Rais Samia anatumia mbinu zilizomuangusha Joyce Banda Malawi, na yeye anaweza kuanguka 2025

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Mwaka 2009 Joyce Hilda Banda alijikuta kwenye mshangao wa bahati baada ya kupendekezwa na Rais Bingu wa Mutharika kuwa makamu wa Rais nchini Malawi. Surprise ya namna hii pia ilimkuta Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya kupendekezwa na chama chake CCM kuwa mgombea mwenza wa John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu 2015.

Wote Joyce Hilda Banda na Samia Suluhu Hassan hawajawahi kuwa na ndoto za kuwa makamu wa uRais achilia mbali kuota Urais ambao ulikuja kuwaangukia baadaye kwa nyakati tofauti. Kwa hiyo nafasi hizi za umakamu wa Urais na Urais zimekuja kuwaangukia by surprise bila wao wenyewe kuwa na matarajio hayo.

Tukianza Joyce Hilda Banda mwaka 2012 alijikuta akishika madaraka makubwa ya kuwa Rais wa Malawi baada ya kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika. Hii tukio halina utofauti na tukio lililomfanya Bi. Samia Suluhu kushika madaraka 2021 baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Joyce Banda alishika madaraka hayo ikiwa imebakia miaka miwili Malawi kuingia katika uchaguzi mkuu huku Bi. Samia akishika madaraka hayo ikibakia miaka minne nchi iingie katika uchaguzi mkuu.

Hivyo basi Joyce Banda alikuwa na nafasi kubwa ya kujijenga zaidi kisiasa na kijamii kwa kuwa mstari wa mbele kutatua shida na kero za wananchi. Kwa bahati mbaya Joyce alishindwa kutumia nafasi hiyo. Kashfa nzito zikaanza kumwandama mwanamama huyo, kashfa nyingi zikihusisha ufisadi wa mali na pesa za umma pamoja na kuiingiza Malawi katika mikataba mibovu. Wapinzani waliposimama na hoja za ufisadi, silaha pekee ambayo Bi. Joyce Banda aliona inafaa ni jinsia yake. Yeye na wafuasi wake wakasimama na kuwajibu wapinzani kwamba wanamshambulia Joyce na hoja za ufisadi kwa sababu yeye ni mwanamke.

Rais Joyce Banda aligeuza jinsia yake kama ngao na kinga yake dhidi ya tuhuma za ufisadi zilizokuwa zimemwandama. Aliwalipa viongozi wa dini na kimila wamtetee na hoja hiyo ya jinsia. Aliwalipia press conference wafuasi wake watetee jinsia yake badala ya kashfa za ufisadi zilizokuwa zinamwandama, akiamini zitamsaidia uchaguzi mkuu uliokuwa unafuata 2014. Wamalawi hawakuwa wajinga uchaguzi mkuu ulipofika waliamua kumpiga chini na kuchagua upinzani.

Joyce akatumia mamlaka yake ya Urais kufuta matokeo ya uchaguzi kwa sababu hakushinda. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alikataa na kumtangaza aliyeshinda kutoka chama cha upinzani. Waziri wa Joyce ambaye alikuwa kiherehere na tabia mbovu kama alivyo Nape alijiuwa kwa kujinyonga akihofia maisha yake baada Joyce Banda kuanguka.

Miaka 10 baada ya anguko la Joyce Banda anatokea Samia Suluhu Hassan ambaye anatumia njia zilezile zilizomwangusha Rais Joyce Banda za kujibu kashfa zake za uuzaji wa bandari kwa DP World kwa mkataba wa milele. Tangu sakata la kuuza/kukodisha bandari lianze kupamba moto kwa wiki mbili sasa, Rais Samia ameshindwa kujibu hoja za wanaopinga mkataba huo na badala yake anatumia silaha ya Bi. Joyce Banda, ijapo yeye kaiboresha kwa kuongeza udini na Uzanzibari.

Watu mbalimbali wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa wanahoji maswali haya matatu kwamba:

1- Kwanini mkataba huo wa kukodisha bandari hauna kikomo cha muda yani ni wa milele?

2- Kwanini mkataba huo hauwezi kuvunjika hata kama wawekezaji hao wana performance ndogo?

3- Kwanini bandari za Zanzibar hazijajumuishwa kwenye mkataba huo na badala yake ni bandari za Tanzania Bara pekee pamoja na kwamba bandari ni sehemu ya mambo yaliyopo kwenye muungano kwa katiba na sheria za nchi?

Huwezi kuamini kwamba pamoja na washauri wa kisiasa alionao Samia, wataalamu na watu wengine wote waliomzunguka, wameshindwa kujibu hoja hizi. Njia pekee aliyoona inafaa ni kujificha kwenye kichaka jinsia, udini na Uzanzibari ili kutafuta uhalali wa kuuza ama kukodisha bandari zetu kwa mikataba mibovu.

Yani unakodisha/kuuza bandari kwa mkataba wa hovyo , watu wanahoji unajibu kwa sababu mimi ni mwanamke ama muislamu au kwa sababu mimi ni Mzanzibar? Kwani ukiwa mwanamke ama Mzanzibar au mwislamu ndio una uhalali wa kuuza nchi kwa kusaini mikataba mibovu? Aliyekuambia dini au jinsia ni kichaka cha kuficha maovu ni nani?

Ukweli ni kwamba njia hii haitamsaidia Samia na badala yake anaenda kuanguka. Miezi 10 sasa Samia anapoteza ushawishi. Mfumuko wa bei, tozo pamoja na kashfa za ufisadi katika serikali yake ni moja ya vitu vinavyompunguzia mvuto kwa wananchi.

Suala la kuuza bandari kwa mkataba wa milele na milele ndio limemchinja mazima Samia. Mkutano alioufanya Mwanza majuzi ulikuwa na watu wachache licha ya kusomba watu kwa malori lakini ni kama alikuwa anahutubia viongozi wa ccm na watumishi wa umma aliotoka nao Dodoma, halmashauri na jiji. Ile ilikuwa ni message kwamba kwa sasa Samia hatakiwi tena. Njia pekee ambayo itamnyanyua Samia kutoka matopeni alikokwama ni kutupilia mbali mkataba huo wa kuuza bandari pamoja na kuwachukulia hatua mafisadi wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG. Tofauti na hapo hawezi kupata kibali tena 2025 hata angetumia majeshi. Ushauri huu ni chungu kama sumu ya nyigu lakini ukifuatwa ni mtamu kama asali.

Mdude Nyagali 7 x 70.
20230617_195705.jpg
 
Mdude Nyagali 7 x 70.View attachment 2661162
Samia mpaka 2030 hutaki hamia zambia
 
Kibongo bongo wananchi wanatakiwa kuchachamaa sana iwapo kweli wanataka jambo hilo litimie. Maana policcm siyo watu wazuri hata kidogo, linapokuja suala la kuilinda ccm kubakia madarakani.

Au kada mtiifu Lucas mwashambwa, una maoni gani juu ya jambo hili? ccm bila ya msaada wa polisi inaweza kushinda hata kiti cha ubalozi kweli? Usisahau hata JK kipindi hicho, alishawahi kuonya juu ya jambo hili.
 
Kibongo bongo wananchi wanatakiwa kuchachamaa sana iwapo kweli wanataka jambo hilo litimie. Maana policcm siyo watu wazuri hata kidogo, linapokuja suala la kuilinda ccm kubakia madarakani.
Mwananchi mwenyewe wa ku chachamaa yupo wapi. Huyu huyu anayeshunda akubashiri matokeo ya mechi kwa 1000 ili awe kama bahresa kesho yake baada ya kushinda ubashiri? Au huyu anaye hongwa kofia na tshert ili amchague mgombea wa ccm?
 
Mwaka 2009 Joyce Hilda Banda alijikuta kwenye mshangao wa bahati baada ya kupendekezwa na Rais Bingu wa Mutharika kuwa makamu wa Rais nchini Malawi. Surprise ya namna hii pia ilimkuta Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya kupendekezwa na chama chake CCM kuwa mgombea mwenza wa John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu 2015.

Wote Joyce Hilda Banda na Samia Suluhu Hassan hawajawahi kuwa na ndoto za kuwa makamu wa uRais achilia mbali kuota Urais ambao ulikuja kuwaangukia baadaye kwa nyakati tofauti. Kwa hiyo nafasi hizi za umakamu wa Urais na Urais zimekuja kuwaangukia by surprise bila wao wenyewe kuwa na matarajio hayo.

Tukianza Joyce Hilda Banda mwaka 2012 alijikuta akishika madaraka makubwa ya kuwa Rais wa Malawi baada ya kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika. Hii tukio halina utofauti na tukio lililomfanya Bi. Samia Suluhu kushika madaraka 2021 baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Joyce Banda alishika madaraka hayo ikiwa imebakia miaka miwili Malawi kuingia katika uchaguzi mkuu huku Bi. Samia akishika madaraka hayo ikibakia miaka minne nchi iingie katika uchaguzi mkuu.

Hivyo basi Joyce Banda alikuwa na nafasi kubwa ya kujijenga zaidi kisiasa na kijamii kwa kuwa mstari wa mbele kutatua shida na kero za wananchi. Kwa bahati mbaya Joyce alishindwa kutumia nafasi hiyo. Kashfa nzito zikaanza kumwandama mwanamama huyo, kashfa nyingi zikihusisha ufisadi wa mali na pesa za umma pamoja na kuiingiza Malawi katika mikataba mibovu. Wapinzani waliposimama na hoja za ufisadi, silaha pekee ambayo Bi. Joyce Banda aliona inafaa ni jinsia yake. Yeye na wafuasi wake wakasimama na kuwajibu wapinzani kwamba wanamshambulia Joyce na hoja za ufisadi kwa sababu yeye ni mwanamke.

Rais Joyce Banda aligeuza jinsia yake kama ngao na kinga yake dhidi ya tuhuma za ufisadi zilizokuwa zimemwandama. Aliwalipa viongozi wa dini na kimila wamtetee na hoja hiyo ya jinsia. Aliwalipia press conference wafuasi wake watetee jinsia yake badala ya kashfa za ufisadi zilizokuwa zinamwandama, akiamini zitamsaidia uchaguzi mkuu uliokuwa unafuata 2014. Wamalawi hawakuwa wajinga uchaguzi mkuu ulipofika waliamua kumpiga chini na kuchagua upinzani.

Joyce akatumia mamlaka yake ya Urais kufuta matokeo ya uchaguzi kwa sababu hakushinda. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alikataa na kumtangaza aliyeshinda kutoka chama cha upinzani. Waziri wa Joyce ambaye alikuwa kiherehere na tabia mbovu kama alivyo Nape alijiuwa kwa kujinyonga akihofia maisha yake baada Joyce Banda kuanguka.

Miaka 10 baada ya anguko la Joyce Banda anatokea Samia Suluhu Hassan ambaye anatumia njia zilezile zilizomwangusha Rais Joyce Banda za kujibu kashfa zake za uuzaji wa bandari kwa DP World kwa mkataba wa milele. Tangu sakata la kuuza/kukodisha bandari lianze kupamba moto kwa wiki mbili sasa, Rais Samia ameshindwa kujibu hoja za wanaopinga mkataba huo na badala yake anatumia silaha ya Bi. Joyce Banda, ijapo yeye kaiboresha kwa kuongeza udini na Uzanzibari.

Watu mbalimbali wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa wanahoji maswali haya matatu kwamba:

1- Kwanini mkataba huo wa kukodisha bandari hauna kikomo cha muda yani ni wa milele?

2- Kwanini mkataba huo hauwezi kuvunjika hata kama wawekezaji hao wana performance ndogo?

3- Kwanini bandari za Zanzibar hazijajumuishwa kwenye mkataba huo na badala yake ni bandari za Tanzania Bara pekee pamoja na kwamba bandari ni sehemu ya mambo yaliyopo kwenye muungano kwa katiba na sheria za nchi?

Huwezi kuamini kwamba pamoja na washauri wa kisiasa alionao Samia, wataalamu na watu wengine wote waliomzunguka, wameshindwa kujibu hoja hizi. Njia pekee aliyoona inafaa ni kujificha kwenye kichaka jinsia, udini na Uzanzibari ili kutafuta uhalali wa kuuza ama kukodisha bandari zetu kwa mikataba mibovu.

Yani unakodisha/kuuza bandari kwa mkataba wa hovyo , watu wanahoji unajibu kwa sababu mimi ni mwanamke ama muislamu au kwa sababu mimi ni Mzanzibar? Kwani ukiwa mwanamke ama Mzanzibar au mwislamu ndio una uhalali wa kuuza nchi kwa kusaini mikataba mibovu? Aliyekuambia dini au jinsia ni kichaka cha kuficha maovu ni nani?

Ukweli ni kwamba njia hii haitamsaidia Samia na badala yake anaenda kuanguka. Miezi 10 sasa Samia anapoteza ushawishi. Mfumuko wa bei, tozo pamoja na kashfa za ufisadi katika serikali yake ni moja ya vitu vinavyompunguzia mvuto kwa wananchi.

Suala la kuuza bandari kwa mkataba wa milele na milele ndio limemchinja mazima Samia. Mkutano alioufanya Mwanza majuzi ulikuwa na watu wachache licha ya kusomba watu kwa malori lakini ni kama alikuwa anahutubia viongozi wa ccm na watumishi wa umma aliotoka nao Dodoma, halmashauri na jiji. Ile ilikuwa ni message kwamba kwa sasa Samia hatakiwi tena. Njia pekee ambayo itamnyanyua Samia kutoka matopeni alikokwama ni kutupilia mbali mkataba huo wa kuuza bandari pamoja na kuwachukulia hatua mafisadi wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG. Tofauti na hapo hawezi kupata kibali tena 2025 hata angetumia majeshi. Ushauri huu ni chungu kama sumu ya nyigu lakini ukifuatwa ni mtamu kama asali.

Mdude Nyagali 7 x 70.View attachment 2661162
Oya, mbona mnakomaa sana na hiyo, kama ufaidiki kama Mimi kelele za nini kila siku. Hayo ni maamuzi ya Mh. Samia, wewe subiri ushike madaraka uamue ya kwako, au kama una hasira 2025 kajipigie au mpigie kura mwingine. Tumewachoka, Bandari, Bandari. Karamagi kala sana, waache wengine nao wachukue. Njoo tulime mihogo Moro.
 
Kwa katiba ILIYOPO ni ngumu sana kuitoa ccm madaraka I,mi nadhani nusu mkate mtaambulia hata serikali ya umoja wa kitaifa kwa matakwa ya CCM yenyewe!!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo SANA!!
 
Njia pekee ambayo itamnyanyua Samia kutoka matopeni alikokwama ni kutupilia mbali mkataba huo wa kuuza bandari pamoja na kuwachukulia hatua mafisadi wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

Ushauri bora kabisa anaopewa yeye Rais na pia chama dola kongwe CCM anachoongoza kuwa 2025 mambo magumu

Bandiko bora kabisa kuhusu tathmini ya hali ya kisiasa na kijamii iliyopo sasa nchini Tanzania
 
Back
Top Bottom