Women...........!

Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,096
708
Miaka mingi iliyopita iliukuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamke,mwanamke alikuwa mwanamke kwelikweli,ni kweli alikuwa MSAIDIZI WA MWANAUME,kwa hali hiyo tulijivunia sana hawa wakina dada zetu na mama zetu.Waliwapikia waume zao,waliwafulia na mengineyo mengi.Lakini siku hizi mambo yamebadilika;wanawake wanataka haki,wanataka kuwa sawa na wanaume,hawapiki tena na wala hawawafulii tena waume zao,wanachotaka waoni HAKI SAWA,eti mwanamke akipika mchana basi mwanaume apike usiku,kulea watoto eti pia iwe zamu.MIAKA HIYO WAKINA DADA WALIPIKA KAMA MAMA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAKUNYWA KAMA BABA ZAO,DUUUUUUU.Je usaw huu unaopiganiwa na wanawake ni sawa?nini faida zake na hasara zake?
 
Siku mtakapoacha kudai 50/50 sharing of bills na ndio sio siku tutafikiria kuwapikia 3 x a day na kuwafulia.
kama ambavyo imeandikwa mwanamke ni msidizi wa mwanaume,so ni jukumu lako wewe kuhakikisha mumeo anakula vizuri na anakuwa msafi,lakini pia kumsaidia kwenye bills kama unauwezo.
 
Maisha ni kusaidiana, kama wanandoa wote wanaenda kazini na wamekubaliana kusaidiana kupika, kuosha vyombo, kufua etc. sio mbaya!
 
Tuliona tumetimiza haki zetu zote kwenu tena bado mnataka haki zenu kwetu tuzifanye sisi ndio maana tunataka haki sawa, tunapika, tunafua, malezi ya watoto, sasa hivi tunalipa karo za shule,kodi za nyumba ,tunawanunulia magari,

huko sasa itakuwa ni ile ishu ya kuwatunza ma mariooo,hapa nazungumzia for a responsible women and men,kumnunulia mmeo gari ni kama zawadi tuu strong lady na hivyo haikuondeshei wewe majukumu yako ya msingi kwa mwanaume.
 
Huletwa na kutoheshimiana kati ya mwanamke na mwanaume! Pia watu kuto timiza majukumu yao!
Haiwezekani utegemee kupikiwa na mtu usiye mjali, mtu usiye muachia matumizi na mambo mengine!

Siku hizi mambo yamebadilika hata wanaume tumebadilika.
 
kama ambavyo imeandikwa mwanamke ni msidizi wa mwanaume,so ni jukumu lako wewe kuhakikisha mumeo anakula vizuri na anakuwa msafi,lakini pia kumsaidia kwenye bills kama unauwezo.

Mnatakaka msaidiwe kwenye bills lazima niwe nimeajiriwa au najituma, at the same time mnataka full service at home, upike, pakua, fua, osha halafu night shift. Hata robot hafanyi hivyo.
 
huko sasa itakuwa ni ile ishu ya kuwatunza ma mariooo,hapa nazungumzia for a responsible women and men,kumnunulia mmeo gari ni kama zawadi tuu strong lady na hivyo haikuondeshei wewe majukumu yako ya msingi kwa mwanaume.
Nakapanya hata mimi naongelea haohao responsible men, kama mimi nafikia hatua ya kufanya majukumu yako kwa familia kwanini na wewe inapobidi usifanye ya kwangu ni sehemu ya mapenzi pia ,
 
Last edited by a moderator:
Miaka mingi iliyopita iliukuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamke,mwanamke alikuwa mwanamke kwelikweli,ni kweli alikuwa MSAIDIZI WA MWANAUME,kwa hali hiyo tulijivunia sana hawa wakina dada zetu na mama zetu.Waliwapikia waume zao,waliwafulia na mengineyo mengi.Lakini siku hizi mambo yamebadilika;wanawake wanataka haki,wanataka kuwa sawa na wanaume,hawapiki tena na wala hawawafulii tena waume zao,wanachotaka waoni HAKI SAWA,eti mwanamke akipika mchana basi mwanaume apike usiku,kulea watoto eti pia iwe zamu.MIAKA HIYO WAKINA DADA WALIPIKA KAMA MAMA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAKUNYWA KAMA BABA ZAO,DUUUUUUU.Je usaw huu unaopiganiwa na wanawake ni sawa?nini faida zake na hasara zake?

Miaka mingi iliyopita ilikuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamume. Mwanamume alikuwa mwanamume kwelikweli. Ni kweli alikuwa kichwa cha nyumba au mkuu wa familia. Kwa hali hiyo tulijivunia sana wakina kaka zetu na baba zetu. Walinunua chakula, mavazi na mahitaji mengineyo mengi ya familia. Lakini siku hizi mambo yamebadilika. Wanaume wanataka kulelewa kama watoto. Hawanunui tena chakula wala mavazi kwa wake zao. Wanadiriki hata kutelekeza familia zao. Mwanamke anahangaikia watoto kwa mahitaji ya chakula, mavazi, malazi, elimu n.k. Mama amekuwa mlezi wa familia. Miaka hiyo WAKINA KAKA WALIJALI FAMILIA KAMA BABA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAJIJALI WENYEWE TU, WAMEJAA UBINAFSI. Wanaume sasa wanataka kununuliwa magari na wanawake!
Je ukwepaji huu wa majukumu ni sawa? nini faida zake na hasara zake?
 
sielewi dhumuni la huu uzi, wanawake wamebadilika lakini wa kizamani bado wapo. usawa kwa wanawake unaoongelewa unahusu kutobaguliwa au kunyanyaswa kwa vile wao ni wanawake
 
ume-edit vizuri kweli :lol:
 
Hahahaha, damn right!
 
Nakapanya hata mimi naongelea haohao responsible men, kama mimi nafikia hatua ya kufanya majukumu yako kwa familia kwanini na wewe inapobidi usifanye ya kwangu ni sehemu ya mapenzi pia ,

na afanye pale tu inapobidi yeye kufanya,isiwe ni kama roster kwamba leo zamu yangu kesho yako,hilo halikubaliki kabisaaaa
 
Last edited by a moderator:
sielewi dhumuni la huu uzi, wanawake wamebadilika lakini wa kizamani bado wapo. usawa kwa wanawake unaoongelewa unahusu kutobaguliwa au kunyanyaswa kwa vile wao ni wanawake

unaweza kuniambia mwanamke anabagulia katika lipi?unazumngumziaje hizi harakati zenu za kutaka hadi baba ampeleke mtoto kliniki?
 
Nakapanya hata mimi naongelea haohao responsible men, kama mimi nafikia hatua ya kufanya majukumu yako kwa familia kwanini na wewe inapobidi usifanye ya kwangu ni sehemu ya mapenzi pia ,

unajua hiari yashinda utumwa;mtu akifanya kwa mapenzi yake haina shida,shida inakuja pale ambapo mwanamke unamfosi mwanaume afanye kama ndo wajibu wake.
 
Last edited by a moderator:
Maisha ni kusaidiana, kama wanandoa wote wanaenda kazini na wamekubaliana kusaidiana kupika, kuosha vyombo, kufua etc. sio mbaya!

mhhhhh.....kwahiyo baba akiwa njiani anrudi kutoka kazini anafikiria kuwa akifika nyumbani anazamu ya kupika,kuosha vyombo na kufua,kwangu mimi nasema moja ya vitu vinavyoleta matatizo katika ni mwanamke kufanya kazi hali inayopelekea kutotumiza wajibu wake kwa mwanaume.
 
Miaka mingi iliyopita ilikuwa ni miaka yenye ufahari juu ya mwanamume. Mwanamume alikuwa mwanamume kwelikweli. Ni kweli alikuwa kichwa cha nyumba au mkuu wa familia. Kwa hali hiyo tulijivunia sana wakina kaka zetu na baba zetu. Walinunua chakula, mavazi na mahitaji mengineyo mengi ya familia. Lakini siku hizi mambo yamebadilika. Wanaume wanataka kulelewa kama watoto. Hawanunui tena chakula wala mavazi kwa wake zao. Wanadiriki hata kutelekeza familia zao. Mwanamke anahangaikia watoto kwa mahitaji ya chakula, mavazi, malazi, elimu n.k. Mama amekuwa mlezi wa familia. Miaka hiyo WAKINA KAKA WALIJALI FAMILIA KAMA BABA ZAO LAKINI SIKU HIZI WANAJIJALI WENYEWE TU, WAMEJAA UBINAFSI. Wanaume sasa wanataka kununuliwa magari na wanawake!
Je ukwepaji huu wa majukumu ni sawa? nini faida zake na hasara zake?

nashukuru kwa kuedit,ila mbona mnaipa kipaumbele sana gari?ukimnunulia gari si kama zawadi as vile unaweza mnunulia boxer,so majukumu ya mwanaume yatabakia kuwa majukumu ya mwanaume n mwanamke atabakia na majukumu yake.
 
Huletwa na kutoheshimiana kati ya mwanamke na mwanaume! Pia watu kuto timiza majukumu yao!
Haiwezekani utegemee kupikiwa na mtu usiye mjali, mtu usiye muachia matumizi na mambo mengine!

Siku hizi mambo yamebadilika hata wanaume tumebadilika.

so unataka kuniambia kuwa kutokuheshimiana huko ndio kumepelekea wanawake kudai haki sawa na wanaume?
 
Back
Top Bottom