Wizara ya Afya yatoa taarifa ya kuenea kwa ‘Red Eyes’. Yawataka Wananchi kuchukua tahadhari

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Wizara ya afya imewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa macho mekundu (Red eyes) Maambukizi ya Kirusi kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” iliyoibuka nchini hivi karibuni.

Hayo yamesemwa leo Januari 15, 2023 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof Pascal Ruggajo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa awali ya ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuathiri watu wengi nchini.

Prof. Ruggajo amesema dalili ya ugonjwa huo ni pamoja na macho kuwasha, kuchomachoma, kuuma, macho kutoa machozi na kutoa tongo tongo za njano.

"Taarifa za uchunguzi zinaonesha Maambukizi ya Kirusi hiki kwenye ngozi ya juu ya gololi ya jicho yajulikanayo kitaalamu “Viral Keratoconjunctivitis” ni maambukizi yanayosambaa kwa kasi kubwa. Hakuna tiba maalumu kwa ugonjwa huu na hata bila tiba dalili huisha zenyewe ndani ya wiki mbili". Amesema Prof Ruggajo.

Prof. Ruggajo amesema mwenendo wa ugonjwa huo unaonyesha kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wanaofika katika Vituo vya kutolea huduma za afya wakiwa wanasumbuliwa na ugonjwa huo.

“Katika kipindi cha Desembe 22, 2023 hadi Januari 11, 2024 kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huu kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya matibabu, kwa mfano katika mkoa wa Dar Es Salaam kuna wagonjwa wapya 869 huku hali ya kawaida katika kipindi cha mwezi Desemba 2023 kulikuwa na wagonjwa 17 pekee” amefafanua Prof. Ruggajo.

Aidha amesisitiza suala la usafi ni jambo muhimu katika kuzuia maambukizi kusambaa kwa wengine Kutokana na tabia ya ugonjwa huu kusambaa kwa kasi, maambukizi haya huleta mlipuko ambao husambaa kupitia kirusi kwa asilimia zaidi ya 80%.

Prof Ruggajo amewashauri wananchi kutokutumia dawa zisizo rasmi na ambazo hazijaandikwa na daktari kwa wakati huo na kutotumia dawa za macho anazotumia mgonjwa mwingine ili kuepuka madhara kwa kuwa dawa za macho ni tofauti na kwa matumizi tofauti.



 
Viral conjunctivitis ni nini?
Viral conjunctivitis ni ugonjwa wa jicho unaosababishwa na virusi. Hutokea pale virusi wanapoambukiza eneo la utando wa jicho, unaojulikana kama conjunctiva. Dalili zake ni pamoja na macho kuvimba, kutoa machozi, na kuwa na kutokwa kwa usaha mweupe. Ni muhimu kuepuka kugusa macho yako na kunawa mikono mara kwa mara ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Ikiwa una wasiwasi au dalili, ni vyema kumwona daktari wa macho.

Husababishwa na nini?
Viral conjunctivitis husababishwa na aina mbalimbali za virusi, ikiwa ni pamoja na adenovirus, enterovirus, herpes simplex virus, na wengine. Hata hivyo, adenovirus ndio chanzo kikubwa zaidi cha viral conjunctivitis. Inaweza kuambukizwa kwa urahisi kwa njia ya kuambukizana na majimaji yanayotoka kwenye macho ya mtu aliyeambukizwa au kutoka kwa vitu vilivyoguswa na mtu huyo.

Viral conjunctivitis husabisha upofu?
Kwa kawaida, viral conjunctivitis haijasababishi upofu. Hata hivyo, inaweza kusababisha usumbufu mkubwa na kupunguza uwezo wa kuona kwa muda mfupi. Ikiwa una dalili za viral conjunctivitis na wasiwasi kuhusu afya yako ya macho, ni muhimu kumwona daktari wa macho. Mara nyingi, dalili hupungua na kupotea baada ya muda.

Tiba yake ni ipi?
Matibabu ya viral conjunctivitis mara nyingi hulenga kupunguza dalili na kuharakisha uponyaji, kwani hakuna dawa maalum ya kutibu virusi vinavyosababisha ugonjwa huu. Hata hivyo, wataalamu afya ya macho wanaweza dawa ya matone ya macho ya antihistamine, Dexaneo, ili kupunguza ukavu na kuwasha. Kwa watu wenye dalili nzito, daktari anaweza kutoa matibabu mengine kulingana na hali yao.
Ni muhimu pia kufuata ushauri wa daktari, na kuepuka kugusa macho ili kuzuia kuenea kwa maambukizi. Ikiwa una mashaka au dalili zinaendelea,

Je kuna njia ya Asili ya kutibu Viral conjunctivitis?
Kuna njia za asili zinazoweza kutoa unafuu au kusaidia katika kurejesha afya ya macho wakati wa viral conjunctivitis. Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa njia hizi hazitibu moja kwa moja virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. Baadhi ya njia za asili zinazoweza kusaidia ni pamoja na:-
a) kujifukiza
b) kunawa uso na maji yaliyo changanywa na chumvi
 
Habari wakuu.
Kuna wimbi la ugonjwa wa macho, kuvimba na kuwasha na kuwa mekundu sijui chanzo ni nini wenye kufahamu sababu watatueleza zaidi.

Nmeshawaona wagonjwa zaidi ya 10 ndani ya siku 2(jana na leo). Kuna mtu wangu wa karibu kanijulisha pia kaupata, tuwe makini na kama kuna tahadhari zozote za kuchukua tufahamishane.

Wizara ya Afya Tanzania
 
20240116_154858.png
 
Back
Top Bottom