Wosia wa Mwl. Nyerere - Mimi ninang'atuka na siasa ya Tanzania

Kung'atuka kwa uelewa wangu mdogo kunachukua muelekeo wa mtu kulazimika kuacha kitu fulani bila ya hiari yake pengine mazingira yamemfanya achukue uamuzi huo. Sina uhakika kwa asilimia 100 kua Mwl alitumia neno hilo kwa mantiki hiyo possibly.
Ambacho nilikikusudia sana ni kutathmini maneno ya Mwl kwa ujumla na ukweli wake ktk wakati tulionao na sio neno mojamoja na ninadhani kua maneno ya Mwl kwa ujumla yanaeleweka no matter kung'tuka itakua na maana gani.

Naomba mchango wako sister au kama ni brother please. Thanks.

Neno Kung'atuka linatoka kwenye neno ng'oka, Ukiliangalia vizuri neno hili utagundua kwamba
mtu hawezi kung'oka kwa hiari yake kama ulivyosema.

hata kwa vitu, ni vitu venye matatizondio ung'olewa, kwa mfano kung'oa jino, kung'oa jino
sio kitendo cha kufurahia sababu mtu anafikia hatua ya kung'oa jino pale jino hilo linapokuwa
tatizo mwilini mwake. Ama kung'oa kisiki.

Kabla sijaenda kwa Mwalimu, Hivi karibuni Marais kazaa wa nchi za Uaribuni wameng'olewa madarakani,
Mchukulie Ali Salehe wa Yemeni, Aling'ang'ania weeee lakini mwisho wa siku alilazimika kuachia madaraka,
Ali Salehe hawezi kusema ameng'atuka kwa mapenzi yake, ameng'atuliwa au ameng'olewa bila yeye
mwenyewe kupenda. Ali salehe, Hussein Mubaraka, Ben Alli, Ghadafi, hawa, katika hisia ama macho ya
wananchi wao walikuwa wamefikia hatua ya kuwa tatizo kubwa nchini mwao ndio maana wakaamua
kuwang'oa.

Sasa kama Mwalimu alilitumia hili neno kwa usahihi, inamaana kwamba Hapa nchini pia na yeye alikuwa
ameanza kuwa tatizo, Je ni kweli ilikuwa hivyo? La hasha, sababu mpaka sasa watanzania bado wanamlilia,
ni nini kilichomg'oa?
Je Mwalimu alikuwa ameishaona kwamba Chama Chake kilikuwa kimeanza kupata kansa ambayo asingeweza
kuitibu akiwa ndani yake? kwa maana ya kwamba dhamira yake ndio iliyomng'oa?

Ama inawezekana kwamba Mwalimu aliona wazi wazi kwamba muelekeo wa uchumi wa dunia ulikuwa unaupa
mkono mfumo wa ujamaa na hivyo dhamira yake ikamlazimisha kung'oka na kuwapisha wengine kuukaribisha
mfumo mpya? I do not know, watetezi wake wapo, watatusaidia humu ndani.

Cha Msingi ni kwamba, CCM imekuwa kama Mwiba kwenye mwili wa binaadamu, CCM imekuwa kama kisu
moyoni mwa Watanzania na tumeamua kuking'oa.
 
Mlikuwa mnaving'ata viti kwa mananihii?

Hilo neno ukitaka usitake asili ya maana yake ndio hiyo, linatokana na kung'ata, halafu huko kwa kina Nyerere si unajuwa meno wanayafanya nini? wee kwa kung'ata yale aking'atuka lazima ubaki na majeraha sio ya kawaida.

Ng'ata, ng'atana, ng'atuka, ng'ang'ania. Huwezi kung'atuka ikiwa hujang'ang'ania. Na ndio maana hao wazee walikuwa wanawaambia "ng'atuka" kwa kuwa hata mnapoona watu wazima nyie bado mmeng'ang'ania kung'ata kwa mananihii hivyo viti, wazee hawajakosea walipokuwa wakiwaambia hivyo.

FF mwanzoni niliona yule alokuambia usubiri umalize Menses ndo ucomment kakuonea lakini sasa naona alikuwa na haki >100%, Unaparamia maneno hata usiyojua, na Jasusi kaeleza asili na Ukweli wa neno Kung'atuka bado huelewi! Usinambia Hormone za Menses ziko kwenye Peak maana huathiri Judgement!
 
Kwanza nianze kwa kuwashauri ndugu wanaoshiriki ktk kutathmini neno Mwl kutotumia lugha chafu ambayo kwa njia moja sio inamdhalilisha mchangiaji bali hata watu wengine wanaoshuhudia matusi mazito kama hayo.

Daiama ninapenda kurudi kwenye topic ambayo labda nitoe historia yake kidogo. Wakati ninaangalia habari 'michuzi' Niliona kikao cha NEC na kukawa na bango ambalo limeandikwa 'Mimi ninang'atuka lakin bila CCM madhubuti nchi itayumba' Kilichonisukuma kuanzisha mjadala huu ni 'Sikufahamu CCM message ile walikua wanaambia watu au wanajikumbusha wao wenyewe'.

Ukifikiria kwa makini mazingira aliyoondokea Mwl mpaka yeye mwenyewe asitumie neno jingine akatumia kung'atuka kuna message alitaka waTanzania wenzake wailewe. La kujiuliza jee message imeeleweka?

Wadadisi wa mambo wanadai kua huwenda Mwl alikusudia kua inawezekana wengine nao wakalazimika kung'atuka baadae sio kwa kupenda lakin mazingira yakawalazimisha. Kuna wanaooona kua Mwl alipambana sana mpaka akafikia hatua ya kukatishwa tamaa kwamba asingeweza kufanikiwa au kutimiza malengo ktk uhai wake possibly! kwa sababu alikua ktk wrong time and wrong place.

Upande mwengine ni ule unaodhani kua Mwl kwa hali yoyote alichukua uamuzi wa busara wa kung'atuka ukilinganisha na mtu kama Gaddafi. Any way wewe unaonaje?
 
Jasusi na wewe wote hamuelewi maana ya uasili wa maneno. Ung'atuke bila kung'ata au kung'ang'ania? Unanchekesha!

Hilo la menses nnaelewa kuwa ufahamu wenu ni mdogo sana, ngoja nikupe darsa kidogo: Kuna "practice" ambayo ilikuwa inatumika sana katika kuwaongezea wanaume afya kimwili nayo ilikuwa "recommended" na "practitioners" ambayo watu kama wewe ambao hamna uelewa hamuitumii, wenzenu "walioendelea" baada ya kuiacha kwa muda mwingi sasa wanairudisha tena kwa kasi sana na inawasaidia sana kuweka miili na akili zao sawa, nayo huitwa "blood letting" au sisi watu wa pwani huiita "chwuku au chuku" kwa Kiswahili. Nakuomba ui google hiyo uielewe ni nini na utaona kuwa Mwenyeezi Mungu aliyetujaaliya sisi kuwa nayo hiyo within our system kuwa AlhamduliLlah katupendelea sana. Nenda na wewe ukafanyiwe manual nna uhakika itakusaidia.

Maana nnakuona una mashaka na Mwenyeezi Mungu alivyotuumba, usiwe na shaka kijana "kazi ya Mungu haina makosa".

Halafu huwa mnashindwa kujenga na kujibu hoja mnarukia kumvaa mtu maungoni, halafu hata huyo wa kumvaa hamtazami kama japo mnalingana-lingana nae uzito, wengine ni ma heavy weight. Mnanchekesha!
 
Kwanza nianze kwa kuwashauri ndugu wanaoshiriki ktk kutathmini neno Mwl kutotumia lugha chafu ambayo kwa njia moja sio inamdhalilisha mchangiaji bali hata watu wengine wanaoshuhudia matusi mazito kama hayo.

Daiama ninapenda kurudi kwenye topic ambayo labda nitoe historia yake kidogo. Wakati ninaangalia habari 'michuzi' Niliona kikao cha NEC na kukawa na bango ambalo limeandikwa 'Mimi ninang'atuka lakin bila CCM madhubuti nchi itayumba' Kilichonisukuma kuanzisha mjadala huu ni 'Sikufahamu CCM message ile walikua wanaambia watu au wanajikumbusha wao wenyewe'.

Ukifikiria kwa makini mazingira aliyoondokea Mwl mpaka yeye mwenyewe asitumie neno jingine akatumia kung'atuka kuna message alitaka waTanzania wenzake wailewe. La kujiuliza jee message imeeleweka?

Wadadisi wa mambo wanadai kua huwenda Mwl alikusudia kua inawezekana wengine nao wakalazimika kung'atuka baadae sio kwa kupenda lakin mazingira yakawalazimisha. Kuna wanaooona kua Mwl alipambana sana mpaka akafikia hatua ya kukatishwa tamaa kwamba asingeweza kufanikiwa au kutimiza malengo ktk uhai wake possibly! kwa sababu alikua ktk wrong time and wrong place.

Upande mwengine ni ule unaodhani kua Mwl kwa hali yoyote alichukua uamuzi wa busara wa kung'atuka ukilinganisha na mtu kama Gaddafi. Any way wewe unaonaje?

Hapo ndipo tunahitilafiana, na Jasusi kaelezea kuwa "wazee" wakikukuta umekaa juu ya kiti na wewe hutaki kuondoka basi wanakwambia "ng'atuka" ili uwapishe kwenye kiti. Sasa fikiria hapo kuna busara gani?

Sidhani kama ni busara ung'ang'anie mpaka ung'atuke (kumbuka kung'atuka ni kuachia bila hiyari, huna budi tu ndiyo unang'atuka) Busara ni kustaafu pale unapoona umeshakosea. Nyerere katuwacha pabaya sana, ukitaka kujuwa hilo nakuomba tafuta hotuba ya Mwinyi kwa wazee wa Dar maarufu sana kama ya hatuba ya Mikuki miwili. Sisitu kikuhadithia hii nchi alivyoikuta Nyerere na alivyoiacha alipong'atuka haitoshi, kaiacha nchi ni ya mwisho duniani kwa umaskini ilhali yeye alipokabidhiwa hii nchi ilkuwa na neema kubwa sana, usisikie porojo eti kulikuwa hamna madaktari, kulikuwa hamna ma engineer, kulikuwa hamna nini sijui. Hayo mnadanganywa msiokuwepo.

Madaktari walikuwepo, huduma za afya zilikuwepo, mpaka mashuleni, mimi nakumbka tulikuwa shuleni kwetu tuna chmba cha "clinic" kabisa na kuna nurse permanent na medical officer anakuja kila wiki mara moja na dawa ni bure na hayo Nyerere aliyakuta kutoka mkoloni. lakini looh, baada ya miaka michache tu, kukawa nyang'a nyang'a, hakuna cha clinic wala medical officer wala nurse.

Wewe kama umewahi kutembelea Uingereza na ukaenda shule zao, ndivyo zilivyokuwa shule zetu hapa wakati Nyerere anapewa madaraka, usisikie, kaharibu kila kitu isipokuwa kimoja tu. Kanisa Katoliki, hilo kalienzi na kulitumikia na ndiyo maana anataka kupewa utakatifu, kwani wewe unafikiri utakatifu wanaompigia debe apewe ni kwa ajili ya nini?

Usione sasa mambo yanaanza kurudi kidogo kidogo, kubomowa ni sahali kutengeneza ni kazi.
 
Jasusi na wewe wote hamuelewi maana ya uasili wa maneno. Ung'atuke bila kung'ata au kung'ang'ania? Unanchekesha!

Hilo la menses nnaelewa kuwa ufahamu wenu ni mdogo sana, ngoja nikupe darsa kidogo: Kuna "practice" ambayo ilikuwa inatumika sana katika kuwaongezea wanaume afya kimwili nayo ilikuwa "recommended" na "practitioners" ambayo watu kama wewe ambao hamna uelewa hamuitumii, wenzenu "walioendelea" baada ya kuiacha kwa muda mwingi sasa wanairudisha tena kwa kasi sana na inawasaidia sana kuweka miili na akili zao sawa, nayo huitwa "blood letting" au sisi watu wa pwani huiita "chuku" kwa Kiswahili. Nakuomba ui google hiyo uielewe ni nini na utaona kuwa Mwenyeezi Mungu aliyetujaaliya sisi kuwa nayo hiyo within our system kuwa AlhamduliLlah katupendelea sana. Nenda na wewe ukafanyiwe manual nna uhakika itakusaidia.

Maana nnakuona una mashaka na Mwenyeezi Mungu alivyotuumba, usiwe na shaka kijana "kazi ya Mungu haina makosa".

Halafu huwa mnashindwa kujenga na kujibu hoja mnarukia kumvaa mtu maungoni, halafu hata huyo wa kumvaa hamtazami kama kama mnalingana nae uzito, wengine ni ma heavy weight. Mnanchekesha!
Bibie,
Mbona king'ang'anizi hivyo? Nimeshakwambia kule kwetu hatuna neno kung'ata wewe unang'ang'ania tu kwamba kung'atuka linatokana na neno kung'ata. Unajua nini? Shida yako ni kwamba unataka kumweka Mwalimu kwenye dhana ambazo umeshajenga mwenyewe kichwani na kuwalazisha wengine kuwa hii ndiyo portrait sahihi ya Mwalimu. Mambo hayaendi hivyo. Kuna yule mwenzako Barubaru naye kakazana kuleta uwongo eti enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna cheo cha President nje ya Ikulu. Na yule rais wa wanafunzi wa chuo kikuu waliogoma je? Aliitwa Kimulson. Nina hakika ulikuwepo 1966 pale wanafunzi wa chuo kikuu waliporudishwa nyumbani baada ya kugoma kupinga national service. Tukubali Mwalimu aliondoka mamlakani kwa hiari na hakukamatwa kwenye mtaro wa maji au shimo la panya kama yale yaliyowakuta viongozi wengine. Na hilo si jambo la kubezwa hata kidogo.
 
Nyinyi kwenu hakuna neno kung'ata kama unavyonifahamisha na nnakuelewa na nnakubali kwa kuwa mimi sijuwi Kizanaki, lakini mimi nnakupa uasili wa neno kung'atuka, halikutoka tu hewani, maneno huwa na asili na fasili zake.

Katika Kiswahili pia kuna maneno yenye asili ya lugha zingine, lakini ukiyafata asili yake utakuta katika kiswahili yamebadilika maana mfano, sarafu, hili ni neno la Kiarabu likimaanisha "chenji" lakini kwetu linamaanisha "coins au bank notes", na mtowa "chenji" kwa Kiarabu anaitwa "sarafa" lakini hili "sarafa" katika Kiswahili halipo. Sijui umenielewa? Hili neno lenyewe "chenji" lina asili ya Kiingereza "change".

Mfano mwingine ni neno la Kiingereza "Alphabet" hili maana yake ni herufi kwa Kiswahili na kwa Kiarabu huitwa "Harf" lakini "Alph-abe-t" ni majina ya zile herufi zenyewe Alif, Bee, Tee. Kwa hiyo utakuta asili ya neno Alphabet ni Kiarabu lakini kwa Kiingereza linageuka maana badala ya kuwa ni majina ya zile herufi kama ilivyo kwenye asili yake, Kiingereza linakuwa lenyewe lina maanisha herufi.

Kwa hiyo neno "ng'atuka" lina asili ya neno la Kiswahili ng'ata ingawa kwa Zanaki hawana hilo neno "ng'ata" (kama unavyosema wewe, mimi sina uhakika), ni kama vile Waswahili wana neno sarafu na hawana neno sarafa ambalo asili yake ni hiyo hiyo sarafu. Tena tukienda mbali zaidi tutakuta hili neno ng'ata lina asili nyingine kabisa (pengine hicho hicho Kizanaki unachosema wewe hakuna neno ng'ata).

Nadhani umenielewa, sina haja ya kumweka Nyerere kwenye dhanna wakati kila kitu cha Nyerere kipo wazi, ni nini cha kudhanni kwa Nyerere? "nnadhani" kuwa anataka kupewa utakatifu? na "nnadhani" kuwa anataka kupewa utakatifu kwa kulitumikia kanisa katoliki? Hizo sio dhanna huo ni ukweli na ukweli mtupu, niambie kuwa huo si ukweli. Be realistic.
 
Ngwendu, unashangaza kweli huna tofauti na wale wanaoanza kwa kunga mkono hoja 100% halafu wanamalizia kwa kukosoa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom