Miaka mingi iliyopita iliukuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamke,mwanamke alikuwa mwanamke kwelikweli,ni kweli alikuwa MSAIDIZI WA MWANAUME,kwa hali hiyo tulijivunia sana hawa wakina dada zetu na mama zetu.Waliwapikia waume zao,waliwafulia na mengineyo mengi.Lakini siku hizi mambo yamebadilika;wanawake wanataka haki,wanataka kuwa sawa na wanaume,hawapiki tena na wala hawawafulii tena waume zao,wanachotaka waoni HAKI SAWA,eti mwanamke akipika mchana basi mwanaume apike usiku,kulea watoto eti pia iwe zamu.MIAKA HIYO WAKINA DADA WALIPIKA KAMA MAMA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAKUNYWA KAMA BABA ZAO,DUUUUUUU.Je usaw huu unaopiganiwa na wanawake ni sawa?nini faida zake na hasara zake?
my dear instead of kulalama na kuanza kwenda history za kale tugange yajayo, mi kijana wangu namfundisha kupika na kazi na kumwambia ukweli dunia imebadilika kuliko kumdanganya ajione kidume kumbe wanawake wenyewe siku hizi ndio hao kama wanaume tu. tuwaambie vijana wetu ukweli kuwa dunia imebadilika na itaendelea na kuzidi kubadilika mambo ya karne zilizopita hayapo tena, we hata angalia familia za sasa zinavyolea watoto wao utachoka binti anakua msichana hata chai hajui kupika loohh!!!!!