha.

Jiji la arusha lilikuwa linasifika kwa kuwa jiji la kusuruhisha ugomvi au mapigano ya nchi za jirani zetu. Mahakama ya kimataifa iko hapa. Kwa sasa limeanza kukosa sifa hiyo.

Jiji la arusha lilikuwa linasifika kwa kuwa kitovu cha utalii. Kwa sasa sifa hiyo imeanza kutoweka. Tunahitaji mabadiliko sahihi ili kuilinda heshima ya jiji la arusha. Vulugu na maandamano ndani ya jiji hili zinasababisha kushuka kwa heshima hii. Wana arusha nawaomba mchague wabunge na madiwani ambao sera zao siyo maandamano.

Ninataka jiji la arusha liwe la mfano katika nchi za afrika ya mashariki na kati. Tuachane na hii dhana ya maandamano. Maandamano ni kufukuza uwekezaji. Ni kupoteza muda wa kazi. Tufanye kazi tu. Mimi kwangu ni kazi tu.

Serikali yangu itahakikisha tunakuwa na mahusiano ya karibu hasa na nchi zilizotuzunguka na pia duniani kwa ujumla.

Nikiingia madarakani kama mtanichagua. Nitazifunga kwa kufuli kama jina langu hizi kero na viushuru ushuru. Hatuwezi kuwa na serikali inayotegemea ushuru wa wafanya biashara ndogo ndogo na wafanyakazi ya kipato cha chini. Serikali yangu itakuwa rafiki wa karibu na wafanyakazi wa kipato cha chini na wafanya biashara ndogo ndogo.

Nitahakikisha hakuna mafisadi nchini ili pato la taifa linufaishe watanzania wote. Nitaanzisha mahakama ya mafisadi na majizi ili niwafunge. Mimi siyo mwanasiasa mzuri, kwangu ni kazi tu.

Kuna mafisadi wengine wameanza kukimbia baada ya mkutano mkuu kuniteua kuwa mgombea urais kwa sababu wananifahamu vizuri. Mimi sina urafiki na wala rushwa au mafisadi.

Nimewaambia wananchi wa monduli, nitaienzi kazi ya marehemu edward moringe sokoine kwa kupambana na mafisadi na majizi.

Serikali yangu itakuwa na mawaziri wachache ambao ni waadilifu na wachapakazi.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu, kuanzia mwaka kesho kutakuwa hakuna kulipa karo (school fees) kuanzia chekechea mpaka kidato cha nne. Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya juu itatolewa haraka ili kazi ya wanafunzi/wanachuo iwe ni kusoma na siyo kukimbizana kwenye mikopo.

Serikali yangu itahakikisha madawa yanapatikana kwenye zahanati na hospitali na wale wanaohusika na usambazi wahakikishe kwa sasa wanabadilika kabla sijaingia madarakani. Siwezi kukubali hata kidogo madawa kukaa kwenye store wakati kwenye zahanati au hospitali hakuna dawa.

Serikali yangu itatoa milioni 50 kwa kila mtaa, kijiji, kata kwa ajiri ya vikundi mbali mbali.

Serikali yangu itapunguza kodi kwa wafanyakazi ambapo kwa sasa wanakatwa asilimia 11.

Suala la experience kama kigezo cha kuajiri tutahakikisha tunaliondoa kama liko kwenye kanuni au sheria. Hiki kigezo cha experience kinaweza kuwa ni kikwazo cha ajira kwa vijana wetu na kinatumiwa na wawekezaji wa kutoka nje na ndani ili walete watu wao kutoka nje.

Ninaomba kura kwa wana ccm, ukawa, cuf, chadema, act na hata wale wasio na vyama kwa sababu nitakuwa rais wa watanzania wote.

aliyekuwa organiser wa maandamano jijini arusha:
mimi nimeamua kujitoa chadema kutokana na baadhi ya viongozi wakuu kushindwa kukisimamia kile ambacho tulikuwa tunakipigia kelele ndani na nje ya chadema.

Msingi mkuu wa chadema ulikuwa ni kupambana na rushwa na ufisadi na siyo kutumia mafisadi na ulaghai kuingia ikulu.

Nilikuwa nikiratibu maandamano hapa arusha ya kumpinga lowassa kutokana na ufisadi wake ambao umelifilisi taifa. Tulimpinga lowassa mpaka wengine walipoteza maisha au kupata vilema vya kudumu lakini kilichonishangaza na kunisikitisha sana siyo tu kukaribishwa kwa lowassa ndani ya chadema bali pia kupewa nafasi ya kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chadema.

Siwezi nikaishi ndani ya uwongo na ulaghai uliofanywa na baadhi ya viongozi wakuu wa chadema. Ninamuogopa mungu.

Nimeamua kuachana na chadema. Nimeamua kujiunga ccm kwa sababu mgombea wake wa urais ni kiongozi ambaye ni mwadilifu, mzalendo na mchapakazi. Nitaipigania ccm kwa nguvu zangu zote.






#hapanikazitu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom