Wingu na Mbingu

Dada Judy we hongera, nimefurahi kujua
wacha nandae kamera, kumbukumbu jiwekea
tigo mpe bila kura, kama livyokwishatuambia
mapenzi yawe imara, nje asahau tokea!
Lol...

hayo mambo ya sodoma mpendwa, achana nayo na Muogope Mungu,

Glory to God!
 
1. Kumpata mwenza bahati, siku hizi ni adimu,
Nakupongeza kwa dhati, machangu sikuhujumu,
Shika sana lake shati, peke yake ndo adhimu,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

2. Maisha kama safari, uchumba kituo kimoja,
Mwanzo hauna shubiri, wambea najikongoja,
Chai yenye sukari, maisha yenye faraja,

3. Uvumilivu muhimu, mapenzi geuka ndimu,
Kila siku si karamu, waweza ishiwa hamu,
Tabia mfano wa bomu, tahadhari ufahamu

1.
Nimepata wa thamani, ni hakika si majungu,

Mwingine sitatamani, nimefunga moyo wangu,
Sikupotea ramani, nimezikubali pingu,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
2.
Kila nionapo wingu, sikosi kuona mbingu,
Huwezi ingia mbingu, bila liingia wingu,
Wingu liko na mbingu, mbingu zina mawingu,

3.
Hayawi hayawi yawa, thelathini siku zawa
Sio nyingi kama chawa, zi nyepesi kama buwa,
Kwa sala na zote duwa, maombi yamejibiwa,

4.
Tangu tulipozianza, ndoto za baba na mama,
Ni mengi tumejifunza, tukabakiza kuhama,
Na sasa twende kufyonza, tamu iliyofichama

5.
Mwaka ule si karibu, subira ndio mtaji,
Tele hayo majaribu, yasiyopozwa na maji,
Imara kama bawabu, makini kama hujaji,

6.
Nyakati nayo majira, na zama zimetimia,
Mapenzi haya imara, silaha kuu ya ndoa,
hazijalishi ngawira, mapendo tumekamia,

7.
mpira ulipoupiga, niliepa nisidake,
kwa mengi ulinikoga, japo hunayo makeke,
na sasa nimejibwaga, hirimu wangu nishike,

8.
za mwizi hazikawii, zetu walizikamia,
pamoja nayo bidii, ya maombi kuazimia,
agizo sasa kutii, la ndoa na familia,

9.
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,

10.
tuijenge hiyo nyumba, yenye kujaa vicheko,
watoto nao kuumba, mbinguni tupate heko,
wala tusije kuyumba, kwani tunao upako,

11.
udumu cha nyumba kichwa, mimi ni wako ubavu,
bidii ipite mchwa, ushinde wote uchovu,
nyuma tusije kuachwa, kwa Yesu uko wokovu

...........................Glory to God!

kwenye nyekundu, you have made my day,.................. kwenye blue, its noted and saved for future use,................ ila fumbo la mbingu na wingu linahitaji watu wa bakita waje watudadavulie....................... manake hata gaijin kajaribu ila naona bado bakita wanahitajika zaidi hapo,.............. by the way, hongera sana mwali wetu, ................... ila nov mbali mno jamani si na kiu itaisha??.............. fanyafanya basi angalau uirudishe nyuma hiyo shughuli japo miezi miwili, eeh??.................. tafadhali mpendwa............... au mwenzetu huna haraka "kufyonza tamu iliyofichama"??...............

Mungu akutangulie katika mipango yako.................. imebidi tu nikuombee aisee japo ningetamani hapo kwa Naiman pasomeke "AK"............... teh teh..................
 
1. Kumpata mwenza bahati, siku hizi ni adimu,
Nakupongeza kwa dhati, machangu sikuhujumu,
Shika sana lake shati, peke yake ndo adhimu,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

2. Maisha kama safari, uchumba kituo kimoja,
Mwanzo hauna shubiri, wambea najikongoja,
Chai yenye sukari, maisha yenye faraja,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

3. Uvumilivu muhimu, mapenzi geuka ndimu,
Kila siku si karamu, waweza ishiwa hamu,
Tabia mfano wa bomu, tahadhari ufahamu
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

mkuu, kumbe na wewe umo??................ hongera sana kuwakilisha!!....................
 
...Hongera sana MJ ila kumbuka "
An Ounce of Action is Worth More than A Ton of Theory or Shayiri la Beti 25"

.......Simple like that...GIVE LOVE....GET LOVE....The more you love, the more you get love

Ile misimamo yako ya kubalehe na kisingo iweke pembeni kidogo....usijemdindia Naiman mpaka pambio la kusifu na kuabudu ndio "Rungu" litangwe .....hahahaaa

BTW: Ni jambo jema sana mtu kupata mke/Mume....hakika ni jambo jema na Hongera tena
 
1. Kumpata mwenza bahati, siku hizi ni adimu,
Nakupongeza kwa dhati, machangu sikuhujumu,
Shika sana lake shati, peke yake ndo adhimu,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

2. Maisha kama safari, uchumba kituo kimoja,
Mwanzo hauna shubiri, wambea najikongoja,
Chai yenye sukari, maisha yenye faraja,
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

3. Uvumilivu muhimu, mapenzi geuka ndimu,
Kila siku si karamu, waweza ishiwa hamu,
Tabia mfano wa bomu, tahadhari ufahamu
Hongera na Mungu akujalie uvumilivu na upendo.

Ndoa zingine maziwa, huishi wewe kunyonywa,
Miaka inavyozidia, wazidi kudanganywa,
Hata kile kilojaa, huishia kumumunywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Kwa dini au sheria, harusi yenu hufanywa,
Ahadi mtazitoa, mkatae kusengenywa,
Na mafunzo mtapewa, na wazazi mkakanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ukweli hujifichua, wakati mnap0ofinywa,
Maslahi kupungua, kila pembe mnaminywa,
Hali zinapotitia, watu rahisi kugawanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ndugu na hao jamaa, ya uongo hutawanywa,
Hubakia kuvizia, yatangazwa yasiyofanywa,
Na mitego husambaa, wategwe wasiokanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Hodari walioamua, milele kutokugawanywa,
Kisha wakajititimua, wasiwe watu wa kunywa,
Fedha kudundulizia, waache tena kunyonywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Kuwekeza wakitua, vinginevyo wakatonywa,
Mke anapoamua, hataki tena kunyonywa,
Mbele akavichukua, huku mume anasonywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Mme chumvi hudaiwa, na chake kikamenywa,
Bahili mke akawa, sio wa kumumunywa,
Mme nguvu hulegea, asitake kutekenywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa.

Ndoa jambo maridhia, ila pasiwe kunyonywa,
Nikahi kitu murua, mtu asiposengenywa,
Nyumba hujititimua, na watu msipogawanywa,
Ndoa zingine kunyonywa, na huku unadanganywa
 
...Hongera sana MJ ila kumbuka "
An Ounce of Action is Worth More than A Ton of Theory or Shayiri la Beti 25"

.......Simple like that...GIVE LOVE....GET LOVE....The more you love, the more you get love

Ile misimamo yako ya kubalehe na kisingo iweke pembeni kidogo....usijemdindia Naiman mpaka pambio la kusifu na kuabudu ndio "Rungu" litangwe .....hahahaaa

BTW: Ni jambo jema sana mtu kupata mke/Mume....hakika ni jambo jema na Hongera tena

nimekupata vizuri sana mpendwa

Mungu akubariki sana
 
1.
Nimepata wa thamani, ni hakika si majungu,

Mwingine sitatamani, nimefunga moyo wangu,
Sikupotea ramani, nimezikubali pingu,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
2.
Kila nionapo wingu, sikosi kuona mbingu,
Huwezi ingia mbingu, bila liingia wingu,
Wingu liko na mbingu, mbingu zina mawingu,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
3.
Hayawi hayawi yawa, thelathini siku zawa
Sio nyingi kama chawa, zi nyepesi kama buwa,
Kwa sala na zote duwa, maombi yamejibiwa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
4.
Tangu tulipozianza, ndoto za baba na mama,
Ni mengi tumejifunza, tukabakiza kuhama,
Na sasa twende kufyonza, tamu iliyofichama
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
5.
Mwaka ule si karibu, subira ndio mtaji,
Tele hayo majaribu, yasiyopozwa na maji,
Imara kama bawabu, makini kama hujaji,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
6.
Nyakati nayo majira, na zama zimetimia,
Mapenzi haya imara, silaha kuu ya ndoa,
hazijalishi ngawira, mapendo tumekamia,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
7.
mpira ulipoupiga, niliepa nisidake,
kwa mengi ulinikoga, japo hunayo makeke,
na sasa nimejibwaga, hirimu wangu nishike,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
8.
za mwizi hazikawii, zetu walizikamia,
pamoja nayo bidii, ya maombi kuazimia,
agizo sasa kutii, la ndoa na familia,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
9.
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
10.
tuijenge hiyo nyumba, yenye kujaa vicheko,
watoto nao kuumba, mbinguni tupate heko,
wala tusije kuyumba, kwani tunao upako,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
11.
udumu cha nyumba kichwa, mimi ni wako ubavu,
bidii ipite mchwa, ushinde wote uchovu,
nyuma tusije kuachwa, kwa Yesu uko wokovu
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
12.
Asante wote wapendwa, kwa maombi nazo dua,
Ni kweli hamkushindwa, shetani kumkemea,
Upendo uliopandwa, hitaji kuu la ndoa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

wapendwa,

pamoja na kuzidiwa na majukumu mengi kikazi, Mungu aliyajibu maombi tena vizuri sana. mchumba wangu anaitwa Naiman na ni mzaliwa wa Iringa. kama mjuanvyo masuala haya yana logistics nyingi na hivyo kukamilisha yote yaliyo ya muhimu inahitaji muda. hadi sasa mengine hayajakamilika. hapo katikati nilibahatika kupata scholarship ya kuripoti chuoni september mwaka huu na hivyo mtaona kuna kibarua cha kupangilia mambo hapo, kupata ruhusa na likizo ya masomo kazini na kuandaa harusi na wakati huohuo kutakiwa kuwa chuoni. so baada ya panga pangua, natarajia kwenda chuoni kwanza na kisha kurudi nyumbani november kwa ajili ya kufunga ndoa.

Mungu awabariki sana,

Glory to God!

Mie nimefurahi sana Judith maana umeweza kuuthibitishia umma wa JF kwamba ile thread yako ya mwanzo haikuwa usanii. Sasa tunasubiri kwa hamu kuu mtutangazie harusi, harusi ambayo nadhani itakuwa ya kwanza kuhudhuriwa na wanaJF wengi. Kila la heri katika safari yenu.
 
nashukuru sana mpendwa, bila shaka sitawasahau wote jamvini. aliyedhani ni usanii tusichoke kumuombe. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayekuwa juu yetu. mkononi mwake tunapata kushinda na zaidi ya kushinda.

Glory to God!
 
Hongera sana miss Judy
Mungu azidi kukuongezea
Nguvu na baraka zaidi katika
Mipango yako...

My dear nimeanza kulifikiria
hilo gauni la harusi hahaha lol
Kila lakheri na masomo yako pia.
 
9.
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

yaani alishike vizuri rungu
kwa sababu ana kazi kubwa ya kukubikiri au.......................................
 
nashukuru sana mpendwa, bila shaka sitawasahau wote jamvini. aliyedhani ni usanii tusichoke kumuombe. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayekuwa juu yetu. mkononi mwake tunapata kushinda na zaidi ya kushinda.

Glory to God!

tatizo langu ni kuwa ulikuwa wapi hadi ukashtuliwa na Pakajimmy?..........................
 
Hongera sana miss Judy
Mungu azidi kukuongezea
Nguvu na baraka zaidi katika
Mipango yako...

My dear nimeanza kulifikiria
hilo gauni la harusi hahaha lol
Kila lakheri na masomo yako pia.

asante sana mpendwa
nawe nakutakia kila la heri kwa kila mkono wako unalotia bidii kulifanya
Mungu akubariki sana
 
tatizo langu ni kuwa ulikuwa wapi hadi ukashtuliwa na Pakajimmy?..........................

Nilikuwa nafikiria the same...................

wapendwa, majibu ya maswali haya yako kwenye post no. 88 ukurasa wa tano na ni kama ifuatavyo:
[h=2]
icon1.png
Re: Mchumba wa Miss Judith![/h]samahani sana wapendwa,

nimechelewa kuiona hii thread hadi imefika ukuasa huu!! nimefurahishwa na PJ kwa kukumbusha ahadi yangu ya kuwajulisheni nini kinaendelea baada ya maombi mazito ya siku 30. kipekee namshukuru sana Mayasa kwa kujitahidi kuwaweka sawa wengine. ubarikiwe sana dada. pia nawashukuru wote kwa upendo huu mkubwa mliouonyesha kwangu, nasema asanteni sana.

kwa kifupi, pamoja na kuzidiwa na majukumu mengi kikazi, Mungu aliyajibu maombi tena vizuri sana. mchumba wangu anaitwa Naiman na ni mzaliwa wa Iringa. kama mjuanvyo masuala haya yana logistics nyingi na hivyo kukamilisha yote yaliyo ya muhimu inahitaji muda. hadi sasa mengine hayajakamilika. hapo katikati nilibahatika kupata scholarship ya kuripoti chuoni september mwaka huu na hivyo mtaona kuna kibarua cha kupangilia mambo hapo, kupata ruhusa na likizo ya masomo kazini na kuandaa harusi na wakati huohuo kutakiwa kuwa chuoni. so baada ya panga pangua, natarajia kwenda choni kwanza na kisha kurudi nyumbani november kwa ajili ya kufunga ndoa.

pia kuna thread inaitwa Wingu na Mbingu, ni shairi linalotoa majibu niliyoahidi, baada ya kumsoma PJ kwenye thread ya loliondo ilinilazimu kukaa chini kwa dakika chache ili niwape feedback kwa mtindo wa shairi.

nawapenda wote wapendwa na mbarikiwe sana na Bwana

Glory to God!

basi Mungu na ashukuriwe
atupaye sisi kushinda
basi ndugu na uimarike
uzidi kuitenda kazi
hata mwisho uifikie
furaha ile ya milele

post hii inapatikana https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/148512-mchumba-wa-miss-judith-5.html
 
Back
Top Bottom