Habari za muda tena, heri ya siku ya mapinduzi.
Moja kwa moja kwenye mada, jana nikiwa katika harakati za kutafuta mkate wa siku muda wa saa 4 asubuhi nilianza kuhisi maumivu jicho la kulia kadri muda ukivyozidi kwenda hali ilizidi kuwa mbaya nikaona hata isiwe shida acha nijipumzishe na kazi nielekee home kwa ajili ya matibabu.
Sasa nikiwa narudi home kutoka Makumbusho nikaona sio mbaya nipite Zahanati japo kupata dawa. Muda huo nipo maeneo ya UDSM hapo, nikashuka kwenye gari na kuingia Zahanati ya chuo. Nikiwa katika benchi la kusubiri matibabu nikaona kama watu wawili wakiwa wamevimba macho mmoja alivimba yote, hata haikunishtua.
Ikafika zamu yangu nikaingia kwa Daktari nilipofika tu baada ya kumkabidhi fomu ya NHIF akaanza kuandika dawa then akaniuliza kuna kingine tofauti na macho ikabidi nijibu hapana. Akasema nenda Duka la Daw kachukue dawa.
Nimefika Duka la Dawa nikapewa dawa kilichonishangaza zaidi nikaona ile meza ya pale dirishani kumejaa dawa za macho tu. Akili ikanambia acha kufatilia mambo yasiokuhusu. Nikachukua zangu dawa chaap nikaelekea home kupumzika.
Nimefika home mida ya saa 12 jioni mara kidogo namuona jamaa yangu nae amerudi analalamika jicho linauma nikwambia hata mimi linazingua sema nenda hospital ukapate dawa.
Jamaa akanambia shida ni nini mbona familia ya Mzee fulani watu zaidi ya watatu nao wanashida hiyo hiyo.
Sasa ombi langu kwa Wizara kama kuna shida tupeane taarifa tusisubiri ugonjwa uenee sehemu kubwa pia Wanajamii waelekezwe namna ya kujikinga na maambukizi hayo.
Naomba kuwasilisha