Bibie,Hakuondoka kwa hiyari "aling'atuka", tafadhali usichanganye kustaafu na kung'atuka.
Soma tena nilichoandika. Usikurupuke. Hata kama hakuondoka kwa hiari, alifanya mipango ya kiungwana kuhakikisha mwingine anapasiwa kijiti cha uongozi kwa utulivu. Hilo ni jambo la kusifiwa si kubezwa. Kipi hapo usichoelewa? Na kuuma katika Kizanaki siyo kung'ata. Ni "kuruma." Achana kabisa na ung'ataji wako haihusiani kabisa na ung'atukaji. Msilazimishe mnachopenda kukiona hata kama ushahidi unawasuta.