Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,593
Bibie,
Nakwambiaje? Katika lugha yetu hatuna neno ng'ata kwa maana ya kuuma. Kuuma ni kuuma tu. Ukishaelewa hivyo ndipo utaweza kuelewa kwamba hakuna uhusiano baina ya maneno hayo mawili. Ng'ata ni kuuma kwa meno. Lakini kung'atuka ni neno la Kizanaki ambalo maana yake ni kuondoka kwenye kiti (specific). Kwa mfano huwezi kulitumia neno hilo kwa mtu anayetoka kitandani. Ni mahususi tu juu ya kiti. Na ndiyo maana limeingizwa katika kamusi ya Kiswahili likiwa na maana ya kuondoka kwa hiari kutoka nafasi ya uongozi ( Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la pili, ukurasa wa 306)
Ni kamusi gani hiyo Jasusi? Ya TUKI au BAKITA?