Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Kung'atuka kwa uelewa wangu mdogo kunachukua muelekeo wa mtu kulazimika kuacha kitu fulani bila ya hiari yake pengine mazingira yamemfanya achukue uamuzi huo. Sina uhakika kwa asilimia 100 kua Mwl alitumia neno hilo kwa mantiki hiyo possibly.
Ambacho nilikikusudia sana ni kutathmini maneno ya Mwl kwa ujumla na ukweli wake ktk wakati tulionao na sio neno mojamoja na ninadhani kua maneno ya Mwl kwa ujumla yanaeleweka no matter kung'tuka itakua na maana gani.
Naomba mchango wako sister au kama ni brother please. Thanks.
Neno Kung'atuka linatoka kwenye neno ng'oka, Ukiliangalia vizuri neno hili utagundua kwamba
mtu hawezi kung'oka kwa hiari yake kama ulivyosema.
hata kwa vitu, ni vitu venye matatizondio ung'olewa, kwa mfano kung'oa jino, kung'oa jino
sio kitendo cha kufurahia sababu mtu anafikia hatua ya kung'oa jino pale jino hilo linapokuwa
tatizo mwilini mwake. Ama kung'oa kisiki.
Kabla sijaenda kwa Mwalimu, Hivi karibuni Marais kazaa wa nchi za Uaribuni wameng'olewa madarakani,
Mchukulie Ali Salehe wa Yemeni, Aling'ang'ania weeee lakini mwisho wa siku alilazimika kuachia madaraka,
Ali Salehe hawezi kusema ameng'atuka kwa mapenzi yake, ameng'atuliwa au ameng'olewa bila yeye
mwenyewe kupenda. Ali salehe, Hussein Mubaraka, Ben Alli, Ghadafi, hawa, katika hisia ama macho ya
wananchi wao walikuwa wamefikia hatua ya kuwa tatizo kubwa nchini mwao ndio maana wakaamua
kuwang'oa.
Sasa kama Mwalimu alilitumia hili neno kwa usahihi, inamaana kwamba Hapa nchini pia na yeye alikuwa
ameanza kuwa tatizo, Je ni kweli ilikuwa hivyo? La hasha, sababu mpaka sasa watanzania bado wanamlilia,
ni nini kilichomg'oa?
Je Mwalimu alikuwa ameishaona kwamba Chama Chake kilikuwa kimeanza kupata kansa ambayo asingeweza
kuitibu akiwa ndani yake? kwa maana ya kwamba dhamira yake ndio iliyomng'oa?
Ama inawezekana kwamba Mwalimu aliona wazi wazi kwamba muelekeo wa uchumi wa dunia ulikuwa unaupa
mkono mfumo wa ujamaa na hivyo dhamira yake ikamlazimisha kung'oka na kuwapisha wengine kuukaribisha
mfumo mpya? I do not know, watetezi wake wapo, watatusaidia humu ndani.
Cha Msingi ni kwamba, CCM imekuwa kama Mwiba kwenye mwili wa binaadamu, CCM imekuwa kama kisu
moyoni mwa Watanzania na tumeamua kuking'oa.