Wingu na Mbingu

Mwalimu naomba tofauti ya hayo maneno mawili

Mwenyewe Miss J kasema

Huwezi kuifikia mbingu bila kukutana na wingu lakini najua kuwa unaweza Likuta wingu bila ya kuhusiana na mbingu!

Pia anasema wingu lipo pamoja na mbingu lakini mbingu inayo mawingu (plural)

Sasa ni dhahiri kuwa mbingu Ina upper hand kwenye huu uhusiano
 
asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

Mie nimeona hapo kwenye blue............ nitakutafuta unifundishe mashairi.............. hongera MJ

Ndoa bila rungu ni kama govi na mzungu
Hivi ndiyo ilivyo kwa wanaojua mizungu
Tena ukutane na rungu liloota magugu
Utajisikia hamu kushinda ile ya njugu
Kama hunisadiki waulize machangu

Shairi umelisoma, na pia umefahamu
Kama bado hujakoma, jina lako chakalamu
Yakikukuta ni noma, iweke yako awamu
 
Mwenyewe Miss J kasema

Huwezi kuifikia mbingu bila kukutana na wingu lakini najua kuwa unaweza Likuta wingu bila ya kuhusiana na mbingu!

Pia anasema wingu lipo pamoja na mbingu lakini mbingu inayo mawingu (plural)

Sasa ni dhahiri kuwa mbingu Ina upper hand kwenye huu uhusiano
Definitely hapa Miss Judy ndio Mbingu...!!
 
Mwenyewe Miss J kasema

Huwezi kuifikia mbingu bila kukutana na wingu lakini najua kuwa unaweza Likuta wingu bila ya kuhusiana na mbingu!

Pia anasema wingu lipo pamoja na mbingu lakini mbingu inayo mawingu (plural)

Sasa ni dhahiri kuwa mbingu Ina upper hand kwenye huu uhusiano

Wingu = Cloud
Mbingu = Sky

Wingu likiwa jeusi ni dalili ya mvua
Mbingu ikiwa clear (blue sky) maana ni vipindi virefu vya jua!
 
Panaweza kua na Mbigu pasipo wingu, ila hapawezi kua na wingu pasipo mbigu
Vp mwalimu hapa nipo sawa?

Very much so ...:))

Yaani kwa Hisabati za primary moja tunaiita ni set na nyengine ni ki-subset chake tu.
 
Dada Judy we hongera, nimefurahi kujua
wacha nandae kamera, kumbukumbu jiwekea
tigo mpe bila kura, kama livyokwishatuambia
mapenzi yawe imara, nje asahau tokea!
Lol...
 
Dada Judy we hongera, nimefurahi kujua
wacha nandae kamera, kumbukumbu jiwekea
tigo mpe bila kura, kama livyokwishatuambia
mapenzi yawe imara, nje asahau tokea!
Lol...

Kwenye bold ninashaka wewe u dini gani
Ndoa na mapenzi si mashaka ikafanyiwa matani
Tigo utoe wewe yeye atampa ya pajani
Wewe huna ya pajani labda ukachonge japani
 
Thread yangu imefanya kazi...Sometimes kukumbushana si mbaya!
Hongera MJ, JAPO SIJAMALIZA KUSOMA unachomaanisha!

Kaka hongera sana kwa kukumbushia maana bila wewe MJ (Duh sometimes nikiiona hii naskip heartbeat!) asingefunguka!!

MJ wa ukweli, karibu ukaribie
Hakuna raha ya kweli, kupata umpendae
Mwenye mapenzi ya kweli, mpende akupendae
Karibu kwenye himaya, ufurahie mapenzi

Ladha ya penzi kupendwa, sikuijua mapema
Nikaanza na kutendwa, wakaumiza mtima
Kupenda nisipopendwa, kuwa ya kwangu alama
Karibu kwenye himaya, ufurahie mapenzi

ANGALIZO: Ushikwapo shikamana, usijilegeze kuwa wapendwa ukabweteka..........mapenzi ni kupendana wifi!
 
1.
nawashukuru wapendwa, shairi mmelipenda,
nitaheshimu kufundwa, juu ya kulila tunda,
sitakinai kupondwa, nimeshazoea mlenda,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

2.
nakushukuru kifrogu, vionjo kunitilia,
wachangamsha blogu, wengine wakimbilia
hata walio na sugu, somo litawaingia,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

3.
wa pili ule ubeti, ni wazi pasi kiwingu,
kwa wima ama kuketi, utajua nini wingu,
fikira iliyo ya dhati, itaing'amua mbingu,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

4.
paka jimi mchokozi, kweli nilikuwa bize,
mimi sijawa mpuuzi, yalojiri nisiwajuze,
bila ule udokozi, kazi nisizibakize,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

5.
wote mloniwosia, tazingatia ushauri,
nisijebaki mkia, maisha kutahayari,
sitakuwa mmbea, kwa kila ilo habari,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

6.
ni mengi yalitokea, na jibu kuchelewa,
shule ya ng'ambo tokea, mipango nililemewa,
baraka nizopokea, sio za kuambiwa,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!

7.
harusi iko novemba, hapo sasa ni kamili,
nitavaa na kilemba, nitang'arisha na kandili,
mapambo nitajiremba, tena yale ya ukwel
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
 
Kama unataka kunificha jambo basi liweke kwenye shairi..
Anyway, kama hutajali tuwekee kwenye muundo wa Riwaya ili na sisi tusio wapenzi wa Mashairi tuelewe basi Bandugu...
 
Kama unataka kunificha jambo basi liweke kwenye shairi..
Anyway, kama hutajali tuwekee kwenye muundo wa Riwaya ili na sisi tusio wapenzi wa Mashairi tuelewe basi Bandugu...

Tanmo, hujambo kaka? nimekumiss kule mahali, riwaya nilikuwa natunga zamani, siku izi napenda zaidi mashairi. usihofu siku moja nitakufundisha kutunga na kuyaimba

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!
 
Kwenye bold ninashaka wewe u dini gani
Ndoa na mapenzi si mashaka ikafanyiwa matani
Tigo utoe wewe yeye atampa ya pajani
Wewe huna ya pajani labda ukachonge japani

mkristo mimi kwa dini, na wala sina matani
ila
kuna siku jukwaani, dada judy alighani
tigo apewe mwandani, maelezo kiundani
sijehubiri waini (wine), yeenda jipoza majini!
 
mkristo mimi kwa dini, na wala sina matani
ila
kuna siku jukwaani, dada judy alighani
tigo apewe mwandani
, maelezo kiundani
sijehubiri waini (wine), yeenda jipoza majini!

mpendwa, muogope Mungu, sijawai kusema kitu kama hicho iwe kwa shairi ama vinginevyo.

ubarikiwe sana

Glory to God!
 
Back
Top Bottom