Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 9,146
- 6,056
Hiyo sehemu fulani wameanza na ziara ya 'Royal Tour' na kurudisha mawaziri incompetent madarakaniMwaka 2012, Makamu wa Rais wa Malawi, Joyce Hilda Banda alichukua nchi baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika. Waliomuwekea mizengwe kipindi anatakiwa akabidhiwe nchi, alikuja kuwashughulikia alipokuwa Rais. Akawa mwanamke wa kwanza kuongoza Taifa hilo.
Akaingia madarakani, akawa haambiliki, maisha ya wananchi wa Malawi yakapanda maradufu. Wala hakujali, akawa busy na ziara za nje ya nchi yake katika kuifungua mipaka ya nchi.
Mwaka 2014, Uchaguzi Mkuu ukafanyika na Wamalawi hata hawakukosea, wakampiga chini kwenye sanduku la Kura. Ukawa mwisho wa Bi Joyce Banda kama Rais wa kwanza na wa pekee (mpaka sasa) wa Malawi.
Naiona hii simulizi ya Bi Joyce Banda inaendana kabisa na ya sehemu fulani ambapo inaweza ikatokea...