sijasema mwanaume kutotimiza wajibu wake kwa familia,nasema mwanamke atimize wajibu wake na mwanaume atimize wajibu wake,sio kunilazimisha nikufanyie majukumu yako kwa sababu ya kudai haki/usawa.
mke alikua msaidizi, msaidizi sio hausigeli aka beki tatu... usaidizi upo kwenye naniliu banaaa
unaoa ili upate mpishi na dobi?
kupika na kufua n.k mwanamke anafanya kwa mapenzi, mapenzi aliyonayo juu ya mumewe, kupika kufua kuosha vyombo sio jukumu la mwanamke pekee...ukiona ndoa imara ujue wanandoa wameoana kwa sababu wanapendana na wanashirikiana na si kuoana ili kufuliana na kupikiana.........
ruksa kwa wanaume kunywa ila mwanamke hairuhusiwi?
kuna ubaya gani mume ukaamua kumkarangizia mkeo?
huoni inakuwa romantic?
ndoa ni vile mnavyoijenga, je unamwonaje mwenzi wako? mke/ubavu au dobi/mpishi?
au ndo aina ya mwanaume hata mtoto akilia unamuita mkeo aje ambembeleze?
hiyo nyumba mke anatoa maoni yake au akitoa maoni ndo inakuwa anataka haki?
afterall haki kumbe inatafutwa kwa kupangiana zamu za kupika?
huko sasa itakuwa ni ile ishu ya kuwatunza ma mariooo,hapa nazungumzia for a responsible women and men,kumnunulia mmeo gari ni kama zawadi tuu strong lady na hivyo haikuondeshei wewe majukumu yako ya msingi kwa mwanaume.
wanamme wenyewe wakwapi???
Hawa tunaogombea nao mabwana???
Una utani
Kwangu mwanaume yeyote anayeshindwa kuya handle majukumu yake ipasavyo na kuja kuishia kulalama hapa ni wazi ana matatizo.
Kila kitu kimeundwa/umbwa so kama ukiwa mwanaume kweli usitegemee out of the blue mwanamke afanye vile utakavyo. Ndoa na familia pamoja na muundo wake hujengwa. Mwanaume ukiwa kichwa cha familia na kutimiza majukumu yako sidhani kama mkeo atapata nafasi ya kukupanda kichwani. Nadhani hapa unazungumzia zaidi ya kuosha vyombo, unazungumzia zaidi mamlaka ya mwanaume kutotambulika. Usipojenga heshima kwa mkeo atakuheshimu kweli?
Mimi napenda Mume wangu awe na mamlaka na mwenye kuwajibika...mamlaka hayo kwa maana ya kumanage wajibu wake vyema sio mamlaka ya ku abuse
Si tu kwamba ana matatizo bali si mwanaume kabisa, avalishwe baibui na kanga.
kama ambavyo imeandikwa mwanamke ni msidizi wa mwanaume,so ni jukumu lako wewe kuhakikisha mumeo anakula vizuri na anakuwa msafi,lakini pia kumsaidia kwenye bills kama unauwezo.
Miaka mingi iliyopita iliukuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamke,mwanamke alikuwa mwanamke kwelikweli,ni kweli alikuwa MSAIDIZI WA MWANAUME,kwa hali hiyo tulijivunia sana hawa wakina dada zetu na mama zetu.Waliwapikia waume zao,waliwafulia na mengineyo mengi.Lakini siku hizi mambo yamebadilika;wanawake wanataka haki,wanataka kuwa sawa na wanaume,hawapiki tena na wala hawawafulii tena waume zao,wanachotaka waoni HAKI SAWA,eti mwanamke akipika mchana basi mwanaume apike usiku,kulea watoto eti pia iwe zamu.MIAKA HIYO WAKINA DADA WALIPIKA KAMA MAMA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAKUNYWA KAMA BABA ZAO,DUUUUUUU.Je usaw huu unaopiganiwa na wanawake ni sawa?nini faida zake na hasara zake?
mhhhhh.....kwahiyo baba akiwa njiani anrudi kutoka kazini anafikiria kuwa akifika nyumbani anazamu ya kupika,kuosha vyombo na kufua,kwangu mimi nasema moja ya vitu vinavyoleta matatizo katika ni mwanamke kufanya kazi hali inayopelekea kutotumiza wajibu wake kwa mwanaume.
Siku mtakapoacha kudai 50/50 sharing of bills na ndio sio siku tutafikiria kuwapikia 3 x a day na kuwafulia.
majukumu ya familia ni kusaidiana jamani, hebu fikiria wote mnafanya kazi,mnarudi home late mkifika mwanaume unakaa tu kwenye kochi umeshikilia rimoti, mwanamke aandae chakuka,ule aoshe vyombo na bado utahitaji na kile chakula cha ndoa, hee ist possible? majukumu ya familia ni ya wote jamani tusifanye ndoa iwe burden kwa upande wa mwanamke tu.
majukumu ya familia ni kusaidiana jamani, hebu fikiria wote mnafanya kazi,mnarudi home late mkifika mwanaume unakaa tu kwenye kochi umeshikilia rimoti, mwanamke aandae chakuka,ule aoshe vyombo na bado utahitaji na kile chakula cha ndoa, hee ist possible? majukumu ya familia ni ya wote jamani tusifanye ndoa iwe burden kwa upande wa mwanamke tu.